Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

tatizo lilianzia kwa mwalimu aliyepita hakuweza kuweka msisitizo juu ya mambo hayo matatu mbele ya hadhara na hata kwenye viwanja vya mazoezi, amekuja mwanadamu anayehitaji sifa hizo tatu wachezaji wanahisi uzito kubadilika.

bahati mbaya sana kwa wakati huu upepo umewavumia vibaya wachezaji wetu kwani hakuna chochote watakacho kilalamikia mbele ya hadhara au kwa kuvujisha taarifa kama wafanyavyo baadhi yao wakaaminiwa na kuungwa mkono kama ilivyotokezea hapo nyuma (kuanzia Ole hadi mourinho)

kwa sasa presha imehamia kwao na kwa ushahidi wa hilo

  • jaribu kufuatilia mahojiano ya maguire hapo juzi (yeye kama nahodha inasemekana aliitisha mkutano rasmi wa wachezaji na kocha kuzungumzia mwenendo wa timu)
  • fuatilia majibu ya bruno baada ya kuvumishiwa tetesi za kuhamia barcelona, umeona wapi mchezaji wa ulaya kujibizana na tetesi za magazeti ya kufungia maandazi
  • fuatilia post ya fred hapo juzi akikemea taarifa za uongo zinazosambazwa juu yake
  • fuatilia post ya rashford hapo juzi
  • fuatilia maneno ya msemaji wa pogba alipokanusha habari za kwamba mteja wake amefikia makubaliano ya kupewa mkataba mpya wa paundi laki 5.

kwa sasa wana machaguo mawili yanayowakabili nayo ni:
  1. kufuata matakwa ya mwalimu (kocha ameendelea kusisitiza pressing 😛😛😛
  2. au kuendeleza ukaidi ndani ya uwanja baadae wapambane na matusi ya mashabiki na pundits.
tumemsikia evra akitoa duku duku lake
roy keane kama kawaida yake ameendelea kumpa za uso harry maguire
lou macari naye amebwatuka
Sahivi wachezaji hawatamani hata huyo RR apewe consultancy role.

Wamekaliwa shingoni.

Ukisoma comments za mashabiki kwenye page za Man Utd utajua jinsi gani wachezaji wana hali ngumu.
 
Tatizo ni kocha, System yake ya uchezaji.Wachezaji ni wale wale walio kochiwa na Carrick kabla ya kocha huyo Kutua.Mbona wakati wa Carrick walikuwa hawapotezi mipira?
Carrick ame coach mechi ngapi.?

Wakati Ole alipewa kazi ya interim alishinda mechi ngapi?

Leo hii huyo Carrick mngeshamkataa.
 
Mwalimu Hana mbinu.Ana technique Moja tuu ambayo wanafunzi wameshindwa kuielewa yeye ana force tuu,Kocha asiforce aangalie na aina ya wachezaji alio nao.Kwanini Rb Leipzig walifit mfumo wake vizuri na Man UTD wanaonekana kuto kufit??? Kaangalie mechi za Leipzig wakati RR ni kocha,mipira ilikuwa haipotei potei ovyo,mpira safi unao vutia,mwendo wa kupress tuu.

Mechi za Carrick zilikuwa dhidi ya Villarreal Arsenal.
Akiwa Leipzig alikuwa na wachezaji sahihi.

Sahivi United ana wana mitindo na mafaza. Hakuna mchezaji kule.
 
Mwalimu Hana mbinu.Ana technique Moja tuu ambayo wanafunzi wameshindwa kuielewa yeye ana force tuu,Kocha asiforce aangalie na aina ya wachezaji alio nao.Kwanini Rb Leipzig walifit mfumo wake vizuri na Man UTD wanaonekana kuto kufit??? Kaangalie mechi za Leipzig wakati RR ni kocha,mipira ilikuwa haipotei potei ovyo,mpira safi unao vutia,mwendo wa kupress tuu.

Mechi za Carrick zilikuwa dhidi ya Villarreal Arsenal.
Unakua professional player na huelewi kupress basi ni tatizo kocha yuko vizuri shida wachezaji wavivu sana na hawataki kuelekezwa wanacheza wanachojua wao.
 
Mimi naamini wachezaji wanazingua sana maana ukiwa tu mchezaji tena professional kama wa united huhitaji hata kocha jamani kujua kupiga pasi mbili tatu kati yenu huhitaji kabisa. Hawa jamaa wameridhika tu halafu viburi sana ukiona RR kasema jana kuna timu ndogo tu lakini wachezaji wanapambana sana unaona kabisa wanakimbia mda wote ila hawa wetu wao kutembea tu akipoteza mpira anatembea.

Wana mentality ya aina gani sijui hawa jamaa hawapambani kabisa hata transition ya mpira kwenda mbele ni slow sana, angalia aston villa wakipata mpira speed yao kuelekea golini ndo utajua hawa wachezaji ni weupe tu tusafishe wote yani asibaki mtu pale misimu miwili ijayo.

watu wanalipwa 80k na wanavuja jasho dakika 90 wapuuzi wanapokea 200k kazi kukuna pua na kuzurura uwanjani hii sio sawa.
 
Diogo Dalot

FIx1JmwXsAYcHs8.jpg

FIx1J8vXwAcpF6l.jpg
 
Having given specific triggers for the Wolves game, Rangnick simplified his instructions on how to press Aston Villa and added detail on what he wanted from his #mufc players when in possession, an aspect that some in the squad felt was lacking before #mulive
[@lauriewhitwell]
 
Kweli kabisa msimu huu nimeangalia mechi zote mpaka sasa mechi tuliyocheza vizuri ni ya Leeds tu na hizo dk chache kwenye mechi ya Crystal Palace, hadi nikajisemea "United are back" kumbe ni danganya toto tu wachezaji walimsikiliza mwalimu mechi hiyo basi.

Mechi nyingine tulizocheza vizuri kidogo ni ya Newcastle pale OT na game ya Spurs basi hizo nyingine tunashinda tu kwasababu hii ni Manchester United anatokea mchezaji atafunga tutashinda.
Mimi nafikiri game tuliyocheza vizuri ni game yetu na Chelsea.

Mechi zingine tumecheza katika standard yetu ya laissez faire nafikiri uchezaji wetu huu ulitupa mafanikio makubwa mechi yetu na Liverpool maana tulikipata tulichokuwa tumekipanda kwa muda mrefu tuliporuhusu wachezaji wetu wacheze kulingana na walivyoamka.
 
Nikiangalia lists ya wachezaji walioachwa na josep guardiola pale kwa majirani miaka miwili ya mwanzoni ya utawala wake then uwalinganisha na hawa waliopo kwetu nabaki na mshangao dhidi ya wale wanaomnyooshea kidole mwalimu juu ya uwezo wake, hivi jurgen klopp alisafisha wachezaji wangapi mpaka alipojenga timu yenye kuogopesha.kwa timu kubwa mfumo ni wachezaji, Tuchel thomas alipata bahati ya mtende kwa kurithi timu iliokuwa na udhaifu wa kukosa nidhamu ya ushindi lakini kuhusu ubora wa wachezaji ulikuwepo kwa maeneo mengi ya uwanja.
Maybe mchezaji anayetakiwa kubaki United ni De Gea tu !!
 
Toka tufungwe na Liverpool sijawahi tena kutamani kuangalia mechi za united
 
Msimu huu hakuna siku hii timu imepata ushindi kwa wepesi "comfortable win"
Jana ilikua kama tunacheza na Bayern, kumbe Aston Villa.
 
Back
Top Bottom