Kipindi alichonunuliwa Benteke tayari soko lilishaanza kuwa Crazy Market, kwahiyo £32.5m ilikuwa ni ya kawaida tu ingawa hakustahiki kununuliwa kwa bei hiyo.
Lakini kumbuka kuwa tulimuuza Palace kwa bei ambayo almost ni hiyohiyo! Kwahiyo hatukumuuza kwa hasara.
mashabiki wa manchester united tumeanza kusumbuliwa na wivu wa kijinga na hali hii imetokana zaidi na mafanikio ya wapinzani wetu.
miaka 18 iliopita bwana ferguson alitumia paundi millioni 30 kwa ajili ya kumsajili rio ferdinand kutoka leeds united, si hivyo tu pia SAF alitumia paundi millioni 28 kwa kumsajili juan sebastian veron labrujjitta kutoka lazio, miongo miwili iliopita tulikuwa tunapata mafanikio makubwa sana ndio maana hakuna aliyehoji fedha iliotumika kufanya usajili wa rio, rooney na veron.
kinachotokea hivi sasa ni kwamba tunatumia hela nyingi kufanya usajili halafu wachezaji wanaokuja wanashindwa kufikia malengo yaliotarajiwa ndio maana tumekuwa mabingwa wa kulalamikia soko chafu la usajili tofauti na nyakati zile tunawasajili rio, rooney, berbatov, nistelrooy kwa gharama kubwa.
wivu wa mashabiki wa man utd unakuja pale tunaposhuhudia majirani zetu wa man city na liverpool wanatumia hela kubwa kufanya usajili halafu takribani asilimia kubwa ya wachezaji wao wanaowaleta wanafikia matarajio ya klabu zao.
mohammed salah = amefikia matarajio ya liverpool
fabinho = amefikia matarajio ya klabu
allison becker = amefikia matarajio ya klabu
van virgil = amefikia matarajio ya klabu
sadio mane = best player
naby keita = hakuwa na msimu mzuri na miongoni mwa sababu ni majeruhi pamoja na mwalimu kubadilika na mifumo ya uchezaji.
lakini ukija kwetu mambo hayaeleweki kuanzia paul labile pogba, lukaku, matic, sanchez mpaka fred the red wote wamekuwa na homa za vipindi.
kwa makusudi unalipa paundi millioni 50 kwa wan bissaka halafu unalalamikia crazy market wakati thomas mounir yupo thamani yake ni paundi millioni 25.
maisha yote mshindi ndiye mwenye haki ya kuandika maandishi ya kihistoria hata kama ni ya uongo yataaminiwa, kwa sasa liverpool na man city wameshakuwa washindi.
liverpool wameshasahau kama miaka iliopita waliwasajili carrol, benteke, lazar markovic, aquilani, balotteli, david ngog, lambert, konchesky kwa sababu maumivu ya miaka 30 yanasahaulishwa na furaha ya siku moja.
vile vile maumivu ya miaka 6 yanasahaulisha furaha ya miaka 20