Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Sema tusiende kichwa kichwa...Ajax wanataka €100m..kitu ambacho naona sio..tuende nao taratibu ili dogo aje kwa dau ya chini ya hapo ili pia tumwondolee pressure.
Makubaliano binafsi Antony na sisi tayari wamebaki Ajax kukubali ofa ya pili ikitumwa. Hawa ndio aina ya wachezaji tunapaswa kusajili mwenye hamu ya kuja kucheza United.
 
Binafsi sijaelewa nini kafanya paka dirisha linafungwa. Timu haina technicians kwa build up phase na idea yake ni kuplay out from the back, De gea, Varane, Bissaka, Lindelof are so weak with the ball, unadhani mtacheza long kick paka msimu unaisha?
Timu nyingi siku hizi zinapress high line, na ukikutana na physical teams that means intensity haiwezi kuwabeba kwa game zote 38.
 
Jinsi Lisandro anavyojitoa uwanjani ndivyo Captain anapaswa kucheza.

Lile li-engereza likienda Chelsea inabidi Lisandro apewe kile kitambaa.
 
Mkuu Bruno jana amecheza vizuri sana.
 
Jinsi Lisandro anavyojitoa uwanjani ndivyo Captain anapaswa kucheza.

Lile li-engereza likienda Chelsea inabidi Lisandro apewe kile kitambaa.
Tupo slow sana kuwaondoa flops wetu..

Mtu kama Maguire ni wakuondosha kikosini chapchap..kuendelea nao ni yaleyale ya kujitafutia ugumu kuwa-offload kama ilivyo kwa Phil Jones.
 
Tupo slow sana kuwaondoa flops wetu..

Mtu kama Maguire ni wakuondosha kikosini chapchap..kuendelea nao ni yaleyale ya kujitafutia ugumu kuwa-offload kama ilivyo kwa Phil Jones.
Hawa wajinga wapo kama 10 hivi wanamaliza mikataba yao mwezi wa 6 mwakani wote wanapaswa kuondoka hata wakicheza vizuri kiasi gani msimu huu wametudhalilisha msimu uliopita.

Mf. Rshford jana kafunga goli zuri ila bado inapaswa aondoke kwenye sura mpya United. Luke Shaw, Degea, Jones, Ronaldo, Fred, Dalot, Chong, Tuanzebe sioni haja ya kuendelea kubaki na hawa wachezaji. Ten Hag akijiloga kumpa hata mmoja mkataba tutaendelea na makapi yale yale ya hovyo.
 
Bodi ilikataa Phil Jones kuuzwa. Na juzi ilikataa ofa ya Chelsea ya kumchukua Maguire.

Kuna maamuzi kocha anaamuliwa na bodi.
 
Vipi Bado hatujacheza na LiverKuku!!!?
 
Vipi mkuu. .... Matokeo yalikuwaje
 
Nyie kenge mmeshaanza kuwa na maneno maneno humu

Wkend sio mbali
 
Yes ila aache kujiangusha angusha kijinga jinga,na kupoteza muda bila sababu.

Mfano ile ya kung'ang'aniana mpira baada ya goli ya salah ni uf*****ing.
Alichofanya Bruno baada ya goli la Salah ndiyo captain anapaswa kuwa na tabia kama zile. Liverpool baada ya goli la kusawazisha walishaanza ku-gain momentum na ambacho kilikuwa kinatokea ni ku-press zaidi kwasababu goli lingine linawahakikishia alama.

Ile ni North-West Derby ni vizuri kuwa na captain anayejua umuhimu wa kushinda ile mechi pamoja na yote alama 3 kwetu zilikuwa za muhimu sana. Kuuchukua mpira ni mbinu ya kuwa-upset wachezaji wa Liverpool. Sisi ndiyo tulikuwa tunaanzisha mpira na Bruno alikuwa na haki ya kuchukua mpira.

Kama uliona pia Martial kwenye mpira wa kona dk za mwishoni alimuelekeza ball-boy atulie kwanza asimpe mpira yote ni katika mbinu ya kupunguza kasi ya mchezo na dk ziende.

Kwa wapenzi wa soka wengi tunapenda shithousery!
 
Bodi ilikataa Phil Jones kuuzwa. Na juzi ilikataa ofa ya Chelsea ya kumchukua Maguire.

Kuna maamuzi kocha anaamuliwa na bodi.
Sunk cost fallacy. Wanaamini wamewekeza fedha nyingi hawako tayari kukubali kula hasara.

Ralf aliwahi kusema kila wakiwa training anaona kundi kubwa sana la wachezaji ila ukifika muda wa kupanga timu ya kucheza haoni watu wa kuamini uwanjani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…