Kosa kubwa alilolifanya Ten Hag ni kutosikilia ushauri wangu, siku moja kabla ya mechi nilimpigia simu na kumshauri game Vs Liverpool asithubutu kuwachezesha Rafael Varane na Casemiro maana Liverpool wakiwaona uwanjani ni kama vile umekua umewatonesha kile kidonda cha kufungwa na Madrid, vyovyote itavyokua wataforce kupiga comeback ili wasonge mbele kwenye Uefa.
Jamani Liverpool sisi hata siku moja hatujawahi kuwa na ugomvi na nyie, hata maugomvi yenu na Madrid tunaomba muwe mnamalizana wenyewe kwa wenyewe, kutuingiza sisi kwenye maugomvi yenu ni kama vile mnatuonea bure tu.
Sijapenda kwa kweli jinsi mlivyotufanyia.