Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
SANCHO??? WA NINI? MCHUKUENI HARRY KANE
MKONGWE Steve McClaren amewaambia Manchester United kuweka mkazo kwenye kuwasajili mastraika Erling Haaland na Harry Kane kwa ajili ya manufaa ya timu na sio kuhangaika na saini ya Jadon Sancho
Man United kwa muda mrefu wameng’ang’ania kumfukuzia Sancho, huku klabu yake ya Borussia Dortmund mara kwa mara ikisema kwamba haina mpango wa kumuuza winga huyo.
Jumapili iliyopita, Man United ilichapwa 2-1 na Sevilla kwenye nusu fainali ya Europa League, huku safu yao ya ushambuliaji ikikosa nafasi nyingi kwenye kufunga mabao jambo linalomfanya McClaren, aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo chini ya Sir Alex Ferguson kuwataka wasajili namba 9 badala ya winga kama Sancho.
“Wale wachezaji wanne pale mbele wapo haraka sana, wapo vizuri na wamekuwa wakisababisha matatizo mengi sana kwa mabeki wa timu pinzani. Hata Anthony Martial naye amekuwa na kiwango kizuri,” alisema McClaren.
“Lakini, kwenye mechi kubwa wanaonekana kuwa na tatizo hawaonekani kama ni wafungaji wa kweli. Wanahitaji wachezaji wa daraja la juu kwenye nafasi hiyo. Sidhani kama Lukaku angefiti kwenye kikosi cha Man United, hivyo wanahitaji mtu kama (Erling) Haaland. Atawafaa zaidi.
“Nimemtazama Jadon Sancho sana kwenye mechi za Dortmund na anavutia, lakini amewazidi kidogo sana Martial, Rashford na Greenwood, hivyo nashangaa kwanini wanamhitaji kwa nguvu zote hizo?
“Yeye si namba tisa, na Martial, Rashford na Greenwood nao si namba tisa. Lazima uwe na mnyama kwenye boksi, mfungaji na namba tisa wa ukweli.”
Kutokaa na hilo, Haaland ndiye mchezaji ambaye McClaren anataka asajiliwe Man United badala ya Sancho na kama ikishindikana basi wavamie Tottenham Hotspur kwenda kumsajili Kane.