Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Game ya juzi first half Spurs alikuwa anatolewa but Pochettino alikuwa flexible akamuingiza "big man" Fernando Lllorente wakawa wanampigia mipira ya juu akawachanganya defence ya Ajax Spurs wakashinda (hii approach Mourinho aliitumia kwenye Uropa final)
Hii timu yetu ilibidi kwanza ipate kocha fundi wa mpira ambaye sio "Yes man" and then mambo mengine yafuate..silioni hili kwa OGS pia but ngoja tuone maybe he can prove me wrong
 
Umeyaorodhesha matatizo na ukapendekeza mabadiliko lakini hujataja mabadiliko unayoyahitaji ni yapi ?
HAKUNA kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Hilo ndilo linalowahusu Man United. Lakini, hilo sio tatizo kubwa linalowakabili, kwa hali ilivyo kwa sasa hawaonekani kama mambo yatatumia ndani ya miaka ya karibuni.
Shida haijulikani ni wachezaji au makocha? Hakuna mashaka wachezaji wataletwa kwenye dirisha lijalo la usajili wakati Ole Gunnar Solskjaer atakapohitaji kukijenga upya kikosi chake, lakini suala la wachezaji kuletwa limeshafanyika sana huko nyuma na mambo yamegoma kukaa sawa.
David Moyes, Louis van Gaal na Jose Mourinho wote walipewa pesa za kusajili, zaidi ya Pauni 600 milioni zimetumika tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson. Lakini, hakuna nafuu, mara ya nne katika miaka sita tangu Ferguson alipoondoka, Man United inamaliza ligi nje ya Top Four.
Hilo ndilo walilostahili. Kwenye mchezo wao dhidi ya Huddersfield hawakuonekana kabisa kuwa na nia ya kutaka kushinda mchezo huo ili walau kuendelea kwenye mambambo ya kuwamo kwenye Top Four.
Man United imeshindwa kuandikisha ushindi mbele ya timu ambayo imepoteza mechi zake 22 kati ya 24 zilizopita. Lakini, pengine wakati mchezo huo unafanyika kulikuwa na timu zinazofanana tu viwango.
Sawa Huddersfield wameshuka daraja, lakini kwa mwendo ambao Man United ilikuwa ikienda nao, ulikuwa unatishia kwelikweli. Kushinda mechi mbili kati ya 11 za karibuni, hicho si kiwango cha kuvunia kabisa kwa Man United.
Hali ni mbaya na haionekani itakwisha lini. Maisha yamegeuka kwa haraka sana. Siku zimekwenda kasi sana kwa kocha Ole. Mechi zake 11 za mwanzo, alishinda 10 na kutoka sare moja tu.
Kwa wakati huo, Arsenal, Chelsea na hata Tottenham wote walionekana wataachia tu zile nafasi zao wanazoshika kwenye msimamo wa ligi.
Ilifika wakati Man United hadi waliingia kwenye ile Top Four na kuonekana kama mambo yangemalizika hivyo. Kufumba na kufumbua, mechi 11 za karibuni, Ole ameshinda mara mbili tu, sare mbili na vingine vyote vichapo. Man United imefungwa na timu kama Wolves mara mbili. Imefungwa na Everton 4-0. Wamefungwa na Watford na West Ham.
Ni aibu.
Kitu kibaya, kwenye mechi hizo hakuna hata moja ambayo hawajaruhusu wavu wao kuguswa. Huo ni mwendo wa ovyo zaidi kuwahi kuutembea kwenye maisha yake ya kisoka tangu miaka ya sabini huko.
Kama utakuwa umeitazama Man United kwenye mchezo wao na Huddersfield basi bila shaka utakuwa na matatizo milioni moja yanayohitaji kupatiwa utatuzi kwenye kikosi hicho. Man United imemegukameguka.
Huwaoni kuwa na mpango wa kutafuta goli, kuwa na mpango wa kuzuia wasifungwe.
Alexis Sanchez amekosa maajabu. Paul Pogba amekuwa wa aina ileile licha ya kugongesha mwamba mara mbili. Marcus Rashford amepoteza shabaha yake ya goli, naye anahitaji nafasi nyingi kufunga mara moja.
Hayo ndio mengi yanayoigharimu timu hiyo. Imekosa huduma ya wale wafungaji hatari kama alivyokuwa Robin van Persie kwenye kikosi chao.
Kwenye ligi ya kisasa, unahitaji kuitumia vyema kila nafasi inayopata kwa sababu hutazamii kuona zikipatikana nyingi ndani ya mchezo mmoja. Hayo ndio maisha magumu yanayoikabili Man United kwa sasa. Yanahitajika mabadiliko makubwa.
 
Game ya juzi first half Spurs alikuwa anatolewa but Pochettino alikuwa flexible akamuingiza "big man" Fernando Lllorente wakawa wanampigia mipira ya juu akawachanganya defence ya Ajax Spurs wakashinda (hii approach Mourinho aliitumia kwenye Uropa final)
Ndio maana Jose juzi, akichambua kutolewa kwa Ajax alisema football game is a sport battle

Sometime you have to abondone your philosophy to win a game
 
One of low profile names signings? View attachment 1093212

Kwa mtizamo wangu huu usajili wa style hii nakubaliana nao 100%, sahv tunahitaji kusajili watu wenye njaa ya mafanikio na wenye umri mdogo ambao bado wana dreams na ambition za kufanya makubwa kwenye career zao,hyu dogo sijamfatilia sana ila kwa haraka haraka anaonekana ni fighter na kwa sahiv tunahitaji winger mpambanaji.

Sema kuna baadhi ya mashibiki huwa nashindwa kuwaelewa unakuta anaponda usajili wa low profile players akidai kwamba watakuja kuwa mizigo,hawatatufikisha popote na kwamba Glazers wanabana hela za kuspend, alafu tena tukisign wachezaji wenye majina makubwa wakifeli anarudi tena kuponda kwamba kwann wakina woodward wanapoteza hela kwa wachezaji wakubwa alafu wanakuja kuwa maflop kama kilichotokea kwa Sanchez,Falcao,Di maria,Bastian etc...yaani kwa ufupi mashabiki wa mpira sometimes hatuelewi tunataka nn na mambo yakifeli lazima tutafute mchawi!
 
Ujumbe wa Edo Kumwembe siku Ferguson anastaafu
20190510_192842.jpeg
 
Nadhani United ni club kubwa sana kwa OGS,

Lakini approach ya kusajili majina madogo inaweza msaidia kocha kukua na timu taratibu

Baada ya muda ataweza kuvaa viatu vya kuifundisha club ya United

Apewe muda
Mashabiki wa man u wanataka mafanikio ila kwa njia ya mkato sana sijajua kama mafanikio huja kwa kusajili majina makubwa peke yake na fantastic coach bila kujenga chemistry ya team?

Ilimchukua miaka miwili Callo Anceloti kuchukua champions league pale Madrid lakini iliwachukua miaka saba kutengeneza team ya kuchukua cahmpions league mfululizo Mara nne in five years

Ilimchukua misimu mitano man city kujenga team na kuanza kuchukua ubingwa wa epl tu lakini Leo mwaka wa Tisa hawajawahi hata kufika nusu fainali ya UEFA wala Europa.

Huyu Mauricio Pochetino huyu hajawahi hata kutwaa kombe la mbuzi katika career yake Tottenham amekaa msimu wa tano sasa achievement yake kubwa ni kushika nafasi ya pili kwenye EPL na kufika finali UEFA msimu huu.

Tusiwe na haraka kiasi hicho team iko katika wakati ambao mashabiki tunapaswa kuwa na subira sana ijengwe taratibu siyo kwa kufanya ukusanyaji wa players wasio na matumizi kama PSG.

Ole hata mwaka hajamaliza tunaanza kujudge uwezo wake katika kikosi ambacho manager yoyote angeweza kustruggle nacho ?
 
For now United is too big for OGS lets give him time,he has been in charge for half of the season.
Poch was the right candidate and available to rebuild this team he tick almost every box
Maybe Ed contacted him before appointing OLE.

1 year into a new 5 year contract
New stadium finally finished
Great squad of players
Team improving year on year

There’s no way he would leave all this for another English club .
 
Mashabiki wa man u wanataka mafanikio ila kwa njia ya mkato sana sijajua kama mafanikio huja kwa kusajili majina makubwa peke yake na fantastic coach bila kujenga chemistry ya team?

Ilimchukua miaka miwili Callo Anceloti kuchukua champions league pale Madrid lakini iliwachukua miaka saba kutengeneza team ya kuchukua cahmpions league mfululizo Mara nne in five years

Ilimchukua misimu mitano man city kujenga team na kuanza kuchukua ubingwa wa epl tu lakini Leo mwaka wa Tisa hawajawahi hata kufika nusu fainali ya UEFA wala Europa.

Huyu Mauricio Pochetino huyu hajawahi hata kutwaa kombe la mbuzi katika career yake Tottenham amekaa msimu wa tano sasa achievement yake kubwa ni kushika nafasi ya pili kwenye EPL na kufika finali UEFA msimu huu.

Tusiwe na haraka kiasi hicho team iko katika wakati ambao mashabiki tunapaswa kuwa na subira sana ijengwe taratibu siyo kwa kufanya ukusanyaji wa players wasio na matumizi kama PSG.

Ole hata mwaka hajamaliza tunaanza kujudge uwezo wake katika kikosi ambacho manager yoyote angeweza kustruggle nacho ?

Unapomlaumu Poch kaka miaka 5 bila ndoo ukumbuke it took Alex Ferguson 6 years to start winning something
 
Maybe Ed contacted him before appointing OLE.

1 year into a new 5 year contract
New stadium finally finished
Great squad of players
Team improving year on year

There’s no way he would leave all this for another English club .

Maybe unachosema nikweli lakin i don't think so,sidhani kama Woodward alimpa Poch hyo offer,natend kufikiria hivi kwasababu zifuatazo

1. UTD ni club kubwa sana klinganisha na Tottenham makocha wote bora duniani huitolea macho hyo nafasi maana ukiweza kutoboa UTD legacy utakayojijengea ni balaa,hvyo siamini kama Poch angeweza kukataa kama angepewa hyo offer,hata kwenye interview zake alikuwa anababaika sana akiulizwa hilo swala la kwenda UTD.

2.,Shida nyingine ni kwamba Tottenham hawawezi shindana kabsa na UTD financially hvyo hawezi pata financial backing pale TOT kama ambavyo angeweza ipata UTD, angalia mpka sahv Spurs wamenunua mchezaji gani wagharama sana?,Msimu huu walianza bila kusajili mtu yoyote wa maana na hata kihistoria ndani ya hii miaka ya karibuni ukiangalia utaelewa nachosema hyo kitu nauhakika inamkwaza sana Poch,ukiangalia interview yake juzi kati hapa alisema kama akifanikiwa kushinda CL msimu huu atasepa,Ofcoz hakusema wazi kabsa ila kila mtu alimuelewa!

3.Kwa position/situation tuliokuwa nayo kipindi kile kwa performance ya timu na support ya mashabiki ilikuwa ni almost impossible kumpa hicho kibarua mtu mwingine zaidi ya OLE,Hata humu kwenye hili jukwaa asilimia kubwa tulikuwa tunataka OLE apewe huo mkataba haraka iwezekanavyo,wengine walianza na kulalamika kabsa kwann mpka muda huo bado hajapewa mkataba.
 
mashabiki wa United hatuna uvumilivu hatujui kabisa kitu kinachoitwa transition, sijui ingekuaje timu hii ndo ingekuwa Arsenal au Liverpool.
 
New signing 6????

Mkuu umewahi kulitembelea soko la wachezaji la Siku hizi lakini?

Kamchezaji kama Di Ligte aliyekuwa mwisho kuchezea ligi ya Wachunga Farasi kule uholanzi unajuwa kasimama na £ ngapi?

Kwa Market ya sasa OGS kupewa £300m usidhani kama anaweza kupata hao wachezaji 6.

Mchezaji wa Kushindania Makombe kwasasa anaanza na £75m.

Au afanye kama Klopp kunuwa cheap option za kina Mane, Salah na Robertson then aboreshe.
Lakini hapo atahitaji misimu miwili au mitatu kuwaboresha jambo ambalo Man U hamuwezi kulivumilia.
Wengine ananunua kwa kubadilisha wachezaji. Pia fedha zingine atazipata kwa kuuza Amina Lingard, Martial, Pogba, Young, Alexis nk
 
Back
Top Bottom