Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Lukaku ni bonge la striker pamoja na ubovu wake goli 10 uhakika sasa hawa wenye dna ya manchester hata goli 7 kufikisha bila penat mtihan
Hakuna kocha mwenye akili anayeweza kumuuza lukaku

Matatizo yake ni madogo sana na anaweza kuyabadilisha kwa muda mfupi, nayo ni kuongezeka uzito wa mwili, ambapo ilikuwa ni kumpangia tu ratiba ya mazoezi na misosi.

Kwa hali ilivyo sasa natamani pogba aende real tu ili kuepusha kuzidi kupoteana,
 
Harry maguire anahusika na nini hapa umetia wivu

Kwa upande wa lukaku siku ya kwanza tu nilijua kocha kabugi huwez kujenga timu bila wajuz angalia klopp alivyoanza na liverpool alichomoa wazoefu wabovu taratibu huyu sosha dirisha moja kafukuza wazoef si chini ya wa 5

Hilo jambo lipo arsenal kama la sosha nako kule hamma jipya yamejaa mazeee ya bure tu
Unatutafuta Arsenal , sisi tumeondoa deadwood karibu 90% ,na tunaleta quality tupu,

Wazee arsenal hawazid wanne ,Ozil ,luiz ,sokratis
 
20190831_165201.jpeg
 
Mkuu kumbuka mwanzo ulikuwa unapigania overhaul ya squad nzima sasa imefanyika malalamiko ya nini ?

Ole ni Mwalimu Mzuri tu kinachomwangusha ni quality of players tu
Hamna kocha hapo,Ole hamna kitu.

Ni mchezo wa tatu huu anaona kabisa mfumo anaotumia ni wakubahatisha ushindi lakini bado anakomaa nao.

Kumpanga Pogba na Scott pale kati ni kumpa kazi Scott ambae bado ni dogo tu, na pia ni kuwapa kazi mabeki. Pogba hakabi,muda wote anatembea tu na akipewa mpira 'anaulambalamba' na kuupoteza.

Nilitegemea kama amekomaa na hiyo 4-2-3-1 yake basi hiyo '2' ingekuwa Matic na Scott bishoo Pogba apande 10. Sasa Ole hajirekebishi na mchezo unaokuja atarudia utumbo wake. Sasa anakuwaje mwalimu mzuri huyo?

Na hiyo ni Soton kiungo kinapata shida hivi, nasubiri kuona kiungo cha Ndombele-Sissoko- Eriksen tutawatafuta akina Pogba tusiwaone mpaka mpira unaisha.

Unafukuzia mbali Sanchez na Lukaku ili Rashford atambe, tazama leo D.James anamimina mipira kati tena ya kuingia nayo kwenye nyavu Rashford haonekani.

Tena kwa huyu D.James anavyokimbia na vila anamimina mipira kati hii ndio ilikuwa kipindi cha Lukaku kutamba na uzito wake kama Tembo kugusa mipira tu uzame nyavuni.

Sijui kama Christmas itapita huyu Ole hajatolewa kafara.
 
.....siwezi kusahau maneno ya Brendan Rodger, alisema baada ya Ferguson kustaafu United itapita kwenye wakati mgumu sana. Na ndio tunachokiona kwa sasa.

Na akaongeza, united fans mnabidi muwe na roho ngumu kama wale wa liverpool na Milan ya Gang Chomba. Ufalme wenu umeshafika mwisho. Itapita miaka na mikaka kurudia enzi zenu.
 
Back
Top Bottom