Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hili suala linaniumiza sana kichwa....

Samatta anacheza Genk alafu Lingard na Rashford wanacheza Manchester united....
Na ndo maan nikauliza hivi Rashid na Samatta nani mkali? Sasa mkuu radika anaanza kunitolea povu. Uyu ukimpeleka pale Genk na Samata ukamshusha apo OT ..kutakuwa na tofauti kubwa sana.. Kwanza Genk watastrago kupata matokeo..Samata ana uhakika wa kukupa goli kila gemu atakayocheza..
 
Tutolee bangi zenu ninyi.. Yaani Samata alingane na Rashford??! ... Acha dharau.

Najua tunamsakama Rashford ila Ni mchezaji ambae ameshaprove uwezo wake EPL akiwa kwenye team "Mbovu" .. ameshazichana chana almost team zote kubwa za EPL..

Na kwa taarifa yako Manchester United ina matatizo ya ya kitimu kuliko mchezaji mmoja mmoja .. Hujiulizi kwa nini Micktaryan, Lukaku, Memphis Depay, Rooney , Blind, Di Maria , Falcao , na wengine walionekana Flop na hawana uwezo wakati wakiwa United?? Ila baada ya kutoka United almost wachezaji wote wanafanya vyema .. Je hapo tatizo Ni nini ....

Unataka kuniambia Huyo Samata Ana uwezo exceptional kuwazidi hao wachezaji woooote ... Sitaki kuamini Samata Ana kipaji kumshinda Di Maria au Depay... Narudia Tena Huyo Rashford akitoka United kwenda timu yoyote uwezo wake utaonekana Kama tunavyoona uwezo wake wachezaji wengine ambao walionekana Flop walipokuwa United.
 
Kwahiyo hili tukio jana hatujaliona 😁😁😁
Huyu beki gari tabia ya kukabia matako kaanza lini
IMG-20191025-WA0000.jpg
 
Unajua mkuu nilichogundua hawa madogo tuwavumilie tu mbona wakina salah na mane wamehangaika ktk miaka yao 21 hao wakina mane na salah walikuwa wapi na walifunga goli ngapi?
Katika umri wa miaka 21 Rashford tayari ameshacheza misimu minne Ya EPL tena katika timu hiyo hiyo

Wakati katika umri huo Mane na Salah tena hawakupitia Academy walikuwa wanastruggle Kwa kuhama hama vitimu vidogo vya nchi mbalimbali kutafuta malipo mazuri wakati Rashford ni fresher from academy ya Club tajiri duniani
 
Hivi ni kwanini Ole anaanzishaga Young badala ya huyu dogo?
Mkuu hapo ni LUKE SHAW ajiandae kisaikolojia maana young hana muda mrefu wa kucheza Luke Shaw toka kasajiliwa hajawahi kuonesha kiwango chake murua ina maana toka aondoke Patric Evra ule upande una shida
Mapema sana ila Brandon William anakuja kumkalisha Shaw soon
 
Katika umri wa miaka 21 Rashford tayari ameshacheza misimu minne Ya EPL tena katika timu hiyo hiyo

Wakati katika umri huo Mane na Salah tena hawakupitia Academy walikuwa wanastruggle Kwa kuhama hama vitimu vidogo vya nchi mbalimbali kutafuta malipo mazuri wakati Rashford ni fresher from academy ya Club tajiri duniani
Sasa wamecheza mpira gani kama hawakuanzia kwenye academy?

Tukubali rashford anachukiwa kwakuwa anachezea manchester united na anachezea timu yenye pressure na matokeo kipindi hicho hao wakina mane na salah ktk miaka yao 21 hawakuwepo kwenye raman ya mpira tena rashaford kaanza na ligi ngumu si bora hao wameanza kupata uzoefu huko pembeni na kuzoea pressure kisha kuja kusukwa hapo liverpool

Ktk umri wa miaka 21 wa rashford ana goli nyingi kuwashinda hao wakomavu

Rashaford alishindanishwa na madogo kibao wanaochipukia ktk umr wake wengi wamepotea

Wakina iwobi wakina ihenacho wakina solanke wakina asensio ambao walikuwa na uzoefu wa kucheza kwa mikopo huko real mallorca idadi ni ndefu lakin dogo yupo tu aliemuacha rashford ktk utokaji wake ni mbape

Kuna takwimu hapo ktk umr wa miaka 21 wa rashford alan sherer 22

Alan Shearer

Games: 118
Goals: 23

Marcus Rashford

Games: 120
Goals: 31
 
Na si kwamba namaanisha rashford ni top striker kwa hii timu tunaemuhitaji kwa muda huu hapana tunatakiwa kuwa na mshambuliaji mzoefu na makini dogo bado ni mdogo majukumu makali timu haina muunganiko ila hatupaswi kumdharau sana kwamba mtu wa hovyo hapana ana vingi vya kujifunza muda anao na tayar kishafanya makubwa na kaprove premier league mech kubwa hapotei utamwona na anatoa mchango mzur tu kushinda vikombe baadhi na hii timu

Kama Fa cup Europa league na carabao huko anamchango wake mkubwa sana kafunga goli muhimu sana hasa mech ya celta vigo na anderletch

Rashford ni hazina ya hii timu hasa tutakapopata viungo makini bado tunacheza mchezo wa kujilinda lazima washambuliaji wahangaike sana kama tukicheza mchezo ambao walicheza na liverpool wa kushambulia nafikir wote mlimuona rashford

Ukiangalia timu ambazo madogo wanang'ara huko angalia viungo wao na mbele kulivyo madogo pressure inakuwa ndogo tofauti na kwetu

Jana pamoja na kusema martial ni mzembe anakuja chini kabisa kwa bissaka kuchukua mpira apande nao mbele ina maana mabek watakuwa wanamuangalia tu awapite hapa ina maana kakosa huduma ya viungo bora
 
Mkuu Radika, kwa hali ya timu yetu kwasasa ni kweli kuwalaumu kina Rashford na Martial hata mimi nimegundua ni kuwaonea tu.

Timu haitengenezi nafasi za wazi,ni kupiga pasi na kurudisha nyuma tu. Kama jana sio penalty tungetoka sare.

Ndio maana Scholes anapendekeza Ozil anunuliwe atakuwa msaada kwa sasa hasa ukizingatia Unai hamtaki. Sioni #10 wa kumtuliza bench Ozil.
 
Ni kweli mkuu
 
Back
Top Bottom