Interlacustrine Region,
Bado Man U ni mbovu tu na ni swala la muda tu, hivi utaweza kuifananisha na Man U ya akina Olesendeka iliyomgaga Buyern 2-1 miaka ya 1999? itaifikia hata theluthi tu kwa ubora?
You serious? Haujengi timu kwa kulinganisha na zama za nyuma sana, bali timu hujengwa kulingana na malengo yenu ya sasa, uwezo wa kifedha mlionao pamoja na aina ya ushindani mlionao kwa sasa mf. hauwezi kutumia mabomu ya nyuklia wakati unapambana na adui anayetumia mishale hapa unakuwa unapoteza rasilimali fedha, zamani tulitumia zana nzito nzito kwa ssb wapinzani wetu pia walitumia zana nzito, so it was a prudent decision by then.
Pia kuna variables nyingi sana zinazofanya timu kubwa kama Manchester United kusua sua japokuwa we have all the weapons at our arsenal, hatuna tatizo la kifedha wala nini. Bali tatizo letu kubwa ni football executive wetu alilalamikiwa sana na almost makocha wote waliondoka haleti wachezaji kwa wakati kwa mf. Mourinho alimuhitaji Harry Maguire lakini Ed alimleta miezi 6 baadae baada ya yeye kuondoka. Hata Bruno alihitajika kabla ya msimu kuanza ila akamleta kati kati msimu baada ya maandamano ya mashabiki.