Nimesoma Ole anataka kumpa ukapteni Pogba kumshawishi asiondoke.

Nshaona dalili za huyu jamaa kutoondoka.
Pogba mwenyewe anataka kuondoka hata last week kwenye interview Evra alisema Pogba ataondoka issue ni timu zinazomtaka zimeanza kutafuta altenative na kikwazo kikubwa ni mshahara wake,OGS anajua hilo ndio maana anajaribu kumshawishi abaki
 
Hiyo ndiyo bajeti inayotajwa kuwa Tajiri yupo tayari kuitoa (£200m-£250m)

Lakini pia Tajiri yupo tayari kutoa fedha yoyote itakayopatikana Baada ya kuuza wachezaji waliopo sasa

Pia OGS amewahi kusema kwamba hategemei kusaini wachezaji 6
Kwa hiyo bajeti tusishangae Ole akileta wachezaji wasio na majina.
 
Pogba mwenyewe anataka kuondoka hata last week kwenye interview Evra alisema Pogba ataondoka issue ni timu zinazomtaka zimeanza kutafuta altenative na kikwazo kikubwa ni mshahara wake,OGS anajua hilo ndio maana anajaribu kumshawishi abaki
na udhaifu aliokuwa nao paul pogba, ukweli tetesi za kuondoka kwake hazinifurahishi hata kidogo. Tupo katika nyakati ambazo hatulazimiki kumruhusu mchezaji muhimu kuondoka.

wanaosema paul pogba si mchezaji muhimu klabuni wanajidanganya
 
Hata mkopo. Ila msimu uliopita wamechangia maovu mengi sana.
tatizo linakuja kwenye market.
unataka kumuondoa smalling na jones kwa wakati mmoja halafu bajeti yako ya usajili ni paundi millioni 200.
unahitaji winga
unahitaji kiungo wa chini baada ya kuondoka herrera
unahitaji playmaker
unalalamika striker wako ni butu
unahitaji mlinzi wa kati
unahitaji mlinzi wa kulia


hatuna jeuri ya kufanya mabadiliko makubwa kama hayo, ni man city pekee ndio wenye jeuri hiyo.
 
Mkuu hatuna winga teleza kabisa, huyu mtoto msingi mbio, mechi na city aliwaacha otamendi na walker kama wamesimama, tunahitaji mtu wa kutia njaaa kule pembeni. Hakuna mchezaji yoyote kwenye ligi sasa hivi anayemfikia kwa speed ame peak 37mph na fastest msimu huu tfm ni around 35mph. Pia ni mzuri anakaba. Ana potential ya kuwa mchezaji mkubwa itategemea na atakavyolelewa.

Dah alivyowaacha jamaa hatari
 
Nimesoma Ole anataka kumpa ukapteni Pogba kumshawishi asiondoke.

Nshaona dalili za huyu jamaa kutoondoka.
Pogba haendi popote kwa sasa, Man u hawatakuwa tayari kupoteza kipaji na mapato unless OGS mwenyewe aseme hamuhitaji publicly au asimpe nafasi kikosini.

Japo ningependa aondoke ili timu ipate mbadala wake na iwe stable kwenye midfield kuliko hivi sasa inajaribu kila mfumo kumuaccomodate lakini bado mambo hayaendi sawa sawa.
 
tatizo linakuja kwenye market.
unataka kumuondoa smalling na jones kwa wakati mmoja halafu bajeti yako ya usajili ni paundi millioni 200.
unahitaji winga
unahitaji kiungo wa chini baada ya kuondoka herrera
unahitaji playmaker
unalalamika striker wako ni butu
unahitaji mlinzi wa kati
unahitaji mlinzi wa kulia


hatuna jeuri ya kufanya mabadiliko makubwa kama hayo, ni man city pekee ndio wenye jeuri hiyo.
Fans wanataka timu isajili wachezaji kumi at once tena world class talent ili smalling na Jones waondoke tu.

Of course tunataka overhaul ila siyo kwa mtindo huo timu itashuka daraja
 
HAWA WAKITUA MAN UNITED LAZIMA HESHIMA IRUDI BWANA


SIO siri msimu wa 2018/19, umekuwa moja ya misimu mibaya zaidi kwa Manchester United kwenye Ligi Kuu England. Walipoteza mechi nane katika michezo 12 ya mwisho ukiwemo ule wa kufunga pazia la msimu.
Mashetani wekundu walipokea ubatizo wa moto kutoka kwa Barcelona (3-0), katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Wakapigwa na Everton (4-0), kabla ya kupokea kichapo cha 2-0, kutoka kwa vibonde Cardif City, walioshuka daraja.
Tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, United hawajatwaa ubingwa wa EPL hata mara moja, licha ya kusajili mastaa kadhaa kama, Paul Pogba, Alexis Sanchez, Angel Di Maria na Romelu Lukaku. Mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2013.
Ukiachana na ubutu wa safu ya ushambuliaji, Man United pia imekuwa na tatizo katika safu yao ya kiungo na beki. Msimu ujao, endapo Ole Gunnar Solskjaer, atawapata nyota hawa watano, watamsaidia kurudisha heshima pale Old Trafford.
5. Paulo Dybala
Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa, Muargentina huyu, yuko njiani kuihama Juventus. Wakala wake, ambaye ni kaka yake, Gustavo Dybala, hivi karibuni alinukuliwa akisema staa huyo, hana furaha kabisa pale Turin.
Mshambuliaji huyu wa zamani wa Palermo, huenda akapata amani baada ya kuondoka kwa Massimiliano Allegri, ambaye hakuwa na mzuka naye kabisa, lakini United bado wanaweza tumia mwanya wa matatizo yake uwanjani, kupata saini yake.
Kiwango cha Dybala, kim kuwa kikiporomoka kila uchao, tangu Cristiano Ronaldo alipotua Turin. Msimu uliomalizika amefunga mabao matano tu, tofauti na msimu uliopita ambao alifunga mabao 22. Vita vya mafahali wawili, vinamkimbiza Turin.
Kutokana na staili yake akitua Old Trafford basi ni mzuka sana kwani, hauna tofauti na uchezaji wa Lionel Messi na itakuwa ni rahisi kuwa staa na kumfunika Lukaku. Uhusiano wake mzuri na Paul Pogba, utaisaidia sana Man United kurejesha heshima yake.
Aidha, Dybala sio mchoyo. Hii itaongeza kasi ya ushambuliaji ya United, ambayo tayari inajivunia uwepo wa Marcus Rashford na Anthony Martial. Hebu piga picha itakuwaje kama Man United ikiwasimamisha Dybala, Rashford na Martial pale mbele?
4. Aaron Wan-Bissaka
Kinda huyu wa Uingereza, amekuwa sehemu ya ngome isiyopitika ya klabu ya Crystal Palace. Ni mmoja wa wachezaji walioisaidia, kufanya vizuri msimu huu. Aaron Wan-Bissaka, anatajwa miongoni mwa mabeki bora waliopo kwenye ligi tano kali za Ulaya.
Rekodi inaonesha kuwa, ana wastani 3.7 wa kupokonya mipira, wastani wa kuzuia mipira 2.4 na 3.7 ya kuondoa hatari. Pia ni mzuri hewani, ambapo ana wastani wa 1.2 ya kushida mipira ya juu, jambo linalochangiwa na urefu wake.
Mbali na ubabe wake katika safu ulinzi, Wan-Bissaka ana rekodi nzuri ya kupandisha mashambulizi, ambapo ana asisti tatu. Ukiangalia beki ya United, kwenye msimu wa 2018/19, utaona wameruhusu mabao mengi sana msimu.
Ujio wa Wan Bissaka, utawaongezea nguvu kina Ashley Young, Phil Jones na Chris Smalling, pale nyuma. Huyu ataisaidia kikosi kuwa huru zaidi, lakini atamkinga David de Gea, kutokana na dhoruba kali pale langoni.
3. Matthjis de Ligt
Kila mtu ameshuhudia namna ambavyo Liverpool, walimwaga fedha nyingi kuipata huduma ya mchezaji bora wa EPL, msimu wa 2018/19, Virgil van Dijk, ambaye kwa kiasi kikubwa ameifanya Liverpool, kuwa moja ya klabu bora Ulaya.
Man United wanaweza kuwaiga Liverpool, kwa kumsajili nahodha na beki wa Ajax, Matthijs de Ligt.
Kinda huyu wa Uholanzi, ana uwezo mzuri wa
kukaba, kushambulia na kuongoza jahazi uwanjani. Ni mfungaji mzuri, lakini pia ni mfia timu.
Msimu huu, ameiongoza Ajax kutwaa ubingwa wao wa 34 katika Ligi Kuu ya Uholanzi, baada ya miaka sita, na ubingwa wa KNVB Beker, huku pia wakifika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kishindo, wakiwabwaga mabingwa watetezi Real Madrid na Juventus.
Matthijs de Ligt (19), ni mzuri katika mipira ya juu, na anaweza tengeneza kombinesheni nzuri na Phil Jones na Chris Smalling, kama sio kuziba pengo lao. Anahusishwa pia na Barcelona, lakini hakuna dili iliyosainiwa, hivyo United wana nafasi kama itaamua kumfuata.
2. Jadon Sancho
Nyota ya Jadon Sancho, imeendelea kung’aa tangu alipojiunga na Borussia Dortmund, akitokea Manchester City, mwaka 2017. Uhamisho huo, ulimshuhudia kinda huyu wa Uingereza akibadilika kutoka mchezaji wa kawaida, hadi mmoja wa mastaa wanaowindwa zaidi duniani.
Thamani yake pia imepanda maradufu. Hivi sasa, kumpata Sancho (19), lazima uwe tayari kulipa Euro 100 milioni. Msimu huu, amefunga mabao 11, na kuongoza kwa asisti, kwenye Bundesliga. Kwa muda mrefu amekuwa akihusisha na mashetani wekundu.
Tangu achukue mikoba ya ukocha pale Old Trafford, Ole Gunnar Solskjaer, amekuwa akihangaika kupata winga tegemeo, kwenye kikosi chake bila mafanikio. Juhudi za kuwajaribu Jese Lingard, Martial, Juan Mata, na Alexis Sanchez, katika nafasi hazijazaa matunda.
Martial na Rashford, ni aina ya mawinga wanaopenda kufunga kuliko kutoa krosi za mabao. Hapa ndipo ubutu wa Lukaku unapoanzia. Ujio wa Sancho unaweza kuwa tiba sahihi kabisa kwa Lukaku.
1. Thiago Alcantara
Kiungo huyu, raia wa Hispania, hakuweza kupata namba ya kudumu katika kikosi cha Barcelona, licha ya kuwa zao la akademi yao ya La Masia.
Alianza katika mechi 15 za msimu mzima wa 2012/13. Hata hivyo, Pep Guardiola, alipompeleka Bayern Munich (2013), aliionesha dunia nzima, uwezo wa miguu yake. Alianza kwa kasi ya kusuasua pale Allianz Arena, lakini kwa sasa, kila kitu kimebadilika.
Amekuwa Staa katikati ya kundi la wajerumani. Alcantara ni aina ya kiungo, ambaye Solskjaer anamtafuta. Ni injini yenye uwezo wa kupiga pasi, kupiga chenga, kufunga mabao na wakati huo huo, akakaba mpaka kivuli cha wapinzani. Ni mrithi sahihi wa kiatu cha Ander Herrera, aliyeondoka Old Trafford.
 
DE GEA AWAGOMEA MAN U


Manchester United ipo katika presha kubwa ya kuuza kipa wake David de Gea baada ya ‘kukataa dau la mwisho alilopewa’ huku Paris Saint-Germain ikiwa tayari kumsajili kwa pauni 60milioni.
Mabingwa wa Ufaransa, PSG wapo tayari kumlipa De Gea kiasi anachotaka cha pauni 350,000 kwa wiki huku wakiweka wazi wapo tayari kutoa pauni 60milioni kumsajili msimu huu.
De Gea ameshinda tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu England katika misimu mitano kati ya saba, huku ndani ya Man United ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa misimu minne mfululizo kati ya 2014 and 2018.
Vyanzo vya ndani vya mtandao wa The sun, vimebaini kuwa kipa huyo, anadaiwa kuweka wazi kwamba hayupo tayari kuendelea kusalia Old Trafford msimu ujao wa 2019/20.
 
DE GEA AWAGOMEA MAN U


Manchester United ipo katika presha kubwa ya kuuza kipa wake David de Gea baada ya ‘kukataa dau la mwisho alilopewa’ huku Paris Saint-Germain ikiwa tayari kumsajili kwa pauni 60milioni.
Mabingwa wa Ufaransa, PSG wapo tayari kumlipa De Gea kiasi anachotaka cha pauni 350,000 kwa wiki huku wakiweka wazi wapo tayari kutoa pauni 60milioni kumsajili msimu huu.
De Gea ameshinda tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu England katika misimu mitano kati ya saba, huku ndani ya Man United ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa misimu minne mfululizo kati ya 2014 and 2018.
Vyanzo vya ndani vya mtandao wa The sun, vimebaini kuwa kipa huyo, anadaiwa kuweka wazi kwamba hayupo tayari kuendelea kusalia Old Trafford msimu ujao wa 2019/20.
dean henderson anatosha degea wa nini?

ENGLAND UNITED
1. dean henderson2 wan bissaka3. luke shaw5. smalling4. lindeloff6. declan rice7. daniel james8. sean longstaff9. rashford10. pogba11.zaha
1104699
 
Back
Top Bottom