Unataka kuniambia kati ya wachezaji maelfu dunia nzima unasema hujapata unaowataka?
Man Utd ina scouts wengi kuliko timu yeyote ile. Wameshindwa kuona vipaji?
Huu ni uongo wa wazi kabisa.
Man Utd haichukui mchezaji yoyote katika maelfu, ingekuwa hivyo tungekuwa tuna kiwango cha mtibwa..... Na utd isingekuwa United. Not all players can be United players
Pili OGS ana vigezo vyake anavyovitaka kwa mchezaji kwa hiyo sio kila mchezaji atakayekuwa identified atasajiliwa. Huyo Bruno Fernandez tumemscout kwa msimu mzima wa mwaka jana lakini hatukumchukua (japo mimi pia namkubali sana). Unaambiwa kwa structure ya sasa pale United katika usajili kuna scouts, kuna Phelan+OGS, kuna mtu anaitwa Mat Judge na Murtough (hapa kuna Head of Corporate Development na Chief Scout na negotiator mkuu) hawa wakiafiki kununua mchezaji wanampelekea Ed ili aandike check.
Tatu United wamebadili sera kwenye kusajili wachezaji. United imepigwa kwa wachezaji wengi, kuna Sanchez, Fred (haendani na bei aliyonunuliwa)na wengine wengi, hivyo hawataki kurudia makosa ndio maana pengine hawajawaona hao maelfu unaowataja. Ukishaumwa na nyoka, jani likitingishika tu lazima uogope.
Pia sio kwamba United haoni wachezaji. Kati ya wachezaji waliokuwa wanawataka ni Sancho ambaye tumeshindwa kumpata sababu ya kutoshiriki Champions League.
Tulimtaka Varane lakini alikuwa kwenye category ya impossible targets. Tulimtaka Koullibally, Napoli wakahitaji £150milion. Scout walimuona Longstaff lakini Newcastle wakataka £50milion, je tungemnunua hivyo hivyo? Nakubali United kuna sehemu tunafeli kwenye transfers, lakini sometime nawaelewa wanavyokuwa makini ili wasikurupuke kama tulivyokurupuka huko nyuma.
Kwa hiyo kusema United hawaoni wachezaji ni kujidanganya. Akina Bailly, Lindelof, Daniel James, Martial, Pogba (alivyokuja academy), na hawa watoto wote unaowaona leo pale United ni kazi ya scouts