twitter nimefollow account nyingi sana kupitia sekta tofauti zikiwemo michezo, siasa, teknoloji, history n.k
ila moja kati ya account inayonivutia sana ni ya huyu mwanadada anayeitwa
Maram AlBaharna, ni mshabiki wa manchester united kama mimi, amehitimu Economics and Management Student at London School of Economics,ana silaha nyengine muhimu ambayo mimi sina nayo ni data analyst (hii elimu imenivutia sana ila sijawa tayari kujifunza)
....jinsi anavyofanya analysis za wachezaji na kiuchezaji kwa timu husika hususani man utd hunifanya nijiulize mara mbili mbili.
je mimi naangalia mpira au napoteza muda kwenye tv?
baada ya kumalizika mechi ya southampton amekuja na bandiko litakalofuata nitakalolishusha kidogo kidogo kwa lugha ya kiengereza, sitoweza kuliweka kwa lugha ya kiswahili kwa kuhofia kuliharibu kimaana.
kwa muda mrefu humu ndani tumekuwa na mijadala yenye kujirejea mara kwa mara, mara tatizo ni beki, mara tatizo ni DM, mara tatizo ni winga na blah blah nyenginezo.
je tatizo letu kubwa ni lipi.
nifuatilie kidogo kidogo
fuentte mtafute huyo dada hapo twitter hutojutia