Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

★Thomas Tuchel is interested in becoming Manchester United manager and Manchester United are interested in hiring him, according to Le Parisien ️★

#GGMU

manutd |
IMG_20201206_194019_248.jpeg
 
★Kwni swla la kusajili namba 10 ndio tusiongee kuwa hajui kufanya mabadiliko yaliyo Timamu acha hivyo bana kuna vitu anavifanya 100% perfect na tunaviona eh hichi katumia akili ila kunavingine nividogo sana kwa akili ya binadam na Bado ndivyo ana boronga mfano Mzuri swala la Sub nazani kati ya Subs alizofanya na zikaleta mafanikio i mean zakueleweka kwenye 100 ni 16 tu kwa Makadirio ya haraka tukienda makadirio ya kuturia hata hizo 13 hafikishi mimi namuelewa huyu jamaa ila kuna muda anaborongo tuache mahaba Mkuu★
Uwanja huru mkuu hebu anza kulist sub alizoboronga kwenye ligi msimu huu.
 
Siku ya game ya UEFA baada half time wamelud uwanjan camera zote kwa fred.. walikuwa wanajua huyu Nyekundu inamhusu.. ilibid awe benchi
Muda huo ole wangu kabet tu kamaa jamaa hatoki na red
Msimu huu mechi tulizo dondosha points kihalali ni mbili tu ile ya Tottenham Hotspur na ya Brighton & Hove ila zingine zote tumesare au kufungwa kwa uwezo mdogo wa safu yetu ya ufundi.

Kuna muda mpaka unajiuliza hivi hawa jamaa huwa wanafanyaga nini viwanja vya mazoezi Carrington? Huoni ubunifu wowote ule ktk timu.

Tunafungwa magoli yale yale kila siku. Mfano kuna angle kila ikitokea free-kick lazima David afungwe huoni safu ya ufundi ikichukua hatua.
 
Msimu huu njia nyeupe sana si Uefa wala EPL kwa ubora wa wachezaji tulionao wangepata mwalimu anayejua kazi yake tungefagia kila kombe.

Mapungufu pekee tuliyonayo kwa sasa tuna mabeki wawili tu wa kati wanaoweza kucheza mechi zaidi ya 20 bila majeraha, nje ya hapo hatuna kisingizio kila idara ina watu wanaoweza kishinda taji lolote lile.
 
Itoshe kusema OLE anatembelea nyota ya Bruno Fernandez.
bila bruno sshv tungekuwa tunafukuzana na arsenal nafasi ya 16 huko..OLE IS NOT COMPITENT!!

Bado hayuko vzr kwny kufanya maamuzi gani na kwa wakati gani.Hes shit
 
MAshabiki wa Manchester bwana !

Timu ikishinda wame shinda wachzaji ila ikifungwa au kusare sio wachezaj ni ole na bench lake la ufundi

Sometimes tuwe tuna appreciate jamani khaa

Weekend tulikua down 1-0 ht ole katoa Cavan na DVB na sub zake zote zime Fanya kitu eg mata laasiast ,Bruno kaasisst ,ford kafung
 
Msimu huu njia nyeupe sana si Uefa wala EPL kwa ubora wa wachezaji tulionao wangepata mwalimu anayejua kazi yake tungefagia kila kombe.

Mapungufu pekee tuliyonayo kwa sasa tuna mabeki wawili tu wa kati wanaoweza kucheza mechi zaidi ya 20 bila majeraha, nje ya hapo hatuna kisingizio kila idara ina watu wanaoweza kishinda taji lolote lile.
Hivi si juzi tu Hapa analyst wote walitaribia Man United hatoboi kwenye kundi la Rb leipzig na Psg? Leo limekuwa kundi laini? Hivi kuna kundi gumu kushinda letu Uefa msimu huu?

Nyie jamaa nimewavulia kofia.

Na hao wachezaji tulio nao wametoka wapi? Mbinguni? Si kocha amewasajili?

Lvg alikuwa na Di maria top Assist wa ulaya nzima, Mou akamnunua Mikhi top Assist wa Ulaya nzima kwa mara ya pili ila wote hawakutusaidia, james Rodriguez alikuwa offered kwetu, mchezaji alieongoza ulaya nzima kwa kutengeneza nafasi ila ole hakumnunua, pia walikuwemo wachezaji wa ndani kama Grealish na Madison wote walikuwa linked na Man united, ni Epl proven, wote hao Ole aliachana nao akamchukua bruno, alijua Ole anachotaka ni nini.

Kuhusu free kick hili ni graph linaonesha jinsi gani tulivyo improve
ifefe26c2m361.png

Msimu uliopita tulikuwa wa mwisho zaidi (timu bora zaidi) kwenye kuruhusu nafasi za vichwa, na yote hii ni yule musiyempenda Maguire ndio ame tu improve.

Na hata msimu huu tupo wa 18, japo tumeruhusu magoli 2 ya Corner mechi 2 zilizopita ila still ni ya 3 kwa ubora wa kuokoa mipira ya Vichwa.

Ukiondoa Timu ya Mou iliokuwa na magiant tupu msimu ule wa ibra miaka yote toka Fergie aondoke tulikuwa vibaya kwenye mipira ya vichwa, ilifika stage timu hata ikipata foul katikati ya uwanja watu wanajaa golini kwetu, kila foul ni kona.

Na hata mechi iliopita na west ham walipiga cross nyingi sana, pogba, maguire na lindelof wamefanya headed clearence nyingi.
 
kile kitendo cha kumpiga kichwa mchezaji ni red card, binafsi sijaona utofauti wowote wa tukio alilolifanya na lile lililofanywa na martial dhidi ya spurs.
kuna rafu fulani alicheza jamaa akapewa kadi ya njano (refa alichemsha)
kipindi cha pili unarudi tena na wanadamu wawili waliokwisha onywa mara tatu na referee tena unacheza na neymar mjanja.
inashangaza sana
Kimsingi pale refa aliongozwa zaidi na busara. Hiyo ni mara ya kwanza kwa tukio kama lile kuisha na kasi ya njano. Siku ile PSG wanacheza ile mechi yenye kadi 5 nyekundu Neighmar alitolewa kwa kumgusa tu mchezaji mwingine shingoni. Kibinadamu ni ngumu kumlaumu refa maana kuna referree hawapendi mchezo uishe mapema kama ile game yetu na United, ya Martial vs Lamela.

Hiyo pia nimeiona jana. Kuna rafu Le Celso alicheza ikapelekea free kick. Ile ilikuwa kadi ya pili ya njano kwa Lo Celso lakini refa kamwita tu na kumwambia "bwana mdogo umeme ninao hapa, jiangalie".
 
Ole lawama zote zinamuangukia yeye...sijui ni kwa nini hawezagi kujiongeza, yaani hata sisi mashabiki tulikuwa tunajua kabisa yule Fred anakula umeme muda wowote nashangaa sana kuona kamrudisha 2nd half na bado kafanya makosa ya wazi refa anamuonya ila yeye OLE alihisi anacheza na southhampton akaamua liwalo na liwe may be atapata come back..
Ole bado sana. Ni sawa na mtoto kamaliza tu kunyonya anapewa dozi ya makande na magimbi. Molde iko sawa na Wycombe Wanderers au Yeovil town, daraja la ngapi sijui huko. Sema mpaka mje mkubali huo ukweli wakati mshakuwa wenyeji wa Europa League kama Asteno au AC Milazo.
 
Ole hajui game management. Usimtetee.

In terms of team selection, substitutions bado sana. Hana impact yeyote.

Ni moods na forms za wachezaji ndo zinamuokoa kwa sasa ni Bruno.

Na hata ukiangalia mpira tunaocheza bado mbaya sana.

Kila mara tunatanguliwa kufungwa, the comes comeback ambayo hatutakiwa kujivunia.
Kweli kabisa. Kwenye game yenu na West Ham juzi nilimsikia hata mtangazaji mmoja akisema Bruno anapokuwa uwanjani kila mchezaji anaanza kuhisi uhai. Unaweza predict kuwa bila Bruno mechi 6 United inaweza kuwa wapi.
 
Msimu huu njia nyeupe sana si Uefa wala EPL kwa ubora wa wachezaji tulionao wangepata mwalimu anayejua kazi yake tungefagia kila kombe.

Mapungufu pekee tuliyonayo kwa sasa tuna mabeki wawili tu wa kati wanaoweza kucheza mechi zaidi ya 20 bila majeraha, nje ya hapo hatuna kisingizio kila idara ina watu wanaoweza kishinda taji lolote lile.
Ligi ndiyo kwanza tuko round ya kumi umejuaje hatutabeba kombe lolote ?
 
Back
Top Bottom