Bora tumemkosa, hata mimi mwanzo nilikuwa natamani aje OT ila ukiangalia uhalisia angekuja kwenye timu yetu yeye ndiyo angekuwa mfalme pale na ingeleta shida kuja kumpata mchezaji wa level zake ili asijione yeye ndiyo yeye katika timu. Ni kama ishu ya Pogba mwanzo alitusumbua sana ila kwa ujio wa Bruno imesaidia kumuweka sawa na kutokujiona yupo juu ya klabu.
Messi ni mchezaji mkubwa sana kucheza kwenye timu yetu hii, ni lazima ukubali hili. Timu anayoenda anakutana na World class players karibia kikosi kizima, the likes of Neymar (ana rekodi yake matata) Mbappe, Ramos. Huko kunamfaa zaidi au timu nyingine ni Man. City (nimefurahi wamemkosa).