Mac Alpho
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 14,020
- 28,069
Onana hana baya yule, ila ni wazi kwamba aina yake ya uchezaji haifit kwenye team ya kipumbavu kama hii.Kipa adake vizuri Ajax, adake vizuri Inter Milan, eti aje kuwa mbovu Manchester United, hell no! Timu ni mbovu
Sisi mashabiki wa Man Utd ni mabingwa wa kutafuta wachezaji wa kuwatupia lawama badala ya ku address tatizo halisi la hii team, tulianza na CR7 licha ya kutufungia magoli mengi, tukaja kwa De Gea licha ya kutubeba sana pale golini tukamuacha kwaaababu za kijinga (footwork), tukaja kwa FRED (huko aliko saaahivi anakichafua sana tu) wengine wengi.
Sasahivi tumehamia kwa Onana bila kujiuliza kwanini alicheza kwa kiwango kikubwa alivyokuwa AJAX na INTER MILAN kisha aje kwetu aonekane mbovu.
Ile interview ya CR7 ilisema uozo wote pale UTD.