Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
12,444
2,000
man u.png

Full name: Manchester United Football Club

Nickname(s): The Red Devils

Founded: 1878 as Newton Heath LYR F.C | 1902 as Manchester United F.C.

League: Premier League

Website: ManUtd.com

traford.jpg

Ground: Old Trafford, (Capacity: 74,994) - Pitch 105m x 68m

1.jpg

Co-Chairmen: Joel na Avram Glazer

1545569869324.png

Manager: Ole Gunnar Solskjaer

Manchester United Trophies:
League Tittles: 20

First Division/Premier League Champions: 20 (1907/08, 1910/11, 1951/52, 1955/56, 1956/57, 1964/65, 1966/67, 1992/93, 1993/94, 1995/96, 1996–97, 1998/99, 1999/2000, 2000/01, 2002/03, 2006/07, 2007/08, 2008/09, 2010/11, 2012/13)

European Trophies: 6
UEFA Champions League: 3 (1967/68, 1998/99, 2007/08)
UEFA Europa League: 1 (2016/17)
UEFA Super Cup: 1 (1991)
UEFA Cup Winners': 1 (1990/91)

FA Cup Trophies: 12 (1908/09, 1947/48, 1962/63, 1976/77, 1982/83, 1984/85, 1989/90, 1993/94, 1995/96, 1998/99, 2003/04, 2015/16)

League Cup: 5 (1991/92, 2005/06, 2008/09, 2009/10, 2016/17)

Community Shield: 21
FA Charity Cup/FA Community Shield: (1908, 1911, 1952, 1956, 1957, 1965, 1967, 1977, 1983, 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011, 2013, 2016)

Other Trophies
Second Division Championship: 2 (1935/36, 1974/75)
Intercontinental Cup: 1 (1999)
FIFA Club World Cup: 1 (2008)

1.jpg

Manchester United Trophies' Cabinet

Kombe.jpg

Manchester United Football Club celebrate as they Crowned Europa League Winners(2016/17)

IMG_20190613_160926.jpg

Manchester United Premier League fixtures for 2019/20

Follow this thread for team updates!
 
Last edited by a moderator:

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
13,555
2,000
Hivi klopp aliikuta liverpool ya namna gani? Kwani mlivumilia si mlikuwa mnapiga kelele lakin mambo yanabadilika taratibu ndivyo ilivyo hata mwaka 2003 timu chini ya sir alex ilipotea kwenye zile timu zenye ushindani baran ulaya tulikuja kurudi strong kuanzia 2006 hata kama akisema ananunua wachezaj wa bei ghali unajua ni kwa namna gani watarudisha hadhi ya timu?
Hapo juu nimekupa mfano wa psg inakila kitu bado wanatolewa na awakina andres pereira na scott mctominay
Naielewa point yako, Klopp kaikuta Liverpool ni mbovu na tumekuwa tunaendelea kulia.

Tofauti ya sisi na ninyi ni uvumilivu, sisi tumeshakaa miaka mingi bila kombe hivyo ni kama tumeshakuwa sugu, tuna kauvumilivu fulani ka kumpa muda kocha. Ninyi ndiyo kwanza miaka 6 imeisha, bado usugu haujaja, swali ninalojiuliza ikitokea next 2 season mkaenda kapa, OGS mtamwacha?

Umezungumzia 2003, hiyo ilikuwa chini ya mkufunzi mkuu ambaye hajapata kutokea, alikuwa amesha-prove beyond reasonable doubt kwamba ni winner, na hata akisema nitawarudisha juu mnaelewa, anaweka mipango mezani mnachotakiwa ni kutekeleza upande wenu na yeye upande wake, huyu OGS ndo kwanza amepewa ajifunzie Man Utd.
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
7,450
2,000
Mkuu hakuna mtu anayetaman Mou arud OT, Mou aliaret tatzo mapema ila akaonekana miyeyusho, kufeli kwake kunachangiwa na mambo mengi, hata alipoondka chelsea aliyekuja alifanikiwa ila mwaka wa pili tatizo lile lile likaibuka pale chelsea na kocha akafukuzwa.....

Unaweza kumdharau ila jamaa CV yake ni kubwa sana, tangu aondoke fergie, Mou ndo kocha mwenye mafanikio zaidi pale OT...
Mkuu hivi unajua kipindi cha miaka miwili ya Mou alisajiri wachezaji 11 kwa zaidi ya pound million 300..
Ulitaka apewe nini zaidi ?? Ulitaka apewe nini zaidi ??

Anyway Mimi nakubali CV ya Mou ila naamini muda wake umeshapita. Enzi za kuangalia mechi unalowa jasho kwa kupaki basi umeshapata.
Unaangalia mechi t-shirt inaloa unakuwa huna tofauti na Smalling au Lukaku .. Wao wanatokwa jasho uwanjani na wewe unatokwa na jasho kibanda umiza ... Ukirudi nyumbani na wewe unapitilizia bafuni kuoga.Mwisho wa siku ni ukweli mchunngu, matatizo ya united si ya kutatuliwa kwa kwa msimu mmoja au miwili. Kama kuna shabiki anajiaminisha ndani ya miezi miwili timu itakuwa sawa namuonea huruma Sana...

Tunataka kocha wa kujenga timu si tu kwa sasa hata baada ya miaka 4 ijayo ..
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
7,450
2,000
Mkuu hakuna mtu anayetaman Mou arud OT, Mou aliaret tatzo mapema ila akaonekana miyeyusho, kufeli kwake kunachangiwa na mambo mengi, hata alipoondka chelsea aliyekuja alifanikiwa ila mwaka wa pili tatizo lile lile likaibuka pale chelsea na kocha akafukuzwa.....

Unaweza kumdharau ila jamaa CV yake ni kubwa sana, tangu aondoke fergie, Mou ndo kocha mwenye mafanikio zaidi pale OT...
Naomba unitajie hayo mambo yaliyomfanya mou akashindwa united ;

NB: Kumbuka ndani ya miaka miwili alitumia zaidi ya pound million 300+ kwa usajili!!!! Na alisajiri wachezaji 11 ....

Amini nakwambia kuna MAkocha ukiwapa hicho kiasi (Mfano Guardiola ) hutokaa uamini ...

Nasubiri majibu yako kwa hamu sana ...
 
  • Thanks
Reactions: Dae

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
18,640
2,000
Hahahahahhah Manchester United haina muda wa kusubiri wa kujenga timu kwa miaka 3 o f 4 United hawana upuuzi huo United sio Liverpool mkuu timu ikikosa kombe hata misimu 3 kocha haulizwi United wanahitaji wachezaji wakubwa ,timu ishinde Trophies then wafanye Business wapige pesa
Kocha anafukuzwa kwa kufanya vibaya uvumilivu ni muhimu kwa nini nasema hivyo mourinho na van gaal walipewa pesa za usajili watu walikuwa wakiangalia uwanjani na pesa waliyotoa vinaendana

Mourinho alitaka kujirekebisha kwa kuanza na mabaek na viungo washambuliaji hapa mm nilimuunga mkono kwa sababu had leo yanaonekana bodi haikuelewa kocha ambae kafukuzwa fasta alikuwa moyes huyu hakutumia pesa na hata alisema sikupewa pesa za machaguo yangu ya kwanza

Ila van gaal alichezea pesa

Nasema kufukuza kocha sio dawa haya OGS anaenda kuanza na program mpya itamchukua muda gani?

Liverpool msimu wa nne sasa timu ipo kiushindani zaidi je sisi?

Pep kaikuta city inawachezaj karibia 7 wametimia na nguvu zao hata anapo msajili Gabriel Jesus hafanyi la maana ubovu wake unafichwa na wakongwe au mendy ingekuwa ni timu mbov pesa za hawa watu zingeulizwa nani anajali mendy kukaa bench kwa ile pesa?

United bado hatuna jeuri ya kufukuza kocha halafu tukaingia top 2 teams

Angalia spurs alifukuza wakina paulinho na sandro hao ni viungo walikuwa wa maana kocha wa spurs alianza kujenga timu taratibu kwa kumzunguka harry kane leo ni kicheko tu japo levy anamuangusha huyu kocha
 
cosmonaut

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
1,250
2,000
Aliyesema hivyo ni OGS, kwamba atanunua wachezaji wa bei rahisi ili atengeneze kikosi cha namna hiyo.

Kwa case hiyo, means at minimum msimu ujao utakuwa mgumu zaidi, hivyo kama ni kuanza kuona matunda ni ule msimu mwingine. Ndiyo maana nikasema msimu ujao ni wa tabu kwenu.

Swali: Je, mna huo uvumulivu? Imagine sisi huu msimu wa nne umekata hatujapata kitu lakini tumo tu tumekubaliana kwamba Klopp anajenga timu. Mungu asaidie tupate hiyo UEFA.
Duh, Kama Kuna shabiki wa utd anategemea msimu ujau timu itakuwa kwenye mashindano ya ubingwa basi atakuwa kipofu na amezidi mahaba,(very Naive )........
Mafanikio ya juu kabisa inayoweza kuyapata utd msimu ujao Ni nafasi ya 5/6 maaana sidhani Kama kutakuwa na zari la kuyumba na kushuka kwa kiwango kwa timu za Asernal, Chelsea na Spurs kama ilivyoyoke msimuu.......
 
Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
3,237
2,000
Naomba unitajie hayo mambo yaliyomfanya mou akashindwa united ;

NB: Kumbuka ndani ya miaka miwili alitumia zaidi ya pound million 300+ kwa usajili!!!! Na alisajiri wachezaji 11 ....

Amini nakwambia kuna MAkocha ukiwapa hicho kiasi (Mfano Guardiola ) hutokaa uamini ...

Nasubiri majibu yako kwa hamu sana ...
Mkuu unapohitaj kocha wa kukurekebishia timu inabid umpe uhuru wa kutosha, manunuz pale OT kwa kias kikubwa yalichangiwa na issue za kibiashara na sio utashi wa kocha kwa 100%, kocha anaweza kusajili ndio ila usijidanganye kuwa ndo ametosha humuongezei hela tena, mabadiliko ni kila msimu, mpak timu inapokuwa stable.....

Mourinho alitumia mil 300, Guardiola ametumia more than one billion na bado anamwaga pesa sa hv kupata wachezaji wengine......kwan wakat wanamwajir Mourinho hawakujua kuwa style yake ni ya kupaki basi?? mbna inajulikana kwamba jamaa huwa anatengeneza timu kutokea kwenye defence, na anashambulia kwa counter, kuotea, na by mistake ya timu pinzani.....

sasa iweje umzuie kusajili et ametosha, ?
 
Tena siku nyingine acha kulinganisha "Kipara" Pep Guardiola na vitu vya kipuuzi kama Mourinho...

Sitakai soka la sasa ni kumwaga Pesa .. Nitajie na unilinganishie achievements z Mou na Guardiola katika kipindi cha miaka yao miwili katika timu zao .. Kama utafiti wako utaonesha Wamelingana au Mou kamzidi Guardiola Mimi nitaacha kuwa member na kuomba life bad humu jamii forum..

Lakini pia kumbuka kiasi alichotumia Guardiola ndani ya miaka miwili pale city ndio kiasi sambamba na kile kile alichotumia Mou united ... Kwanini matokeo chanya yaonekane city ?? .. Hapa sasa tunakuja kumdaka kocha .. Kocha ana uwezo mdogo ... Tena uwezo mdogo mno.

Haina haja ya kutoana mapovu kujua ubovu wa mou , rudi nyuma kidogo ulivyo guru my sh wa Chelsea kwa ibu.. Timu aliiacha ikiwa katikati ya msimamo ( Mid of the table )...

Mou anauzika sokoni kwa CV Na achievements zake kwenye soka .. Ni sawa na wakina Rafael Benitezi muda wao umeshakwenda na maji...Unasema Guardiola natumia 1 billion pound, nikuulize hiyo amount ameitumia kwa miaka miwili ?? Unadhani ndani ya miaka miwili asingefanya vizuri city wangekuwa na hamu ya kumuongezea Pesa za kusajiri ???

Mkuu mpira ni mchezo wa wazi Fanya kazi upewe hela ... Mou aliikuta timu Nafasi ya sita na kaiacha Nafasi hiyo hiyo . Hakuna alichoongeza zaidi ya kutafuna Pesa ..
 
Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
14,600
2,000
PANGA halikwepeki Manchester United. kocha wa kikosi hicho, Ole Gunnar Solskjaer amekuwa mkali na kusisitiza atawaondoa wachezaji wengi kwenye dirisha lijalo la usajili.
Hata hivyo, unaambiwa hivi kocha huyo huenda akagusa wachezaji wote, lakini si kinda Anthony Martial, ambaye mmiliki mwenza wa timu hiyo, Joel Glazer anamwona kama Pele wa Man United.
Martial kujituma kwake kwenye kikosi hicho kumetiliwa mashaka na makocha wote Jose Mourinho aliyeondoka na huyu wa sasa Solskjaer jambo linalotia wasiwasi mkubwa wa hatima ya Mfaransa huyo kuendelea kubaki Old Trafford msimu ujao.
Hata hivyo, kutokana na kuwa mchezaji kipenzi cha bosi, Martial anaweza kuwa salama. Januari mwaka huu, Martial alisaini mkataba mpya hadi 2023 ambao utamshuhudia akiweka kibindoni Pauni 200,000 kwa wiki.
Makamu Mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward naye anamwona Martial ni silaha ya siku za baadaye. Kipindi kile Mourinho alitaka kumwondoa ili kumleta winga Ivan Perisic, lakini mabosi Glazer na Woodward wakamtaka Martial kwenye timu.
Kutokana na hilo, Kocha Solskjaer atakuwa na orodha yake ya wachezaji kadhaa ambao hataguswa akiamua kuwaondoa kwenye kikosi hicho ili kupunguza bili ya mishahara na kuwanasa wachezaji wengine wapya watakaokuwa na faida kwenye timu.
Ripoti zinadai kuna orodha isiyopungua wachezaji wanane wataachana na maisha ya Man United kwenye dirisha lijalo la usajili, huku ikidaiwa kuna sura tano mpya zitatua hapo kabla ya Julai Mosi watakapoanza mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao.
Wachezaji Antonio Valencia na Ander Herrera hao hawatakuwapo Old Trafford msimu ujao, lakini panga la Ole huenda likapitia pia majina ya mastaa kama Matteo Darmian, Marcos Rojo, Eric Bailly, Juan Mata, Romelu Lukaku na Alexis Sanchez.
Kuna taarifa pia zinazomtaja Paul Pogba kuwa ni miongoni mwa mastaa watakaofunguliwa milango ya kutokea licha ya Bosi Woodward kumtaka mchezaji huyo aendelee kubaki Old Trafford kwa sababu za kibiashara.
Ole hataki mzaha na ndio maana kwenye orodha ya wakali wanaotajwa kwamba watapigwa panga Old Trafford kuanzia sasa wote ni mastaa wakubwa.
 
Walas Ba

JF-Expert Member
Sep 6, 2012
3,247
2,000
Boss wenu anasema hivi

BREAKING NEWS
Manchester United Executive Vice Chairman Ed Woodward is pledging to use Manchester United’s financial muscle to help Ole Gunnar Solskjaer with his Summer rebuilding plans after a season he’s labelled as “turbulent”.
As United release their Third Quarter Results, Woodward has said the “underlying strength of our business will allow us to support the manager and his team as we look to the future.”
The statement also hints that the preparations for the new season are well underway and Woodward adds that “everyone at Manchester United is focussed upon building towards the success that this great club expects and our fans deserve.”
Manchester United’s Third Quarter Revenues were up 3.4% to £152.1m with a 94% rise in operating profits to £14.2m. The club’s debt has remained pretty static at £301.7m a rise of £0.4m over the year.
 
  • Thanks
Reactions: Dae

alumelunda

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
648
1,000
PANGA halikwepeki Manchester United. kocha wa kikosi hicho, Ole Gunnar Solskjaer amekuwa mkali na kusisitiza atawaondoa wachezaji wengi kwenye dirisha lijalo la usajili.
Hata hivyo, unaambiwa hivi kocha huyo huenda akagusa wachezaji wote, lakini si kinda Anthony Martial, ambaye mmiliki mwenza wa timu hiyo, Joel Glazer anamwona kama Pele wa Man United.
Martial kujituma kwake kwenye kikosi hicho kumetiliwa mashaka na makocha wote Jose Mourinho aliyeondoka na huyu wa sasa Solskjaer jambo linalotia wasiwasi mkubwa wa hatima ya Mfaransa huyo kuendelea kubaki Old Trafford msimu ujao.
Hata hivyo, kutokana na kuwa mchezaji kipenzi cha bosi, Martial anaweza kuwa salama. Januari mwaka huu, Martial alisaini mkataba mpya hadi 2023 ambao utamshuhudia akiweka kibindoni Pauni 200,000 kwa wiki.
Makamu Mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward naye anamwona Martial ni silaha ya siku za baadaye. Kipindi kile Mourinho alitaka kumwondoa ili kumleta winga Ivan Perisic, lakini mabosi Glazer na Woodward wakamtaka Martial kwenye timu.
Kutokana na hilo, Kocha Solskjaer atakuwa na orodha yake ya wachezaji kadhaa ambao hataguswa akiamua kuwaondoa kwenye kikosi hicho ili kupunguza bili ya mishahara na kuwanasa wachezaji wengine wapya watakaokuwa na faida kwenye timu.
Ripoti zinadai kuna orodha isiyopungua wachezaji wanane wataachana na maisha ya Man United kwenye dirisha lijalo la usajili, huku ikidaiwa kuna sura tano mpya zitatua hapo kabla ya Julai Mosi watakapoanza mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao.
Wachezaji Antonio Valencia na Ander Herrera hao hawatakuwapo Old Trafford msimu ujao, lakini panga la Ole huenda likapitia pia majina ya mastaa kama Matteo Darmian, Marcos Rojo, Eric Bailly, Juan Mata, Romelu Lukaku na Alexis Sanchez.
Kuna taarifa pia zinazomtaja Paul Pogba kuwa ni miongoni mwa mastaa watakaofunguliwa milango ya kutokea licha ya Bosi Woodward kumtaka mchezaji huyo aendelee kubaki Old Trafford kwa sababu za kibiashara.
Ole hataki mzaha na ndio maana kwenye orodha ya wakali wanaotajwa kwamba watapigwa panga Old Trafford kuanzia sasa wote ni mastaa wakubwa.
Inapendeza
 
  • Thanks
Reactions: Dae

Mc cane

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,351
2,000
Aliyesema hivyo ni OGS, kwamba atanunua wachezaji wa bei rahisi ili atengeneze kikosi cha namna hiyo.

Kwa case hiyo, means at minimum msimu ujao utakuwa mgumu zaidi, hivyo kama ni kuanza kuona matunda ni ule msimu mwingine. Ndiyo maana nikasema msimu ujao ni wa tabu kwenu.

Swali: Je, mna huo uvumulivu? Imagine sisi huu msimu wa nne umekata hatujapata kitu lakini tumo tu tumekubaliana kwamba Klopp anajenga timu. Mungu asaidie tupate hiyo UEFA.
Mkuu embu nipe rejea aliposema ananunua wa bei rahisi

Wanatajwa

Pepe (Kati ya £45mil-£70mil)

Fernandes (Kati ya £60-£85mil)

Maguire (£75milion)

Sancho (£100)

Koullibaly (£75-100milion)

Daniel James (£15milion)

Conselo (£50milion)

Wan Bissaka (£40 million)

Reece (£45 million)

Hivi kusema anataka Wachezaji wenye vipaji na wenye njaa ya mafanikio tafsiri yake ni wa bei rahisi. Halafu si kila mchezaji wa bei kubwa ni mzuri, wengine ni virusi tu
 
Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
13,555
2,000
Mkuu embu nipe rejea aliposema ananunua wa bei rahisi
Wanatajwa
Pepe (Kati ya £45mil-£70mil)
Fernandes (Kati ya £60-£85mil)
Maguire (£75milion)
Sancho (£100)
Koullibaly (£75-100milion)
Daniel James (£15milion)
Conselo (£50milion)
Wan Bissaka (£40 million)
Reece (£45 million)
Hivi kusema anataka Wachezaji wenye vipaji na wenye njaa ya mafanikio tafsiri yake ni wa bei rahisi. Halafu si kila mchezaji wa bei kubwa ni mzuri, wengine ni virusi tu
Probably ni misinterpretation, nitaitafuta hiyo article ambayo OGS aliponda wachezaji kwenye bei na majina makubwa.

Akisema atajikita kusajili low profiled players.
 
Nyambiza jr

JF-Expert Member
Oct 5, 2018
805
1,000
Hahahahahhah Manchester United haina muda wa kusubiri wa kujenga timu kwa miaka 3 o f 4 United hawana upuuzi huo United sio Liverpool mkuu timu ikikosa kombe hata misimu 3 kocha haulizwi United wanahitaji wachezaji wakubwa ,timu ishinde Trophies then wafanye Business wapige pesa
United ni sawa na Madrid, Barca, PSG sio club ya kujenga timu ni club inayohitaji mafanikio kwa njia yoyote ile
 
Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
16,942
2,000
HII NDIYO MAANA HALISI YA KUFA KUFAANA.

Unaambiwa kufungiwa kwa Manchester City kutawapa faida Arsenal na Manchester United kucheza Uefa.

Arsenal yupo na fasi ya 5 na Man U yupo nafasi ya 6.

Arsenal watapata faida hata kama hawajashinda Europa kwa vile wapo nafasi ya 5 watasogezwa juu ili zitimie timu nne kama kawaida.

Ila Man U wao watategemea matokeo ya Arsenal washinde Europa Arsenal wakibeba kombe la Europa watakuwa wame fudhu kupitia Europa ndipo Man U watachukuliwa kuziba nafasi ya Man City ili zitimie timu 5.

Kama Arsenal wasipochukua kombe la Europa itakua faida kwa Arsenal tu na Man U itakula kwao.

Hapo nawaona siku hiyo wale mashabiki wote wa Man U waliopanga kuishangilia Chelsea wataamia kuishangilia Arsenal sasa...
 
Top Bottom