Mimi nakubali kwamba kwa sasa sera ya United ni kuangalia waliopo nyumbani kwanza lakini kama hawapo anatafutwa hata mchezaji ambaye sio English ili mradi awe na uwezo
Koullibally ni Muingereza? Mbona United walimtaka lakini walipotajiwa bei ya kiwehu (£130m)wakachapa lapa
Wakati dirisha linakaribia kufungwa tulimtaka Dyabala, je huyo ni Muingereza? Tulimtaka Ericksen, je huyo ni Muingereza?
Ligi nyingi tu zina mawinga wazuri lakini United wanaangaalia zaidi premier league proven player in relation to price. Walishanunua akina Depay, Walishanunua akina Fred lakini zili prove kuwa ni transfer mbovu (in relation to price) . Umeona Pepe amekuja kutoka League 1,ana goli 20+ na assist za kutosha, lakini umeona anavyo struggle EPL?
Chris Smalling amepelekwa mkopo Roma, kama kigezo ni Uingereza mbona OGS alikuwa anam prefer Lindelof na Maquire na si Maquire na Smalling au na Jones kwenye defense?
Ushindi wa 2008 wa UCL ulichagizwa na wachezaji mahiri wengi akiwemo CR7 lakini kulikuwa na English players wengi,na vikosi vya SAF vingi vimekuwa hivyo na amepata mafanikio na kama unamuangalia OGS ana copy vitu vingi vya SAF
Kama kwenye kikosi chako haumtaki Maquire, Harry Kane, Sterling, Bissaka, Daniel James, Mount, Sancho eti kisa ni Wachezaji wa kiingereza utakuwa una xenophobia mbaya sana
Mbona hatujasikia approach yenu kwa Right-Wingers wengine kama waliopo sokoni kutoka Ligue 1 etc?
Ukisema kwamba mmechukua UEFA kwa nguvu ya wazawa hilo nitakukatalia sababu ile UEFA yenu ya mwisho CR7 alikuwepo
Pursuits zenu za wazawa mtupu (Longstaff, Rice,Sancho and the like ), halafu subiria Chelsea watoke kifungoni kama Abramovic atakuwa na roho nyeupe by then uone pursuits zao
Yaani hata Arsenal sajili zao ziko vizuri kama wanaamua kuspend, Utd ya sasa wazawa (sio homegrowns to be precise) ndio kipaumbele