Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Cha ajabu unaleta stats za msimu uliopita kuwa Pogba ni bora, ambaye hajacheza mechi hata 10, hana goli hata moja

Haya ni madhara makubwa ya kukariri

Msimu huu amekuwa bora kupata majeraha na kukalikiti nywele na sio uwanjani

Msimu wa mwaka jana wenyewe amefunga goli 13/14 (hichi ndio kigezo kikubwa kilichotumika kumuweka) , goli 7 kati ya hizo ni penati, kati ya penati 12 alizopiga, kakosa 5

Huyu hata Pep alimkataa hawezi kuwa top 5 ya midfielders UK, hata akina Moutinho wanaweza kumuweka benchi

Hawezi kuwa juu ya KDB, Kante (akichezeshwa juu), Grealish, Madison wala Silva

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii timu hata ukimdumbukiza humo Casemiro na Kroos au Mesi hauwezi sema wako bora

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAMA kuna usajili ulisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Manchester United basi ni huu wa Bruno Fernandes aliyetua Old Trafford juzi akitokea Sporting Lisbon, kulekule walikowachukua Luis Nani na Cristiano Ronaldo enzi zile za Sir Alex Ferguson.
Baada ya kumkosa wakati wa usajili wa kiangazi, Man United imetumia sehemu kubwa ya dirisha dogo la usajili kupambana kunasa saini ya kiungo huyo na hatimaye siku chache kabla usajili kufungwa alitua Trafford.
Kwa nini watu wengi wanaamini Fernandes atakuwa suluhisho katika safu ya kiungo ya Man United? Ametoka wapi? Ni ipi historia yake? Na kipi ataongeza? Ni baadhi ya maswali ambayo yatajibiwa na makala haya;-

Ni nani?
Jina lake kamili ni Bruno Miguel Borges Fernandes, alizaliwa Septemba 8, 1994, katika kitongoji Maia, Porto, nchini Ureno, alianzia kucheza soka katika klabu ya Novara inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Italia, kabla ya kutua Udinese, kisha Sampdoria zote za Serie A.
Mwaka 2017, alijiunga na Sporting Lisbon ambako alijenga jina lake na kuibuka kuwa mmoja kati ya wachezaji tishio zaidi wa kiungo barani Ulaya, akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Ureno katika misimu ya 2017–18 na 2018–19. Januari 2020, Man United ilimnasa kwa dau la awali la Pauni 47 milioni.

Frank Lampard wa Kireno
Fernandes, 25, anajulikana kama Lampard wa Kireno kutokana na aina yake ya uchezaji ambayo imetawaliwa na kufunga mabao mengi akitokea kwenye eneo la kiungo.
Kama ilivyokuwa kwa Lampard ambaye enzi zake uwanjani alisifika kwa kuwa kiungo mwenye mabao mengi, huku akifunga sana kwa mashuti makali ya mbali na Fernandes pia ni hatari sana akiwa katikati ya Uwanja.
Wakati Lampard akifunga mabao 27 kutokea katikati ya Uwanja katika msimu wa 2009-10, Fernandes aliweka rekodi ya kuwa kiungo mwenye mabao mengi zaidi msimu uliopita kutokana na kufunga mabao 32 katika mechi 50.
Mbali na kufunga Fernandes pia anajua sana kupiga pasi za mwisho, katika mechi 134 alizocheza akiwa na kikosi cha Sporting Lisbon amefunga mabao 63 na kupiga pasi za mabao 42 hii inanyesha jinsi gani staa huyu anakuja na mabao Old Trafford.

Fundi mwenye jicho la tatu
Huyu jamaa anajulikana kwa jina la Fundi Mwenye Jicho la Tatu au ‘The Three-Eyed Maestro’ kama ambavyo amekuwa akiitwa huko kwao kutokana na aina yake ya uchezaji.
Pale timu yake inapopoteza mpira hukabia juu akiwa na straika ili kuwapa wakati mgumu mabeki wa kati wa timu pinzani, wapinzani wakifanikiwa kuondoa mpira katika eneo lao la hatari na yeye hushuka chini kabisa kucheza kama kiungo wa chini.
Timu yake ikiwa inashambulia hupenda kupandisha timu juu au kucheza pembeni ya mshambuliaji na kusubiri kugongeana naye haraka na kuwazuru wapinzani. Mashabiki wake pale Sporting walikuwa wanamuita ‘Three-Eyed Maestro’ wakimaanisha kiungo fundi mwenye jicho la tatu jina hili lilikuja kutokana na uwezo wake mkubwa sana wa kupiga pasi kwa wenzake hata katika mazingira magumu.
Fernandes ana uwezo wa kupiga chenga, kukokota mpira na miguu yote miwili, mzuri kwenye mipira ya kichwa anajua kupiga mipira iliyokufa ana mashuti makali sana na ni aina ya kiungo ambaye hukaa nje ya boksi kusubiri mipira ianguke na kumuadhibu mpinzani.

Jezi namba 10
Fernandes anajiamini sana akiwa na miaka 21 alienda Sampdoria akitokea Udinese na baada ya kufika pale akadai kuwa anaitaka jezi namba 10 ya timu hiyo, jezi ambayo inaheshimika sana ndani ya klabu hiyo kutokana na kuvaliwa na magwiji kama Roberto Mancini, hii iliwashangaza wengi, lakini huyo ndiye Bruno ambaye haogopi presha ya mashabiki.

Soka la kimataifa
Wakati akiwa Italia hakuwahi kuitwa kwenye timu ya taifa ya Ureno, kwa mara ya kwanza Fernandes alichaguliwa kujiunga na timu yake ya taifa Agosti 28, 2017 akichukua nafasi ya Pizzi ambaye aliumia kuelekea mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Visiwa vya Faroe, lakini hakucheza mechi hiyo.
Fernandes alichezea timu ya taifa ya Ureno chini ya miaka 23 katika michuano ya Olimpiki mwaka 2016, na kwa mara ya kwanza alichezea timu ya taifa ya wakubwa Novemba 10, 2017 akiingia kuchukua nafasi ya Manuel Fernandes katika mechi ya kirafiki ambayo timu yake ilishinda 3-0 dhidi ya Saudi Arabia.
Alifunga bao lake la kwanza akiwa na kikosi cha Ureno, Juni 7 mwaka 2018 katika mechi ya mwisho ya kujiandaa na fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Algeria ambayo timu yake ilishinda kwa mabao 3-0.

Sent using Jamii Forums mobile app
sio Sporting Lisbon, inaitwa

Sporting Clube de Portugal (sporting cp)

Beggars are not choosers
 
Asee yawezekana ighalo akatusaidia ila naamini Josh alikuwa sahihi sana hasa ikizingatiwa ametoka ktk youth set up yetu. Wapuuzi sana bodi ya hii timu,yaani wwlivyoona ofa ya kwanza imekataliwa wakaahirisha hapohapo na king mwenyewe alikuwa yupo tayari na kocha wake alishakubali matokeo kwa kuamini mchezaji anataka kwenda Man U. Mi niliamini nikiamka ningekutana na habari za King kusajiliwa Man U.
BOUN hawakuwa tayri kumuachia, ukizingatia wanapambana wasishuke daraja.

Kumuachia ilihitaji Man u itoe kitita kirefu.
Kuna sources zinasema, £50ml.

Kwa mtu mwenye akili timamu huwezi mnunua Josh king(28), hata kwa £30ml.
Tungekuja hapa kumponda tena ED na board yake.

Beggars are not choosers
 
KAMA kuna usajili ulisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Manchester United basi ni huu wa Bruno Fernandes aliyetua Old Trafford juzi akitokea Sporting Lisbon, kulekule walikowachukua Luis Nani na Cristiano Ronaldo enzi zile za Sir Alex Ferguson.
Baada ya kumkosa wakati wa usajili wa kiangazi, Man United imetumia sehemu kubwa ya dirisha dogo la usajili kupambana kunasa saini ya kiungo huyo na hatimaye siku chache kabla usajili kufungwa alitua Trafford.
Kwa nini watu wengi wanaamini Fernandes atakuwa suluhisho katika safu ya kiungo ya Man United? Ametoka wapi? Ni ipi historia yake? Na kipi ataongeza? Ni baadhi ya maswali ambayo yatajibiwa na makala haya;-

Ni nani?
Jina lake kamili ni Bruno Miguel Borges Fernandes, alizaliwa Septemba 8, 1994, katika kitongoji Maia, Porto, nchini Ureno, alianzia kucheza soka katika klabu ya Novara inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Italia, kabla ya kutua Udinese, kisha Sampdoria zote za Serie A.
Mwaka 2017, alijiunga na Sporting Lisbon ambako alijenga jina lake na kuibuka kuwa mmoja kati ya wachezaji tishio zaidi wa kiungo barani Ulaya, akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Ureno katika misimu ya 2017–18 na 2018–19. Januari 2020, Man United ilimnasa kwa dau la awali la Pauni 47 milioni.

Frank Lampard wa Kireno
Fernandes, 25, anajulikana kama Lampard wa Kireno kutokana na aina yake ya uchezaji ambayo imetawaliwa na kufunga mabao mengi akitokea kwenye eneo la kiungo.
Kama ilivyokuwa kwa Lampard ambaye enzi zake uwanjani alisifika kwa kuwa kiungo mwenye mabao mengi, huku akifunga sana kwa mashuti makali ya mbali na Fernandes pia ni hatari sana akiwa katikati ya Uwanja.
Wakati Lampard akifunga mabao 27 kutokea katikati ya Uwanja katika msimu wa 2009-10, Fernandes aliweka rekodi ya kuwa kiungo mwenye mabao mengi zaidi msimu uliopita kutokana na kufunga mabao 32 katika mechi 50.
Mbali na kufunga Fernandes pia anajua sana kupiga pasi za mwisho, katika mechi 134 alizocheza akiwa na kikosi cha Sporting Lisbon amefunga mabao 63 na kupiga pasi za mabao 42 hii inanyesha jinsi gani staa huyu anakuja na mabao Old Trafford.

Fundi mwenye jicho la tatu
Huyu jamaa anajulikana kwa jina la Fundi Mwenye Jicho la Tatu au ‘The Three-Eyed Maestro’ kama ambavyo amekuwa akiitwa huko kwao kutokana na aina yake ya uchezaji.
Pale timu yake inapopoteza mpira hukabia juu akiwa na straika ili kuwapa wakati mgumu mabeki wa kati wa timu pinzani, wapinzani wakifanikiwa kuondoa mpira katika eneo lao la hatari na yeye hushuka chini kabisa kucheza kama kiungo wa chini.
Timu yake ikiwa inashambulia hupenda kupandisha timu juu au kucheza pembeni ya mshambuliaji na kusubiri kugongeana naye haraka na kuwazuru wapinzani. Mashabiki wake pale Sporting walikuwa wanamuita ‘Three-Eyed Maestro’ wakimaanisha kiungo fundi mwenye jicho la tatu jina hili lilikuja kutokana na uwezo wake mkubwa sana wa kupiga pasi kwa wenzake hata katika mazingira magumu.
Fernandes ana uwezo wa kupiga chenga, kukokota mpira na miguu yote miwili, mzuri kwenye mipira ya kichwa anajua kupiga mipira iliyokufa ana mashuti makali sana na ni aina ya kiungo ambaye hukaa nje ya boksi kusubiri mipira ianguke na kumuadhibu mpinzani.

Jezi namba 10
Fernandes anajiamini sana akiwa na miaka 21 alienda Sampdoria akitokea Udinese na baada ya kufika pale akadai kuwa anaitaka jezi namba 10 ya timu hiyo, jezi ambayo inaheshimika sana ndani ya klabu hiyo kutokana na kuvaliwa na magwiji kama Roberto Mancini, hii iliwashangaza wengi, lakini huyo ndiye Bruno ambaye haogopi presha ya mashabiki.

Soka la kimataifa
Wakati akiwa Italia hakuwahi kuitwa kwenye timu ya taifa ya Ureno, kwa mara ya kwanza Fernandes alichaguliwa kujiunga na timu yake ya taifa Agosti 28, 2017 akichukua nafasi ya Pizzi ambaye aliumia kuelekea mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Visiwa vya Faroe, lakini hakucheza mechi hiyo.
Fernandes alichezea timu ya taifa ya Ureno chini ya miaka 23 katika michuano ya Olimpiki mwaka 2016, na kwa mara ya kwanza alichezea timu ya taifa ya wakubwa Novemba 10, 2017 akiingia kuchukua nafasi ya Manuel Fernandes katika mechi ya kirafiki ambayo timu yake ilishinda 3-0 dhidi ya Saudi Arabia.
Alifunga bao lake la kwanza akiwa na kikosi cha Ureno, Juni 7 mwaka 2018 katika mechi ya mwisho ya kujiandaa na fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Algeria ambayo timu yake ilishinda kwa mabao 3-0.

Sent using Jamii Forums mobile app
Solskiejar hana uwezo wa kuendeleza kipaji cha mchezaji kikafika palipotakiwa. Kocha hana mbinu za kutosha hivyo sitashangaa huyu BF kugeuka na kuwa average player
 
Bruno to start
manchesterunited___B8B_GM2ArYo___.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Solskiejar hana uwezo wa kuendeleza kipaji cha mchezaji kikafika palipotakiwa. Kocha hana mbinu za kutosha hivyo sitashangaa huyu BF kugeuka na kuwa average player
Upo serious kabisa hayo maneno?
-Kocha ambaye yupo responsible kwa trio ya Rooney/tevez/Ronaldo hajui kudevelop vipaji?
-kocha ambaye wakati yupo u23 ndio kikosi bora kabisa cha watoto miaka ya karibuni kikatoka kuanzia pogba, lingard, drinkwater, king, keane etc
-kocha aliembadili fred toka flop mpaka sasa ni fan favourite
-martial na rashford wote wapo kwenye form of their lives
-kocha alimtoa Haaland jalalani na watu kibao kumtabiria kakosea mpaka leo tunamuona super star
-kocha ambaye hata kabla Greenwood hatujamuona akifanya yake akasema Ni natural scorer ambaye hajawahi kumuona (anasema maneno hayo Rashford na Martial wapo kwenye form mwanzo wa ligi), na leo tunaona vision yake ilivyo accurate.
-mc tominay, wilson, james, lindelof wote wapo kwenye peak ya viwango vyao.

Wachezaji wachache sana utasema viwango vyao vimeshuka chini ya ole.
 
Back
Top Bottom