Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ila kwa yote kajitahidi sana kuleta umoja kwenye timu miaka mingi sana ilikuwa inshu hakuna kocha ambae angeweza kumudu vurugu za pogba na wakala wake kama sosha

Kila siku nitampa sifa hiyo na uchezaj umekuwa mzur hii timu kufunga goli 5 ilikuwa inshu lakin kwa sasa jambo la kawaida sana watu wanakula hadi 9
Akipunguza kutolewa kwenye nusu fainali atakuwa pia ametupigisha step kimtindo..
 
★Two youngsters making their debuts within a week.

That's what Manchester United is all about

#GGMU

manutd |
IMG_20210222_114250_714.jpeg
IMG_20210222_114250_743.jpeg
 
★Bruno Fernandes is only the third player in Europe's top five leagues to reach double figures for both goals and assists this season.

️ 14 goals
10 assists

What an impact

Bruno Fernandes has scored and assisted in a league game for the seventh time this season, more than any player across Europe's top five leagues this season★

#GGMU

manutd |
IMG_20210222_114225_408.jpeg
 
Mkuu Daemusin binafsi nilipenda kusitokee timu ikatawala epl kama anavyojaribu kufanya Mr Pep kwa sasa maana itaondoa kule kutokutabirika kwa bingwa wa ligi msimu hadi msimu.
Mtizamo wangu kama ilivyokuwa kwa wengi wasiopenda liverpool kuchukua kombe msimu ule ni kwa sababu ya kale kaheshima tulikobaki tunajivunia kwa sasa (bingwa wa kihistoria wa epl) maana tuko mbali sana na uwezekano wa kuchukua kombe mbele ya hawa watabe city and co. Hivyo,pamoja na utawala wa City chini ya Pep hata akusanye mara 10 bado hataweza kuivunja hii rekodi. Wakati huo huo kwa upande wa liverpool ni kinyume chake na tungekuwa yatima kwa kusimangwa humu na wale wajuaji.

Kwa upande mwingine Pep amebadili mwelekeo wa uwekezaji kwenye soka la uingereza hasa kwa vilabu vinavyowania mataji kwa nadharia mbili;
1. Kwa sasa kutengeneza wachezaji wa academy ni kwa ajili ya kuuza na kutunisha mfuko ili ununue galactico kwa ajili ya kujiimarisha zaidi.
Hivyo hii nayo inafanyika kwa minajili ya kibiashara zaidi kuliko kuiimarisha timu husika.
2. Waarabu wa city hawategemei faida itokanayo na mpira/klabu kujiongezea kipato bali kuitumia hii platform ya city kujitangaza na kufanikisha madili mengine muhimu zaidi ukilinganisha na wale wamarekani wa liverpool na united wanaotegemea kuvuna kutoka kwenye timu zao.


nakumbuka katikati ya msimu wa 2018/2019 humu ndani kulizuka mjadala mkubwa sana uliojaribu kuangazia au kuonyesha ni upi upande sahihi ambao mashabiki wa manchester united wanapaswa waegemee kwa muda.
  1. wengine tulitaka bingwa awe liverpool bila ya kujali historia kubwa ya kiupinzani iliopo
  2. wengine walitaka bingwa awe manchester city licha ya kwamba hawa pia ni wapinzani wetu (wanaonekana kuwa ni wapinzani dhaifu kihistoria ya mafanikio)
kwa nini liverpool awe bingwa: Nilielekeza hoja zangu maeneo yafuatayo
  1. squad depth ya liverpool ni dhaifu hivyo basi hawatokuwa na nguvu ya kuleta ushindani kwa misimu miwili hadi mitatu kwa wachezaji walionao, itakuwa ni rahisi kuwaondoa kileleni pindi tutakapokuwa serious kwa soka la ushindani.
  2. FSG wanafanana na familia ya glazer kimatumizi na uendeshaji wa timu hivyo niliamini liverpool hawatokuwa na jeuri ya kufanya usajili wa nguvu kwa kila msimu ukilinganisha na manchester city
  3. aina ya wachezaji anaowapenda klopp ni wale wasiotambulikana kwa kiasi kikubwa sana kwenye soka la bara la ulaya(mwenyewe hujificha kwenye hoja ya mfumo), tofauti na guardiola anayevutiwa zaidi na top players waliokwisha tengenezwa huko watokwako.
kwa ufupi sikutaka kuwa mtumwa wa historia za wazungu na kwangu niliangalia zaidi nyakati tulizopo, man city nilianza kuwaogopa tokea siku ile waliofanikisha usajili wa robinho kutoka real madrid na baadae yaya toure kutoka barcelona

Siwezi kumuogopa klopp asiyekuwa na uhakika wa bajeti ya usajili huku nikiendelea kumuombea mazuri guardiola mwenye uwezo wa kumsajili athan ake kwa paundi millioni 40.

====================
fuentte, Bello na wadau wengineo niliowasahau bado munaendelea kuwa na msimamo wa kuwaombea mazuri zaidi manchester city kuliko liverpool hii inayosajili mchezaji wa daraja la kwanza?
 
Back
Top Bottom