severinembena
JF-Expert Member
- Jun 2, 2018
- 2,435
- 2,402
Kupitia link gani au channel gani?Nacheki game hapa ya Man U huku mbele bado sana
Kupitia link gani au channel gani?Nacheki game hapa ya Man U huku mbele bado sana
Wazee mnaoangalia hizi mechi za pre-season Tuanzebe mnamuonaje??
Kupitia link gani au channel gani?
Ni mtoto na Ana potential, work rate yake ni kubwa na anafit profile ambayo Ole anaitaka, hasa Mpira wa speed na counter Attack. Uliona mechi ya Leeds ile counter Aliyogonga mwamba? Beki alikuwa Kama anatembea vile. Unaweza kuangalia hapaDanny amenunuliwa kwa makusudi yepi sasa
Mimi naamini inabidi kwanza uwe na washambuliaji wakali kabla ya kuanza kuangalia nafasi nyingine..Yupo vizuri Beki zote zinapiga kazi Fresh ishu washambuliaji
Sawa nduguNacheki Man U tv Mkuu
Naangalia hii mechi ya Inter milan nabaki kucheka tuDunia inaenda kasi sana
JAMES ,RASHFORD, MARTIAL kwa safu hii na nyie kabisa mnajihesabu kichwani mnategemea kombe msimu ujao nyie watu mnautani na mpira sana.
Martial + Rashford + Lingard = Ni kupiga maritime tu na kupoteza muda Qualify yao ni ndogo mno
Yeah, sureFootball is entertainment bwana
Mkuu nimekuelewa sana especially Para ya kwanza, mimi pia nipo hivyo, hata Jose nilimsapoti enzi zakeMkuu Kama unataka kuona mafanikio ya kocha Fulani na mahala anapoweza kutupeleka Jambo la kwanza ni kuheshimu mawazo yake na kum support anachotaka kufanya. Ili Hata akizingua awe anafukuzwa kwa haki,
Hilo la Lukaku kufunga Magoli mengi si Hoja, Aliondoka Van Nistelroy sababu ya Ronaldo Japo kipindi hicho 2005/06 RVN alikuwa Bonge la Super star na ana average ya Magoli 30 kila msimu, Ronaldo ilikuwa Hata huwezi kumuweka level moja na RVN.
Timu yetu mpaka Sasa hakuna Hata tetesi ya Right wing, left wing yenyewe ukimtoa Daniel James hakuna Hata mmoja anayeweza kumlisha Lukaku, kwa the way Timu yetu ilivyo Sasa hivi ni Jambo la busara kumuuza Lukaku, and I hope watanunua striker Hata wa sub kuja kujaza nafasi yake, hasa tetesi za Ben Yedder.
Mfumo wetu msimu ujao Kama unavyoonekana utakuwa hauna Tena mtu wa kusimama mbele, Cross zitakuwa Nadra, watu watatumia zaidi dribling skills na pace, sioni Lukaku akishine kwenye huu mfumo Sana Sana tutampotezea tu muda wake.
Mkuu kwa ninavyoelewa akiuzwa Lukaku tuna activate clause ya Striker, tetesi zilisema Ben Yedder. Kwa club kubwa Kama Yetu hatuwezi kuwa na striker mmoja tu.Mkuu nimekuelewa sana especially Para ya kwanza, mimi pia nipo hivyo, hata Jose nilimsapoti enzi zake
Hata Ole namsapoti hadi leo, lakini isinizuie kutafakari maamuzi yake critically
Mfano wa Van Nestroy ni mzuri lakini hauendani na mazingira ya United ya sasa. Wakati anaondoka alikuwepo Rooney, nafikiri na Saha na wengine
Kwa sasa anaondoka Lukaku anabaki nani kaka? Rashford? Martial? No way, labda tutafute mwingine.
Greenwood is too good, but is too young
Martial is too inconsistent, Rashford is too unsettled in front of a goal
Lukaku anahitaji wingers ili afunge, ni kweli.... Why not buying a winger then?
Simba vs Sevilla mkuu
Issue ya Guardiola mkuu tumeshaizungumzia humu, ni kazi ya kina Tixi Begiristain, mkuu usiangalie tu mafanikio ya nje ya club ukajua ndio sababu ya hayo mafanikio.
Kabla ya Pep, Man city walianza zamani kuchukua viongozi wa Barca, Huyo Tixi ndio Dof wa City Sasa hivi na yupo na wenzake wengi. Hao jamaa wanajua wanachokifanya na kabla pep kuja tayari walianza usajili wa wachezaji pep anaowataka ama kocha anaefanania na yeye. Ndio maana unaona kina de bruyne, Fernandinho, Sterling etc hawakusajiliwa na pep ila wanafit mfumo wake.
Hawasajili tu eti sababu Mchezaji Fulani makubwa anapatikana, Bali wanasajili Mchezaji anaecheza mfumo Fulani pekee, kifupi Wana identity Kama vile ilivyo Barca.
Upande wetu tuna jambazi kuu Woodward, yeye Maisha yake yote ni banker anajua tu hela, elimu yake ya mpira ni 0, ana mamlaka yote ya usajili, analeta watu ambao watauza zaidi jezi kuliko ku improve timu. Yupo Radhi namba ikae miaka 7 bila mtu as long as hajapata mtu anaemhitaji. Hata Guardiola angekuja Man U asingefanya lolote.
Na mkuu tumesajili watu kibao msimu wa kwanza tu wa LVG kama
-shaw
-Falcao
-Di Maria
-Blind
-Rojo
-Herrera
Wachezaji 6 dirisha moja.
Kifupi Mou na LVG wamesajili so chini ya wachezaji 23, ndani ya miaka 4, hio ni timu nzima.