Hii superleague wanataka iweje?..tofauti na UCL?
Yes, Hii ni ajenda yenye msukumo wa tamaa ya kutaka kupiga pesa kutoka kwa wamarekani wanaomiliki vilabu vya Manchester United, Liverpool na Arsenal. Hili ndio genge lililo nyuma ya huu mpango. Anayenishangaza ni boss Juventus (Andrea Agnelli) naye yuko nyuma ya huu mpango na ni mjumbe wa bodi ya UEFA pia.
Ukisoma mpango wao unaonyesha utakuwa na timu 15 za kudumu kutoka ligi kubwa 5 barani ulaya. Na tayari makubaliano ya awali na siri wamefikia na vilabu vyote 15 na vitaanza kuthibitisha kuanzia jumapili ya leo.
Mfumo wake wa uchezaji utafanana na ule wa mpira wa kikapu (NBA) sio kama huu tuliouzoea wa kawaida yaani kutakuwa na timu 15 za kudumu halafu 5 zitaingia kwa mfumo wa kushindania jumla watakuwa na timu 20. Zitatengwa kwa makundi mawili kila kundi timu 10. Washindi wanne wa juu ktk kila kundi watasonga mbele. Mechi zitakuwa zinachezeka katikati ya wiki na fainali itachezwa weekend baada hatua zote kuisha.
Timu zilizo ktk orodha ni Manchester United, Arsenal, Liverpool, Chelsea, Tottenham, Manchester City, Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, Juventus, Inter Milan, AC Milan, PSG, Atletico Madrid na Borussia Dortmund.
Mpaka kufikia leo ni PSG tu ndio aliyegoma kabisa kufanya makubaliano ya awali bosi wao (Nasser al-Khelaifi) ni mjumbe wa UEFA na pia ni mtendaji mkuu wa beIN Media Group hawa wanamiliki haki za kurusha matangazo ya UEFA kwa hiyo maslai yake yanaguswa.
Business proposal ya hii super league inaonyesha watakuwa wanaingiza €4B kwa mwaka kupitia matangazo mara mbili ya kiasi wanachotengeneza UEFA kwa sasa ( 2018/2019 walipata €2.4B). Vilabu huku vitakuwa vinalamba mpunga mara mbili ya wanaoupata sasa.
Mwenyekiti wa hii super league atakuwa Florentino Perez (Real Madrid) makamu watakuwa wanne Joel Glazer (Manchester United), John W. Henry (Liverpool), Stan Kraonke (Arsenal) na Andrea Agnelli (Juventus).
Hata hivyo vyama vingi vya soka vinapingana na agenda ya hawa wamarekani wakiwemo waingereza na wajerumani. Inaomekana hawatatoa vibali kwa vilabu kushiriki huko.