Tajiri ndio anaewafundisha wachezaji kuruka ruka uwanjani!?
Nenda kaziangalie BRIGHTON Newcastle Brentford na Tottenham zilinganishe na MANCHESTER ni nani katumia hela kwenye usajili!?
Ni nani ana kikosi cha bei mbaya!?
Ni nani alieoza UWANJANI kati yetu sisi wenye mwalimu ten HAG na wao .
Ipi timu isiyokuwa na maajabu yoyote UWANJANI.
Kisha utasema TATIZO ni matajiri hapo!?
Wacheni kuishi kwa kukariri matajiri hawachezi MPIRA.
Ten hag kwanza hata jicho la usajili hana ni anabahatisha mnooo.
Kuoandisha viwango wachezaji pia hawezi.
Tunamlaumu sancho kila siku kumbe sancho ni kakosa mwalimu tu.
Maguire nae kakosa mwalimu tu.
Kwa ten hag ikiwa ronaldo kafeli nani mwengine atakaefaulu!?
Matic pogba mata wote kawatoa na sasa kamtoa FRED.
Kisha nenda katazame aliowaleta na tazama kazi zao wanazozifanya uwanjani kisha linganisha na wachezaji aliowatoa ni sawa!?
Kauza ZIDANE IQBAL kwa bei ya mkaa na juzi kamtoa kipa bora kabisa matej kovar.
Na sasa anataka kipa mwengine na KIUNGO je pana kocha hapo!?
Msimu uliopita UNITED imebebwa na dua tu sasa sijui msimu huu kama mungu ataziskia pia dua zetu au atawaskia Chelsea