Chief-Mkwawa ukipata muda naomba uniondolee mavumbi yaliobaki kwenye ubongo wangu kuhusiana na hii sheria ya financial fair play kuna mambo bado sijayafahamu kiundani
barcelona wamemuuza golikipa cillesen kwa euro millioni 35 siku chache zilizopita kuelekea valencia.
barcelona wamemsajili golikipa neto kutoka valencia kwa euro millioni 26 na ongezeko la euro millioni 9.
ukiziangalia hizi gharama walizozitumia kwa malipo zinafanana, kwa nini hawakufanya swap deal?
nimesoma taarifa kupitia vyanzo tofauti klabu ya valencia wanahitaji takribani euro millioni 30 kwa ajili ya kufunga vitabu vya matumizi kwa mwaka huu unaoelekea kuisha ili wasipate hasara, ina maana mkataba wa cillesen kwa elimu yangu dhaifu utafungwa July 1 ambapo ndio mwanzo wa mwaka mpya wa soka barani ulaya ili valencia waepukane na rungu la FFF.