Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mou tatizo angepewa Maguire na Bissaka angetoboa sana. Ila naye alikuwa na matatizo(sijui ni yeye au Pogba) maana alishindwa kutengeneza mahusiano mazuri na wachezaji.

Naona Ed alijua Mou angebaki Pogba na Martial walikuwa wanatakiwa kuondoka,hakuwa tayari kwa hilo.
Brother, kumuondoa pogba lisingekuwa tatizo, bali tatizo lingekuwapo kama asingemleta mchezaji mwenye uwezo kama pogba.

Timu haiwezi kuenda kama kocha anawalamba miguu wachezaji fulani, au kama timu inamhusudu saana mchezaji ambaye anaweza kutafutiwa mbadala. So mou angefanya vizuri sana
 
Ole ni kinafiki sana..hapa kinamtongoza mtu
20191006_215549_rmscr-1.jpg
 
So sad!
View attachment 1225299
De Gea: “I don’t know what is happening. We cannot even score one goal in two games."

Jamaa kama anataka kulia hiviii!
Nimemtazama jamaa anavyoongea,timu ina hali mbaya sana,sanaa.

Nimeona pia Neville anaiponda management ya timu na jamaa kweli amesema ukweli mtupu. Timu inachukua makocha kwa kukurupuka hamna mipango na wakiharibu wanawafukuza.

Hapo kwenye kuchukua makocha kwa kukurupuka na kimakosa nimeona kabisa anaguswa Ole. Yani Ole amepewa timu kisa alishinda-shinda mechi alizoacha Mou😂😂 ni kama vile wanaangalia kocha wa bei chee.😂

Kwa hali hii safari ni ndefu na vile mapato ndio yanazidi kupaa,tutaharibiwa sana weekend zetu.
 
Kaka yani Jose Mourinho aje kwa wapare? Jose M anataka timu inayojiweza kiuchumi, hlf yule mikakati yake saiv kabadilisha amedai, kuja kulia lia hapo kwenu hawezi!
Wewe timu ina hela , akija 100 zinamtosha ,maana wachezaji wazuri tunao ,aongeze wawili au watatu kwa hiyo 100
 
Brother, kumuondoa pogba lisingekuwa tatizo, bali tatizo lingekuwapo kama asingemleta mchezaji mwenye uwezo kama pogba.

Timu haiwezi kuenda kama kocha anawalamba miguu wachezaji fulani, au kama timu inamhusudu saana mchezaji ambaye anaweza kutafutiwa mbadala. So mou angefanya vizuri sana
Naona kama Ed na mabosi zake wanamchukulia Pogba kama nembo ya timu kwa sasa,wasingependa aondoke.

Mou alianza kumchapa bench baada ya kuona ni kirusi,na mechi ya mwisho kama sikosei alikuwa bench tukipigwa na liver. Hii ilifanya waone Mou hamtaki tena Pogba.
 
"It's a journey we've started on and the culture is getting there. I can't give you any time but we're getting there. Huyu jamaa wa Norway anakusudio Naya na hii timu....ngoja tuone tunapoenda
 
Hii timu kwa kweli inanipa hasira sana. Hivi hawa wachezaji wa Man U wanakosa kitu gani ambacho wengine wanapata?

Vitoto vidogo vinalimbikizwa mishahara mikubwa pasipo kazi yoyote ya maana kweli!!!! Wolves wana aina gani ya wachezaji wenye kuzidi Man U, au hawa Newcastle wamesajili wachezaji wa level ipi ambao wachezaji wetu hawawezi kucheza nao na wapate matokeo?

Hatuwezi kuishi kujisifia mafanikio ya miaka kadhaa wakati tunateketea, tangu atoke Sir Ferguson hakuna lolote la maana limefanyika.

Ina maana uongozi wa Man U hauoni haya madudu au upo kwa ajili ya kutengeneza faida (pesa) msimu wa usajili unafika tunaondoa wachezaji huku tukiacha wazee na watu wasio na umuhimu kwenye timu.

Unaona huwezi kufanya kazi ya Lukaku mwenye kuijua EPL vyema na kwa umri wake akiwa na mabao zaidi ya 100 ya EPL tunabaki na Rashford kweli!!! Tuliuza Lukaku kisa nini sasa kama hatukuwa na replacement yake?

OGS nacho kinafiki kweli hiki kijiti yaani kinashindwa kuwa na msimamo na kupata wachezaji anabaki kuwa NDIYO MZEE hivi kuna mizungu minafiki kumbe.

Lampard anaichukua Chelsea wakiwa na ban ya usajili ila anaunganisha timu na kila mmoja anaona wazi kuwa Chelsea ina jitahida iwapo uwanjani. Tumekuja kuua kipaji cha Wanna na James kwa upumbavu wa uongozi wetu.
Daaah kweli kabisa kwa Mtu mwenye akili timamu kichwani kamwe hawezi kuvumilia huo uozo wa Man Utd inavyopata matokeo mabovu namna hii
 
Ndio maana nesema bodi inamatatizo makubwa sana

Imagine body ya man city imgemzuia pep kumuondoa yaya, hart, zabaleta na wengine ambao kwa macho ya lawaida walikuwa ni watu muhimu city, lakini tumeona timu yao inacheza vizuri zaidi saiv kuliko zamani. TIMU NI KUBWA KULIKO MCHEZAJI
Naona kama Ed na mabosi zake wanamchukulia Pogba kama nembo ya timu kwa sasa,wasingependa aondoke.

Mou alianza kumchapa bench baada ya kuona ni kirusi,na mechi ya mwisho kama sikosei alikuwa bench tukipigwa na liver. Hii ilifanya waone Mou hamtaki tena Pogba.
 
Tatizo wachezaji wengi ni watoto na siyo threat kwa timu yoyote.

Kocha mwenyewe hajielewi unawezaje kutumia mfumo mmoja mechi nane halafu zote unapata matokeo ya aina moja bila kufanya mabadiliko ?

Dirisha la usajili lilipita bila kufanya replacement ya wachezaji waliouza na hakuwa na mpango wa kununua mwingine alitegemea nini ?
Nini kifanyike jamani, tatizo ni kocha au wachezaji au bodi?
 
Nimemtazama jamaa anavyoongea,timu ina hali mbaya sana,sanaa.

Nimeona pia Neville anaiponda management ya timu na jamaa kweli amesema ukweli mtupu. Timu inachukua makocha kwa kukurupuka hamna mipango na wakiharibu wanawafukuza.

Hapo kwenye kuchukua makocha kwa kukurupuka na kimakosa nimeona kabisa anaguswa Ole. Yani Ole amepewa timu kisa alishinda-shinda mechi alizoacha Mou ni kama vile wanaangalia kocha wa bei chee.

Kwa hali hii safari ni ndefu na vile mapato ndio yanazidi kupaa,tutaharibiwa sana weekend zetu.
Zile mechi wachezaji wa Man Utd walizikamia tu kumkomoa Mourinho ili ajue wana uwezo mkubwa kiuchezaji na kiushindi hata asipokuwa kocha wao na ni baada ya kuzinguana na Pogba na Martial
 
Back
Top Bottom