Wakati mwingine mashabiki wa united tunashindwa kuona mapungufu yaliyosababishwa na injury ya Pogba, Scot, Martial na sasa Rashford.
Suala la injury siyo la kumlaum sana Ole na baadhi ya wachezaji kutokuwa form kama timu yetu isingepata injury nyingi mwanzo wa msimu pengine tungekuwa juu ya hapo tulipo.
Vipindi ambavyo United tulipoteza point nyingi sana ni september, October na November lakini ndiyo kipindi Martial, Luke Shaw, Matic, paul Pogba na Scot walikuwa injured.
Mwezi December tulifanya vizuri kuliko timu zote with exception ya Liverpool tu kwani pamoja na udogo wa kikosi chetu tuliweza kupambana tukashinda 4 games za epl na mechi za FA na Carabao.
Nadhani ongezeko la Bruno Fernandez litatupa ahueni kidogo lakini kutokuwepo kwa Rashford kunafanya timu isiwe na madhara sana kwenye final third yetu.
Kosa walilolifanya Woodward kutokusajili striker wa maana kama Haland, Timo Werner au Cavan litaendelea kutufanya tuonekane wanyonge kwa kila timu hasa kutokana na washambuliaji wetu waliopo kutokuwa wapambanaji sana.
Ngoja tuone Ighalo ataongeza kitu gani kwenye safu yetu ya ushambuliaji kama ataelewana vizuri na wachezaji wenzake haraka huenda tukaona matunda yake.
Tactical brilliance ya benchi letu nafikiri siyo mbaya kihivyo, kitu nachokiona mimi ni mapungufu ni bench letu kushindwa kuwafanya wachezaji wetu kuwa real competitors.
Kujiamini kupita kiasi kwa timu yetu dhidi ya timu ndogo na benchi la ufundi kutokulifanyia kazi suala hili kumetugharimu sana msimu huu.
Mechi nyingi tulizotakiwa kupata points tuliziachia kirahisi sana tena bila hata kuonyesha kuwa tunahitaji point hizo.
Msimu tayari tumeshaupoteza huu tujipange kwa next season huenda tutatoboa but lazima tuongeze walau wachezaji wengine watatu ambao ni wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza moja kwa moja kama Bruno.
Sent using
Jamii Forums mobile app