Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Huyu mzee hapana kwa kweli sio kwa style ya man u yule hafai kabisa huwezi kumuuza Rafaeli halafu ukatumia mabeki kama kina Blanket, kazi yao kurudisha mpira nyuma. Kwangu mimi hakuna kipindi nilikuwa nachukia kuangalia mpira kama kipindi cha Van gal yaan mpira mnacheza na kumiliki nyie haladfu mwishowe mnafungwa.
Van Gaal aliuza fringe players wote wa Man united akabaki na wale waliokuwa regular starters tu chini ya Ferguson bila kujua kuwa kundi kubwa sana la wale mabwana lilikuwa limezeeka sana.

Mbaya zaidi wachezaji wote aliowasajili walishindwa kudeliver mpaka msimu wake wa pili ndiyo walianza angalau kuingia kwenye mfumo wake.

Kuna kipindi aliamua kumchezesha Rooney kwenye midfield it was so painful.
 
Emirates Kuna atmosphere Kali , pia huwa tunafungulia Busta Zote sababu ya sapoti ya mashabiki , wachezaji wanakimbia Sana , flow ya pass huwa Ni kubwa Sana .

Kaangalie mechi ya Arsenal vs Newcastle iliyoisha 0-0

Alikuja na 4-3-3 tupishane , walipoona Moto unakuja tu ,for the first time Newcastle wakabadili mfumo 5-4-1 , na kupoteza muda ndipo wakapata Draw

Silaha yenu Ni kaunta attack tu, hamna uwezo wa kubattle Midfield , kimbembe kitaanzia hapo .
Wale mashabiki shoga ?
 
Maguire, Bailly, Telles, Williams, Martial hawa kwa pamoja hatukosi pound 100M majira ya kiangazi.

We jamaa nikikumbuka ulivyosimama na mdogo wako Rashford bega kwa bega kipindi kile tunataka kumla kichwa humu ndani naishia kutabasamu tu. Sasa hivi apewe mkataba wa kudumu yeye na Shaw.
Ukimuuza Maguire inabidi tusajili beki mwengine, Angalau wa 4 wanahitajika. Same kwa martial akiondoka tunahitaji striker wawili badala ya mmoja. Bailly, Telles na Williams wote wataingia sokoni, maybe na Elanga pia hasa Sancho akirudi atakua hana Umuhimu.

Cha muhimu ni timu iuzwe kabla ya dirisha kubwa na Tufuzu UEFA, itasaidia dirisha lijalo.
 
Weka head to head kwa hii misimu mitano kaka tuone nani mchumba tafadhali
Arsenal kipindi cha Ole ndo mlikuwa vizuri kwetu
Screenshot_20230116-190757_LiveScore.jpg
 
Tusitishike kwa arsenal kupata, ushindi dhidi ya totenham jana, sie tuombe wachezaji wetu waendelee na spirit ya kunyoosha kila timu inayokutana na sisi ili tuendelee kubeba point 3.

Naamini kabisa baada ya crystal palace msiba mzito tunauacha pale pale emirates. Mda unavyodhidi kwenda i believe anything can happen and time will tell.
 
Ukimuuza Maguire inabidi tusajili beki mwengine, Angalau wa 4 wanahitajika. Same kwa martial akiondoka tunahitaji striker wawili badala ya mmoja. Bailly, Telles na Williams wote wataingia sokoni, maybe na Elanga pia hasa Sancho akirudi atakua hana Umuhimu.

Cha muhimu ni timu iuzwe kabla ya dirisha kubwa na Tufuzu UEFA, itasaidia dirisha lijalo.
Kuna aina ya wachezaji hawafai kuwa backup hasa hasa mtu kama Maguire in-longrun anaweza kuleta shida ktk dressing room. Spurs inaweza kuwa timu sahihi sana kwake endapo pande zote mbili zitaelewana. Namuona akifanikiwa sana kiuchezaji wake endapo atajiunga nao.

Tayari alishapewa mamlaka makubwa sana ndani ya kikosi tokea 2020 mpaka 2022 chini ya Ole halafu ghafla anapoteza ushawishi ndani ya muda mfupi kuanzia dressing room mpaka uwanjani. Sio mtu sahihi kuendelea kuwepo kikosini kuanzia msimu ujao.
 
Back
Top Bottom