Hii comment nilichelewa kuiona.
Unajua binaadam tuna tabia zinazo tofautiana sana, kuna baadhi ya watu wameumbwa kupinga tu, wenyewe wakiamua kupinga jambo wanapinga tu hata kama jambo hilo lina manufaa kwao.
Kuna baadhi ya watu humu wameamua kumkataa tu (kupinga) Sorkskjaer, tena kwa bahati mbaya hata hojazao si za msingi, wenyewe wanapinga tu.
Kuna mwamba moja huyo yeye huonekanaga sana humu siku tukifungwa, comment yake yeye ni "Bado haja fukuzwa?"
Yani yeye tamaa yake ni kuona kilasiku tuna sajili makocha wapya na kuwafukuza, bila kujua kila kocha huja na falsafa yake, hivyo kila siku tutakua tunaanza upya.
Binafs namkubali Sorkskjaer, kinyume na kumkubali, mimi ni mguuni wakuvumilia makocha.
Hata tulipo mtimua Van gar nilikerekwa sana na kuwaambia mashabiki wenzangu kwamba tutakaa muda mrefu bila mafanikio ya maana, na kweli mpaka leo.
Neema imetokea tume mpata kocha (kijana wetu) alie anza kufufua matumaini lakini chaajabu kuna raia zinampinga.
Tubadilikeni wadau mchizi (Sorkskjaer) kaanza kuleta matumaini tumuungeni mkono.