Mc cane
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 5,569
- 10,527
Bruno is a goal scorer, Bruno is a chance creator, Bruno is a defender, Bruno is a leader.
Kusema ukweli bila mahaba kwa sasa tupo vizuri sana tokea mwanzoni mwa mwaka huu kuliko timu yoyote ile pale Uingereza. Kama tukipindua msimu ujao bila majeraha na hiki hiki kikosi cha kwanza kilichocheza mechi nne mfululizo tuna uwezo wa kubeba ubingwa bila hata kuongeza mtu. (fingers crossed, as long as no serious injuries)
Kama Pogba, Bruno, Greenwood, Martial na Rashford wakacheza pamoja kama sasa mechi zisizopungua 30 za ligi kuu, msimu ujao tunabeba ubingwa. Mara nyingi timu inayobeba makombe ikivuka mstari wa kati mtu yeyote yule anakufunga, wanakuwa na probability kubwa ya kupata goli dakika yoyote ile. Hiki tulikikosa kwa muda mrefu sana.
Bruno kabadilisha sana timu. Apart from being very creative pia ana kitu cha ziada anajua kutengeneza nafasi za magoli na kufunga pia. Binafsi nilikuwa namuona Pobga ndiye aliyekuwa na kipaji kikubwa pale kikosini lakini alikuwa anakosa support ya kipaji kingine cha ziada. Mf. msimu uliopita Pobga alikuwa top goalscorer kikosini alifunga goli 13 za ligi kuu na kutoa assists 9. Just imagine angeunganishwa na Bruno tokea msimu uliopita wangefanya makubwa sana.
Huwa nina imani kubwa sana na Pogba ndani ya uwanja. Japokuwa nje ya uwanja ana behavioral inconsistency labda ssb ya yule wakala wake mwenye tamaa ya pesa Mino Raiola. Niliamini muda mrefu sana Pogba alihitaji kuongezewa mtu mwenye kipaji sawa na yeye au kumzidi ili turudi ktk kiwango cha ushindani wa kweli.
au wewe unaona umeongea a point?

