Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Huyu Mata wa nini tena...au ni ile ya "Kijiji ni lazima kiwe na wazee"??
Kijiji lazima kiwe na wazee, hii kazi wakiachiwa watoto tupu wanaweza kuharibu shughuli. Acha wapewe madini na waliowatangulia.

Kibongobongo tunachukulia soka ni kwenye pitch tu ila kiukweli mpira una mambo mengi yanaendelea nyuma ya pazia.

Mata kubaki ni habari njema, timu yetu imejaa vijana wadogo sana, kuwa na mchezaji mwenye influence kubwa kama Mata kwenye timu ni muhimu sana. Hili naliona hata kwa De Gea tusitegemee akauzwa miaka ya karibuni, De Gea ni moja ya wachezaji waliocheza na vizazi vingi United pia kimafanikio ya PL ndiyo watu wa mwisho katika kikosi cha sasa kushinda taji la PL na babu Fergie.

Kwa sifa anazopewa Mata na wachezaji wenzake unaona kabisa anastahili mkataba mpya kuendelea kubaki kwenye dressing room ya United.
 
I got you.
 
Kama unakumbuka vizuri kiwango cha David Degea kilianza kushuka msimu wa 2017/18 na hata alipoenda world cup ali-perform hovyo sana.

Siri kubwa nyuma yake aligombana na kocha aliyemjenga anaitwa Emilio Alvarez. Jamaa aligoma kuendelea kumfundisha David na ndiye aliyemfundisha toka yuko Atletico Madrid.

Ole akampa kazi Richard Ortis. Huyu ndiye technical staff wa kwanza kupewa kazi na Ole baada ya kuwa kocha kamili june, 2019. From there, David hajawahi kuwa golikipa mzuri ana makosa ya kiufundi mengi sana. Huyu Richards Ortis anaweza ku-click na Dean ila sio David.
Hii ndo proof ya jinsi Ole alivyo clueless.

Hajui nini anafanya.
 
Objective ya kumuongeza mkataba ni ipi? Sioni kama Ole anaweza kumtumia. Ndiyo yale yale ya Odion Ighalo anasainiwa ila hatumiki.
Lee Grant kaongezwa mkataba pia
Screenshot_20210702-210553_Man%20Utd.jpg
 
mnunuzi sijamuona labda tuwajaribu wolverhampton
Hahahahaa Degea hakuna timu inayoweza kumudu mshahara wake ($375k/weekly). Naamini ataleta instability eneo la golini msimu ujao, Ole atarudia ujinga wake wa kutokujua golikipa wake #1 ni yupi. Hii itawafanya wote wawili wawe wabovu zaidi watapoteza kujiamini wote.
 
So far, hii michuano ya euro kuna bwana mdogo wa ki-Belgiji anaitwa Jeremy Doku ameni-surprise sana. Sikuwahi kumfahamu kabla ila ana kipaji kikubwa sana.
leo ni mara yangu ya kwanza kumuona huyo bwana mdogo
amenikumbusha work rate ya shaun right phillips.
mbio, dribbling, nguvu, 1 vs 1 pia ni mzuri sana
 
Back
Top Bottom