Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ningekuwa family ya pogba ningemwambia avunje uhusiano na huyu jamaa, kama unauwezo unauwezo tu. Raioula sio anayecheza, anayecheza ni mtu mwingine kabisa. In case attitude ni ya agent. Lakini kama wanafanana wangeoana kabisa tujue

Mamamamae
Yaani avunje mkataba na Mtu anaemsaidia kuingiza Pesa.

Sent using simu mbovu
 
Maisha ya Mounrinho sio mazuri, angebaki na uchambuzi kule Skysport uku kaja kushusha cv yake
Screenshot_20200101-195533.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesema in a complete sense

Ina maana strengths za Pogba na weakness zake uki compare na strengths za Grealish na weakness zake

Utaona kwamba Pogba anaikaba United

Japo hata kisoka kirusi ni overhyped
Labda nje ya uwanja,
Lakini kama ni ndani ya dimba, unakosea sana .

Note: Sipendezwi na tabia za Pogba na wakala wake pamoja na Media(50% hawa wanachangia).
Kwa manufaa ya Pande zote mbili(Man u vs Pogba), Pogba aondoke Summer.

Sent using simu mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua we are comfortable now, na kitendo cha Haaland kusajiliwa Dortmund hakiwaumi watu wengi sababu ma strikers wetu wote kwa sasa wapo fiti na wapo form, sidhani kama watu wangekuwa na mtazamo huo huo mwezi septemba, Oktoba na Novemba mwaka huu unaokwisha

Unasema tungesajili senior striker ili awafundishe, nimewahi kuuliza huko nyuma, senior striker unayewaongelea ambao wapo sokoni ni akina nani, sikupata majibu. Utanishangaza ukinitajia Mandzukic, Falcao, Ibrahimovic wakati tumemuacha Lukaku ambaye angeweza kufanya hiyo kazi ya "kuwafundisha madogo" kama unavyoshauri

Kwa sasa hivi kikosi chetu kina pure striker wawili, Martial na Greenwood ambaye bado hajacheza senior football kiasi cha kwamba akaaminiwa na kupewa majukumu ya timu, Rashy sio striker (sio namba 9), DJ sio namba 9.

Haaland sio senior (kwa idadi ya miaka aliyonayo), lakini ni senior kwa uzoefu wa kucheza senior football. Pamoja na kumbeza kwamba ametokea ligi laini, lakini kote huko amekuwa outstanding. Ligi ya mabingwa Ulaya ameng'ara, je na hayo ni mashindano nyoronyoro? Wachezaji wakubwa wote Ulaya tunawapitisha kuwa ni bora au wabovu kwa namna watakaocheza ligi ya mabingwa Ulaya.

Haaland ana magoli 8, ni wa pili nyuma ya Lewandowski mwenye magoli 10, na wanaomfuata wana goli 6, kwenye chati ya wafungaji wa UCL 2019/2020. Kuliweka suala hili ili lieleweke vizuri, Haaland kiufungaji yupo juu ya mchezaji anayetajwa kuja kuwa Ballon'dour winner siku zijazo, Mbape ambaye ana goli 5 kwenye UCL. Kwahiyo hapa tusikaririshane uongo kwamba dogo anafunga magoli ligi nyepesi nyepesi tu, huyu dogo ametoboa safu za ulinzi chini ya Koullibaly na VVD, kwa taarifa yako.

Nakukumbusha pia RB Salzburg, timu unayodai inacheza ligi nyepesi ndio imewaleta kwenye ulimwengu wa soka, akina Mane, Naby Keita, Minamino (Liverpool) Upemecano (RB Leipzig) n.k. Kwanini Haaland asiwe bora kisa tu ametokea ligi ya Austria.

OGS akiwa mchezaji alitokea Norway, Nesterloy alitokea Uholanzi, Delle Ali ametokea MK Dons timu ya ligi daraja la 3, Ibrahimovic alitokea Malmo ya Sweden, orodha ni ndefu sana.

Pia nikukumbushe, kuwa scouts wapo kwa ajili ya hiyo kazi, ya kutafuta diamonds kwenye mashimo na si kwenda kununua almasi kwenye masoko yaliyopo mjini

Mwisho nikwambie, kusajili siku zote huwa kuna asilimia flani ya gambling, kuna wakati unaweza ukasajili mchezaji na akacheza kwa kiwango ambacho haukukitazamia au akang'ara, kwa United kufanya gambling ya £20million tu kwa Haaland isinge disturb pochi nene ya Glazers.

Kitu pekee kilichonifurahisha kwa huyu dogo kwenda Dortmund na sio kuja United, ni kutoongeza wigo wa kufanya biashara na tapeli Mino Raiola

Huyu dogo ameshakwenda, tuangalie mambo mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
"Kitu pekee kilichonifurahisha kwa huyu dogo kwenda Dortmund na sio kuja United, ni kutoongeza wigo wa kufanya biashara na tapeli Mino Raiola"

Huyu dogo ameshakwenda, tuangalie mambo mengine


Mkuu nami naungana Sana na wewe katika Paragraph hiyo ya mwisho, Kwa kweli binafsi n
Minefurahi kushindikana kwa hilo deal kwa sababu ya Mino.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda Juve, PSG hawajawahi kumtaka Pogba na Pogba mara kibao amekuwa akisema kuwa hana mpango wa kwenda kucheza mji wa Paris. Nahisi mji/timu aliotoka Pogba una kitu flani ambacho kinamfanya kuwa kama msaliti akienda PSG

Kiujumla, hata akienda Juve Pogba is very average player, maximum a 65% player

Na Madrid anayemtaka ni Zidane tu, lakini hakuna kiongozi anaye fancy Pogba kwenda Madrid
Juve, Psg?

Sent using simu mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Madrid anayemtaka ni Zidane tu, lakini hakuna kiongozi anaye fancy Pogba kwenda Madrid

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana nawe katika hili. Nakumbuka enzi zile Ronaldo anataka kuondoka, na Madrid wakiwa wanamhitaji kweli kweli, tuliweza kudumu naye kwa misimu mitatu tu toka alivyoanza drama(baada ya kombe la dunia 2006). Sasa huyu kirusi, angekuwa anahitajiwa na Barca ama Madrid, tusingeweza kumsajiri mbele ya hao miamba mwaka ule wa 2016.
 
Nimesema in a complete sense

Ina maana strengths za Pogba na weakness zake uki compare na strengths za Grealish na weakness zake

Utaona kwamba Pogba anaikaba United

Japo hata kisoka kirusi ni overhyped

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana aisee ukitoa De bruyne hakuna medfield yoyote uingereza kushinda Pogba.

Mchezaji anaekupa Double digits ya magoli na Assist ni nadra sana kuwapata.
 
Nakubaliana nawe katika hili. Nakumbuka enzi zile Ronaldo anataka kuondoka, na Madrid wakiwa wanamhitaji kweli kweli, tuliweza kudumu naye kwa misimu mitatu tu toka alivyoanza drama(baada ya kombe la dunia 2006). Sasa huyu kirusi, angekuwa anahitajiwa na Barca ama Madrid, tusingeweza kumsajiri mbele ya hao miamba mwaka ule wa 2016.
Seems muna under estimate sana man U, kwamba mchezaji hawezi chagua Man u over hao Madrid na Barca? Wachezaji wa America kusini sawa ila wa ulaya wapo Wengi tu wanaoipenda Man U.

Na 2016 wote Barca na Madrid walimtaka pogba ila alichagua man U.

Mashabiki wa Man U wakikubali siku zote unakuwa legend popote pale duniani, Forlan mwenyewe anashangaa hadi leo wimbo wake unaimbwa na popote anapokwenda Duniani watu wanamkumbuka kama Mchezaji wa Man U japo hajapatia mafanikio yake pale.
 
Back
Top Bottom