Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Wakuu kuna kutoboa hapa kweli? Au ndio mtaenda kupitia mgongo wa Man City ban

Leicester City: 58 pts

Arsenal
Bournemouth
Sheffield United
Tottenham
Man United

Chelsea: 57 pts

Crystal Palace
Sheffield United
Norwich City
Liverpool
Wolves

Man United: 55 pts

Aston Villa
Southampton
Crystal Palace
West Ham
Leicester City
Leicester anaweza poteza kwa spurs na asernal...pia tutakutananae.

Naiona kama uchochoro wetu
 
Mkuu umeongea vyema sana, kiukweli kuna wachezaji huwa ni very promising katika soka la vijana lakini wanapokwenda kwenye soka la wakubwa wanaishia njiani

Man Utd ndio timu ambayo imetoa vijana wengi na wakacheza premier league kwa wingi kuliko klabu nyingine yoyote uingereza (duniani) lakini wengi wao wakichezea vilabu vingine

Umeongea mambo mengi, ila umenigusa sana ulivyotaja Ravel Morrison, huyu bwana mdogo ana kipaji kweli kweli lakini kipaji chake ndio hivyo kinapotea, kwa sasa nadhani yupo Sheffield. Huyu bwana mdogo kwa nyakati tofauti Ferdinand na Rooney wamewahi kusema kwenye kizazi chao pale United alikuwa bora kuliko Pogba na Lingard lakini angalia kwa sasa anavyotangatanga, hata Lingard amemzidi . Kwa wasiomjua huyu dogo anacheza na vitu akina Hazard, ni mtundu mtundu kama Wabrazili hivi. Nadhani huwa kuna shida ya attitude ya wachezaji hawa vijana, angalia hata Chelsea kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikitawala soka la vijana Uingereza lakini hao vijana wako wapi kwenye timu ya wakubwa?

Kwa sasa tunawatazama akina Levit na Garner kama viungo wa kati watarajiwa kwa miaka inayoanzia hivi karibuni, pia yupo Traore na Mejibri. Lakini ili wafikie uwezo wao halisia ni kuwa na right mentality. Wengine pia umewataja.

Kiukweli kwa sasa sioni kama kuna tija ya kuweka hawa watoto katika mechi tunazocheza (labda kwa uangalifu sana), maana mechi zote ni kama fainali, zote ni must win games iwe Europa, iwe FA na ligi ndio kabisa. I hope msimu ujao kutakuwa na fursa za kutosha kwao kuonesha vipaji vyao.
miaka 10 iliopita nakumbuka tulikuwa na kundi kubwa sana la wachezaji vijana waliokuwa wanaleta matumaini ya kuja kuleta mapinduzi makubwa kwenye kikosi cha kwanza kama vile (davide petrucci, lingard, zoran tosic, ryan tunnicliffe, ravel morrison, danny drinkwater, rodrigo posebon, ben amos, michael keane na will keane, paul pogba, danny simpson, cathcart, danny welbeck, jonny evans na mdogo wake corry evans) na baadhi yao waliwahi kujishindia tuzo za uchezaji bora wa vijana kwa ngazi ya klabu na hata kitaifa.

bahati mbaya sana kundi kubwa la vijana hao walishindwa kuvihamisha viwango vyao kwenye timu kubwa kadri walivyokuwa wanapewa nafasi jambo lililopelekea baadhi yao kuuzwa na wengine kutolewa kwa mkopo wa muda mrefu (japokuwa si jambo baya) na hata wale waliofanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza hawakuwa na muelekeo ulio bora (danny welbeck, tom cleverley, danny gibson) wote hao hawakuwa na good performance iliodumu kwa muda mrefu ukilinganisha na graduate wa class 92,

Na wengineo mfano wa paul pogba, drinkwater walikwenda kuanzisha maisha mapya kwenye vilabu vyengine kimafanikio zaidi

ina maana hata huu uwekezaji wa soka la vijana hauna utofauti na mchezo wa kamari ( mara nyingi umdhaniaye ndiye kumbe siye ), tusisahau hata class of 92 walikuwepo vijana wenye vipaji lakini walishindwa kufanikiwa kisoka ndani ya klabu huku tukishuhudia wachezaji wengineo mfano (nicky butt, paul scholes, phil neville) wakiwa na careers nzuri sana kwenye ulimwengu wa soka na wengineo mfano robbie savage alikwenda kutengeneza maisha mapya

======================================

baada ya takribani miaka 10 hali hii ya kuwa na kundi kubwa sana la vijana tunaotamani kuwaona kwenye kikosi cha kwanza imejirudia tena (mengi, ramazani nasikia ameshaondoka, levitt, garner, laird, gomez naye anatimka, laird, mejbir, puigmal ,mensah, bernard),

kivyovyote inaonekana dhahiri kuna gape kubwa sana la kiushindani kati ya michuano ya vijana na ile michuano tulioizowea (premier league) ndio maana si ajabu kushuhudia vijana wengi wanaofanya vizuri huko chini kushindwa kuendana na mikiki ya kikosi cha kwanza pindi wanapopewa nafasi (mfano andreas perreira alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji bora wa reserve lakini huku ukubwani amekuwa wa ovyo sana, muangalie tahit chong anavyoshindwa kuendana na kasi ya ligi kuu lakini akirudi team ya under 23 anafanya vizuri sana)

si vibaya kuweka matarajio makubwa kwa mchezaji fulani kwa kuangalia zaidi ubora wake kupitia soka la vijana hususani pale tu unapokuwa na benchi la ufundi linalojua kuishi na young players, na jambo zuri zaidi kwa sasa klabu ipo chini ya mikono ya mwanadamu aliyelelewa na Fergie (muumini wa kuwapa nafasi vijana kutoka moyoni mwake), uwepo wake klabuni, his vision kuhusiana na kuwapa nafasi vijana wenye DNA za man utd kunazidi kuwapa matumaini vijana mfano wa huyo mengi, levitt, garner, laird, mejbir ya kwamba siku chache zijazo watapata nafasi ya kuingia kikosi cha kwanza kama ilivyo kwa greenwood, chong, scott mctominay na brandon williams

nadhani hii ishu ya kuimpelements young players ni suala la kusubiri uamuzi wa benchi la ufundi likiongozwa na Solskjaer mwenyewe , Mike Phelan, Michael Carrick, Kieran McKenna, goalkeeping coach Richard Hartis, under-23s manager Neil Wood, under-18s manager Neil Ryan, na nicky Butt ambaye ni head of first-team development.

wao ndio wenye uamuzi wa mwisho na wao ndio wenye ufahamu mkubwa juu ya mwenendo wa mchezaji fulani kiukuaji.
naamini Teden mengi atakuwa na nafasi kubwa sana msimu ujao endapo klabu itakapofikia uamuzi wa kumuuza chris smalling, jones, na rojo.

unajua kwa sasa backup pekee ya uhakika tulionayo kikosini ni eric bailly, yule bwana mdogo Tuanzebe inasemekana ni majeruhi mpaka September.

kwenye ile mechi ya astana nilivutiwa zaidi na Dylan Levitt, alipiga complete pass 100

===================================
 
Sio muda huna, sema hizo stats huna! Hazipo na hazitakuja kuwepo so kuliko kutafuta kitu ambacho hakipo kheri tu ufur hizo soksi.

Alafu mzee baba na ngao ya hisani kabisa you keep bothering kuwa ni kombe ambayo mchezaji kwa ngazi ya klabu anayawazia kuwa ni accomplishment?

Get your facts together. Give your sparks a little time to make fire. Acheni nonsense hypes.
SteveMollel mbona umetukaushia kutupa story za movies kwenye jukwaa letu
 
Wakuu kuna kutoboa hapa kweli? Au ndio mtaenda kupitia mgongo wa Man City ban

Leicester City: 58 pts

Arsenal
Bournemouth
Sheffield United
Tottenham
Man United

Chelsea: 57 pts

Crystal Palace
Sheffield United
Norwich City
Liverpool
Wolves

Man United: 55 pts

Aston Villa
Southampton
Crystal Palace
West Ham
Leicester City
Leicester ana fixture ngumu sana, atatupisha pale juu lazima, pia tuna game nae mkononi
 
The problem is mnapigia hesabu wengine kupoteza. Je nyie mtashinda game zote wakati hao wengine wanapoteza? Huu ni mpira
Inaonekana hesabu za probability zilikutesa sana kijana.
Huhitaji kuwa na elimu ya juu kuona kwamba leicester ana ratiba ngumu sana ukilinganisha na sisi ofcourse anything can happen but ni ngumu kuamini atachukua 3 points kwa utd,asernal na spurs.
 
Inaonekana hesabu za probability zilikutesa sana kijana.
Huhitaji kuwa na elimu ya juu kuona kwamba leicester ana ratiba ngumu sana ukilinganisha na sisi ofcourse anything can happen but ni ngumu kuamini atachukua 3 points kwa utd,asernal na spurs.
Mkuu sawa. Ngoja tusubiri
 
Wakuu kuna kutoboa hapa kweli? Au ndio mtaenda kupitia mgongo wa Man City ban

Leicester City: 58 pts

Arsenal
Bournemouth
Sheffield United
Tottenham
Man United

Chelsea: 57 pts

Crystal Palace
Sheffield United
Norwich City
Liverpool
Wolves

Man United: 55 pts

Aston Villa
Southampton
Crystal Palace
West Ham
Leicester City
Sisi tunapigania nafasi ya tatu nyie endeleenii kubaki hapo mlipo sisi hatuwezi kukaa uswahilini.
 
This front 3 has score more goals than Liverpool's this season
manchesterunited___CCOvUPTIgh-___.jpeg
 
Pre season na mwishoni mwa ligi Manchester United utawapenda .
Ngoja ligi ianze upya

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
Msimu uliopita mwishoni mwa Ligi, walipoteza mechi karibia zote.

Msimu 2017/18, matokeo mchanganyiko

Hata 2016/17, napo ililuwa hivyo, Mou aliamishia nguvu zote kwenye Europa league.

Sa sijajua hicho kitu ulikiona wapi?
 
Back
Top Bottom