D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,633
- 121,022
hii ishu ya juan mata tulishawahi kuizungumza na PTER humu ndani, kwa ufupi man utd wana mipango naye juan mata baada ya kustahafu soka ila bado haijajulikana ni kazi gani wanataka kumpa.Mata angepitishwa hivi tu, sioni umuhimu wake, kama wazee mbona tunae Cavan anatosha kulea vijana.
- kocha kama ilivyo kwa michael carrick
- balozi wa klabu
hivyo basi uwepo wa juan mata klabuni unatokanwa zaidi na sababu za kiuongozi kuliko sababu za kiuchezaji. Juan mata anaonekana kuwa ni mwanadamu mwenye taswira ya upole, uvumilivu, aliyeridhika, mpinga fitna(hajawahi kuanzisha mgogoro wowote dhidi ya mwalimu), mwingi wa ihsan na ikhlaq nafsini mwake.
Naweza kusema huu ni msimu wa nne kumshuhudia Juan akikosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza lakini sijawahi kukutana na malalamiko yeyote kutoka kwake kupitia media tofauti ukilinganisha na wachezaji wengineo wenye changamoto inayoshabihiana na ya kwake kwa kuanzia utawala wa mourinho ambaye tuliamini havutiwi na uchezaji wa mata (rejea sakata lake pale chelsea) mpaka huu utawala wa Ole gunnar. Si hivyo tu pia juan amekuwa akichezeshwa nafasi asiyoipendelea kiuchezaji tokea asajiliwe manchester united lakini ameendelea kujitolea kwa moyo wake wote pindi anapopewa nafasi.
nimeona vugu vugu kubwa la usajili wa wachezaji vijana kutoka Spain kwa miaka hii ya karibuni kama vile:
- alvaro fernandez: mlinzi wa kushoto kutoka real madrid na amepandishwa timu ya miaka 23 licha ya kuwa na miaka 17.
- marc jurado: anatokea barcelona, amezaliwa miaka 16 iliopita
- armau puigmal: anacheza timu ya miaka 23 (hajaongezewa mkataba mpya hivyo ameshaondoshwa)
- Mateo Mejia
- alejandro ganacho: miaka 16 na amesajiliwa kutoka atletico madrid