Naona Solkjaer anachelewesha sana kumuintroduce kikosini Teden Mengi.
miaka 10 iliopita nakumbuka tulikuwa na kundi kubwa sana la wachezaji vijana waliokuwa wanaleta matumaini ya kuja kuleta mapinduzi makubwa kwenye kikosi cha kwanza kama vile (davide petrucci, lingard, zoran tosic, ryan tunnicliffe, ravel morrison, danny drinkwater, rodrigo posebon, ben amos, michael keane na will keane, paul pogba, danny simpson, cathcart, danny welbeck, jonny evans na mdogo wake corry evans) na baadhi yao waliwahi kujishindia tuzo za uchezaji bora wa vijana kwa ngazi ya klabu na hata kitaifa.
bahati mbaya sana kundi kubwa la vijana hao walishindwa kuvihamisha viwango vyao kwenye timu kubwa kadri walivyokuwa wanapewa nafasi jambo lililopelekea baadhi yao kuuzwa na wengine kutolewa kwa mkopo wa muda mrefu (japokuwa si jambo baya) na hata wale waliofanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza hawakuwa na muelekeo ulio bora (danny welbeck, tom cleverley, danny gibson) wote hao hawakuwa na good performance iliodumu kwa muda mrefu ukilinganisha na graduate wa class 92,
Na wengineo mfano wa paul pogba, drinkwater walikwenda kuanzisha maisha mapya kwenye vilabu vyengine kimafanikio zaidi
ina maana hata huu uwekezaji wa soka la vijana hauna utofauti na mchezo wa kamari ( mara nyingi umdhaniaye ndiye kumbe siye ), tusisahau hata class of 92 walikuwepo vijana wenye vipaji lakini walishindwa kufanikiwa kisoka ndani ya klabu huku tukishuhudia wachezaji wengineo mfano (nicky butt, paul scholes, phil neville) wakiwa na careers nzuri sana kwenye ulimwengu wa soka na wengineo mfano robbie savage alikwenda kutengeneza maisha mapya
======================================
baada ya takribani miaka 10 hali hii ya kuwa na kundi kubwa sana la vijana tunaotamani kuwaona kwenye kikosi cha kwanza imejirudia tena (mengi, ramazani nasikia ameshaondoka, levitt, garner, laird, gomez naye anatimka, laird, mejbir, puigmal ,mensah, bernard),
kivyovyote inaonekana dhahiri kuna gape kubwa sana la kiushindani kati ya michuano ya vijana na ile michuano tulioizowea (premier league) ndio maana si ajabu kushuhudia vijana wengi wanaofanya vizuri huko chini kushindwa kuendana na mikiki ya kikosi cha kwanza pindi wanapopewa nafasi (mfano
andreas perreira alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji bora wa reserve lakini huku ukubwani amekuwa wa ovyo sana, muangalie
tahit chong anavyoshindwa kuendana na kasi ya ligi kuu lakini akirudi team ya under 23 anafanya vizuri sana)
si vibaya kuweka matarajio makubwa kwa mchezaji fulani kwa kuangalia zaidi ubora wake kupitia soka la vijana hususani pale tu unapokuwa na benchi la ufundi linalojua kuishi na young players, na jambo zuri zaidi kwa sasa klabu ipo chini ya mikono ya mwanadamu aliyelelewa na Fergie (muumini wa kuwapa nafasi vijana kutoka moyoni mwake), uwepo wake klabuni, his vision kuhusiana na kuwapa nafasi vijana wenye DNA za man utd kunazidi kuwapa matumaini vijana mfano wa huyo mengi, levitt, garner, laird, mejbir ya kwamba siku chache zijazo watapata nafasi ya kuingia kikosi cha kwanza kama ilivyo kwa greenwood, chong, scott mctominay na brandon williams
nadhani hii ishu ya kuimpelements young players ni suala la kusubiri uamuzi wa benchi la ufundi likiongozwa na Solskjaer mwenyewe , Mike Phelan, Michael Carrick, Kieran McKenna, goalkeeping coach Richard Hartis, under-23s manager Neil Wood, under-18s manager Neil Ryan, na nicky Butt ambaye ni head of first-team development.
wao ndio wenye uamuzi wa mwisho na wao ndio wenye ufahamu mkubwa juu ya mwenendo wa mchezaji fulani kiukuaji.
naamini
Teden mengi atakuwa na nafasi kubwa sana msimu ujao endapo klabu itakapofikia uamuzi wa kumuuza chris smalling, jones, na rojo.
unajua kwa sasa backup pekee ya uhakika tulionayo kikosini ni
eric bailly, yule bwana mdogo
Tuanzebe inasemekana ni majeruhi mpaka September.
kwenye ile mechi ya astana nilivutiwa zaidi na
Dylan Levitt, alipiga complete pass 100
===================================