Tukimchukua Grealish tunapigwa tena, Aston Villa wata-take advantage ya kubaki Premier League kupiga pesa. Kuliko kumchukua Grealish kwa £80 ni bora tufufue dili la Brooks (Bournemouth) Umri mdogo (23) na pesa ndogo, hazidi £25 ukizingatia wameshuka daraja, ni bora kubet hapo kuliko kwa Grealish. Msimu wake wa kwanza akitokea Sheffield United ali-perform vizuri. Msimu huu majeruhi yaliathiri kiwango chake na hakucheza karibia msimu mzima ila bado aliporudi baada ya break ya Covid-19 ali-manage kupata goli moja. Ni Premier League proven. Kumpata huyu bado dili la Sancho linapaswa kushughulikiwa, tupate na CB na Striker, msimu tutauanza vizuri sana.