tukiachana na mazoezi ya viungo na lishe nafikiri solution nyengine kubwa ya kutibu hilo tatizo ni kuwapa nafasi ya kucheza
mara kwa mara wapate kuzizoea changamoto kutoka kwa wapinzani.
greenwood akitembea na mpira anapepesuka kama mlevi sijui ni uoga unaotokanwa na majukumu makubwa wanayobebeshwa?
sisi tunahitaji greenwood, chong, gomez na james watupe matokeo kwa sababu hatuna wengine wa kuwategemea lakini ukiziangalia timu nyengine mfano barcelona hali ni tofauti kwa young stars.
nilimuangalia
ansu fati kwa dakika 30 mechi ya jana dhidi ya valencia kiukweli alikuwa anacheza akiwa huru kabisa kifikra na kimwili kwa sababu ya waliomzunguka ndani na nje ya uwanja, benchi yupo messi, dembele na suarez kwa nini uwe na khofu?
ukiziangalia hata movements zake hazina utofauti mkubwa sana na rashford.
==========================================================
genius maddison + tielemans + ndidi = hawa wajinga jana walituvuruga sana mpaka ikawa natamani umeme uzimwe nisiishuhudie tena ile mechi.
tusije kuwaruhusu man city wakamsajili james maddison tutakuwa tumefanya makosa makubwa sana hapo mbeleni, nawakumbusha tu david silva msimu huu huenda ukawa ndio wa mwisho kwake.
sidhani kama guardiola ataendelea kumuamini phil foden kama mrithi sahihi wa muda mrefu wa david silva