Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Special one for winning tactics but not football ball possesion.
Mou tatizo angepewa Maguire na Bissaka angetoboa sana. Ila naye alikuwa na matatizo(sijui ni yeye au Pogba) maana alishindwa kutengeneza mahusiano mazuri na wachezaji.

Naona Ed alijua Mou angebaki Pogba na Martial walikuwa wanatakiwa kuondoka,hakuwa tayari kwa hilo.
 
Kama MUFC inataka kujengwa irudie makali yake, Ole sio kocha sahihi. Hawezi kuijenga hata apewe misimu sita.

Kocha anayewalambalamba wachezaji hawezi kujenga timu,wakati unawalambalamba baadhi ya wachezaji unashusha morali ya wachezaji wengine na hapo ndo kaburi la timu linapochimbwa.
Sawa ila mou alijaribu kuwa mkali ndo yakaibuka ya pogba na martial na wengineo
 
Mou tatizo angepewa Maguire na Bissaka angetoboa sana. Ila naye alikuwa na matatizo(sijui ni yeye au Pogba) maana alishindwa kutengeneza mahusiano mazuri na wachezaji.

Naona Ed alijua Mou angebaki Pogba na Martial walikuwa wanatakiwa kuondoka,hakuwa tayari kwa hilo.

Mou a man with winning strategy..mambo ya possesion ni ya mpinzani!
Sitasahau ile mech ya Arsenal 75% vs man utd 25% ila mechi ikaisha Arsenl 1-3 Man u kama sijakosea!
 
So sad!
View attachment 1225299
De Gea: “I don’t know what is happening. We cannot even score one goal in two games."

Jamaa kama anataka kulia hiviii!
Ubora wa huyu kipa alistahili kuwa anashinda sana mataji,kwa hii MUFC ya Ole hatumstahili kabisa.

Kwa mchezaji mwenye mapenzi na timu inaumiza sana kuona timu inacheza kama kuku alitekatwa kichwa.

Na hatuwezi kufunga magoli kwasababu kiungo chetu kimetepeta hili nalisema kila siku,mipira mingi inapotea sana pale kati. Fred(sijui ni mbrazili wa wapi huyu) ni mzito sana kati hapawezi kuchangamka.

Timu yetu hamna mchezaji/kiungo anayeweza kukimbia kwa kasi akijaribu kuwatoka mabeki pale hali inapokuwa ngumu kama leo. Timu ikijilinda mwanzo mwisho hatuwezi kufunga goli, tutaanza kugonga pasi tu na kurudisha nyuma mpira.

Timu yetu inahitaji kocha mpya mzoefu na wachezaji wengine kama watano hivi ili iweze kuwa timu na sio hili genge la 'instagramers' kati yao hao watano kuwe na CDM teleza aina ya Kante na #9 anayewafuata mabeki( sio anaewakimbia kama Rashford) kwenda kumtumbua kipa.

Zaidi ya hapo,hamna timu hapa.
 
"Remember when Harry Maguire said he was leaving for bigger and better things?"
Ever since,

-Leicester city are above them

-Tammy Abraham better than Rashford

-Ole Gunnar Solskjaer's misery deepens

-Chelsea and Arsenal better than Manchester United right now
Better things iliokusudiwa hapo ni mkwanja, baba manyuu kuna mkwanja mrefu kulee
 
Sawa ila mou alijaribu kuwa mkali ndo yakaibuka ya pogba na martial na wengineo
Basi tatizo la hii timu limeanzia kwa wamiliki na Ed, huwezi kuwa na timu bora kwa kuwapigia magoti wachezaji. Pale kwa Pep. ukizingua umekwenda.
 


Hii timu kwa kweli inanipa hasira sana. Hivi hawa wachezaji wa Man U wanakosa kitu gani ambacho wengine wanapata?

Vitoto vidogo vinalimbikizwa mishahara mikubwa pasipo kazi yoyote ya maana kweli!!!! Wolves wana aina gani ya wachezaji wenye kuzidi Man U, au hawa Newcastle wamesajili wachezaji wa level ipi ambao wachezaji wetu hawawezi kucheza nao na wapate matokeo?

Hatuwezi kuishi kujisifia mafanikio ya miaka kadhaa wakati tunateketea, tangu atoke Sir Ferguson hakuna lolote la maana limefanyika.

Ina maana uongozi wa Man U hauoni haya madudu au upo kwa ajili ya kutengeneza faida (pesa) msimu wa usajili unafika tunaondoa wachezaji huku tukiacha wazee na watu wasio na umuhimu kwenye timu.

Unaona huwezi kufanya kazi ya Lukaku mwenye kuijua EPL vyema na kwa umri wake akiwa na mabao zaidi ya 100 ya EPL tunabaki na Rashford kweli!!! Tuliuza Lukaku kisa nini sasa kama hatukuwa na replacement yake?

OGS nacho kinafiki kweli hiki kijiti yaani kinashindwa kuwa na msimamo na kupata wachezaji anabaki kuwa NDIYO MZEE hivi kuna mizungu minafiki kumbe.

Lampard anaichukua Chelsea wakiwa na ban ya usajili ila anaunganisha timu na kila mmoja anaona wazi kuwa Chelsea ina jitahida iwapo uwanjani. Tumekuja kuua kipaji cha Wanna na James kwa upumbavu wa uongozi wetu.
 
Mou a man with winning strategy..mambo ya possesion ni ya mpinzani!
Sitasahau ile mech ya Arsenal 75% vs man utd 25% ila mechi ikaisha Arsenl 1-3 Man u kama sijakosea!
Mou alikuwa kocha wenu sahihi kuwapeleka sehemu salama ,

Ila mkamuona hafai ,mm mou namuelewa sana anajua kuzicheza mech za kila aina ,kikubwa mtimizie mahitaji yake


Namtaman sana aje arsenal maana hatuna kocha ,
 
Naona Kuna misukule inamkumbuka mou na kutuona sisi wanajeshi tuliempindua yule hayawani kuwa tulikosea kwa maamuzi Yale pendwa .. Nasema Tena timu ilifanya maamuzi sahihi kumuondoa nduli yule .. Kufanya vibaya kwa ole hakuondoi upuuzi wa Mou ...




Narudia Tena na nimekuwa nikilisema hili several times man United lazima iwe timu ya kocha akifanya vibaya FUKUZAAAAAAAA... Sio kung'ang'ania .. Mou Fukuzaaaaaa ... Huyo Ole Fukuzaaaaaa Mpaka turudi njia kuu.



Sasa nazisubiri zile mbuzi au mifugo ya nduli mou ije kichwa kichwa kujibu hii comment kipuuzi puuzi niwaoneshe kwanini Kilimo kiliitwa Ni uti wa mgongo.


GGMU



GGMU
Stress mbaya sana
 
Huyu kocha sio Ole ni hOle kabisa


Alitabiri
IMG_20191006_214634.jpeg
 
Sio kocha ni mfumo mzima wa uongozi unaambiwa uza lukaku na wewe unakubali bila kupima maana yake mambo ya mpira ni zero wale wote wakina ed wakufukuzwa wapo kibiashara mashabik wa hii timu wanachotakiwa kufanya ni kuacha kununua bidhaa za hii timu na kuingia uwanjani wakipata hasara kwenye biashara jibu watapata wao wanafaidika kifedha mambo ya uwanjani hayawahusu
Kwa upande wangu kocha na body nzima ndiyo tatizo.
Ukiisikiliza press ya leo na ya mechi zingine tunazofungwa basi utagundua kwamba kocha hazungumzi uhalisia na mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi, bali anasema timu imecheza vizuri na tutafika kwenye kiwango bora. Hivyo body inamtumia kocha huyu kama PUPPET AU KIBARAKA ili atupooze tuashabiki na kutoifuatilia body.

Utakumbuka ulipokuwa unaanza msimu uliopita mou aligombana na bodi kwasababu ya usajiri na body haikupendezwa na hilo. Ndiyo maana wanampenda sorkjaer ambaye anawatetea wao.

Kocha ndiye tatizo lingine, amewaamini wacheza wadogo, wasiona uzoefu katika ligi, hana mbinu binafsi za kuifanya timu ishinde, anabahatisha.
 
Hata akifukuzwa ni ujinga wake. Unakubali vipi kupewa mkataba bila kuhakikisha utapatiwa unachotaka?

Nini kilimfanya akubali Herrera aondoke wakati anajua hatopewa mid.kama Herrera?

Nini kilimfanya akubali kumtoa Lukaku bila kuhakikisha atapewa #9 mwingine? Unamtegemea Rashford

Unamtoa kwa mkopo Sanchez? Unabaki na nani?

Acha aishushe timu daraja kwanza ili akaitengeneze
Point ya mwisho nimeielewa saaana hiyo
 
Haya ni mapito tuu.

Kosa kubwa saana ni swala la watu kuamini kwamba ili man u ifanikiwe inahitaji aje mtu wa kurestore zile philosophy za sir alex. Au mtu mwenye kuijua vema united. Yan mtu anaekuja kuishi chini ya kivuli cha united. Hapo lazima tufeli tuu.

Sir alex alikuwa mjanja mjanja tuu timu inaweza kucheza vibaya na ikashinda alikuwa na average players but anashindana.

Man u inahitaji mtu mpya mwenye pholosophy zake mpya aunde timu upya sio kurudisha old philosophy ambazo haziwork out kwenye modern footbal.

Man u iache tabia ya kuwabeba watu wenye asili ya great britain. Vile alivyo kuwa anaandamwa lukaku ndio hivyo hvyo rashford awajibike.


Tutafute world class coach. Sio makocha wa field kama ole. Yupo kazin wakati yeye bado anasomea mbinu
 
Back
Top Bottom