Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ila siyo siri , mkikosa huu ushindi wengi wenu mtaugua.
Maana mmeshaanza tambo kabisa.
Hatuwezi kuugua. Huu ushindi mnauhitaji kwa hali na mali.

It's make or break (ila kwa point of view yenu nyie mlioko Nanjilinji mnadhani ndio mawazo ya OGS na wachezaji wake kuwa wapoteze mechi kwa kutaka).

Hata kama mkifungwa ki-sport kuna game ya Burnley na Leicester nazo ni ngumu kwa City. Tunagemea City apoteze points zaidi ya 4 mpaka end of the season.
 
Liver wenyewe tia maji tia maji, when it matter the most anatokea legend anateleza. Tunamsubiria mrithi wa slippy G mechi kadhaa zijazo.
 
Liver wenyewe tia maji tia maji, when it matter the most anatokea legend anateleza. Tunamsubiria mrithi wa slippy G mechi kadhaa zijazo.
Alishateleza Andy Robertson game ya Chelsea, fortunately for us we won. Unfortunately for you who are always saying "Liverpool mechi ijayo wanapigwa" tokea mmeanza hizi ramli sisi tunateleza tu.

Three to go.


Poetry In Motion. Tralalalalaaa
We are Liverpool. The best Football Team in the World. Yes We Are.
 
Mkuu ni kwamba hujanielewa. Pogba ni mchezaji mzuri lakin attitude mbovu. Similar to diego costa. Mchezaji mzuri yes lakin tabia mbovu.
Hawa wengine uingereza unawaponza.. na mm nilishangaa wanaongezwa mkataba kwa lipi hasa wanalojua. Toka msimu uliopita licha ya mashabiki kupiga kelele kuwa akina jones na smalling young hawafai... lakin upngoz umewapa mkataba.

Na hapa it is down to mtu mmoja mwenye kuleta madudu. Edwoodward. Huyu ndio cancer..
 
Unashindwa kutofautisha genuibe fans na plastic fans.

Despite Arsenal prfimance kuna watu bado ni arsenal kufa kupona, despite liverpool kukaa 20+ years with no title kuna watu bado ni liverpool, man city hana hii kitu.

Hivi wewe hujiulizi Puma kuwapa biggest deal a team that cant even fill their 30 thousand seats stadium badala ya Arsenal? Hapo lazima ujue kuwa both city na puma wapo desparate. Deals za man city zimejaa na utata na haswa Etihad deal. Hiz vitu zimevuja na infantino yumo nae. Huu ni mchezo wa city na psg. Both clubs haziwez kufanya usajili walioufanya kihalali
 
Ni ngumu timu kupoteza mashabiki, lakini inawezekana ...... Wapo mashabiki ambao wanahiari ya kuhama, lakini si wengi sana, ila wapo

Lakini kwa 100% timu ikiwa haifanyi vizuri uwanjani kwa kipindi kirefu, ni ngumu KUVUTIA MASHABIKI WAPYA, na in the long term run kama United akiendelea kumbwela hivi atabaki na mashabiki wale wale aliokuwa nao bila kuongeza na pengine atapoteza wengine kwa timu nyingine ikiwemo Man City

Unataka Arsenal apewe deal kubwa na Puma au Whoever ili akawatangaze huko Europa? City anapewa deal kubwa kama hiyo kwa kuwa Puma anakuwa ana uhakika wa bidhaa yake kutangazwa kwenye biggest stage possible, ambapo kwa muktadha huu ni UCL

Wewe unadhani kwanini adidas ameona kuna haja ya kuweka kipengele cha kuinyima United milioni £75 kwenye mkataba endapo kwa miaka 2 mfulilizo timu haitafuzu kucheza UCL, sababu ni moja tu UCL ni special tournament kwa biashara yoyote kwenye suala la marketing

So Puma wameona fursa kwa City. We unadhani kwanini Everton hawajapewa dili kubwa, au Cardiff .... Sababu ni moja tu, matokeo uwanjani

Man United yenyewe wakati inaanzishwa ilikuwa sawa (possibly imepitwa) na Leeds United, kipindi hicho ni wapinzani haswa. Lakini United kwa sasa wana fan base possibly mara 100 ya Leeds, kwanini ......? Simple, kwa sababu walipata mafanikio uwanjani kwa kipindi kirefu.
 
Sijakataa kuwa mafanikio yanafaida ya kukuongezea mashabiki, lakini CITY inapoteza hadi mashabiki wake pamoja na mafanikio yote. Kikubwa nlichoona ni kuwa city inapoteza fans, na all these big spendings na izo deals ni to gain attention. Pale uwanjani wanaoenda kukaa jukwaa la city home fans wanaenda manutd fans na wengine kutizama mpira tu. Ata kuna siku city alicheza mtangazaji akauliza mashabiki watatu waliova jez za citeh kila mmoja kumbe ni shabiki wa timu tofauti. Pamoja na mafanikio yao, hata kwenye academy ya citeh kuna players wanataka kuchezea Man utd wakimaliza hapo.

City haijui kujibrand kibusiness, city is used to clean the image of the oil nations pamoja na psg yake. Miaka saba sasa inakwenda bila kuwa na mafanikio uwanjana kwa Man utd, still Utd inapata more deals than City. Hujiulizi why?

Narudia, City wapo desperate na Puma wapo ivo ivo wamekutana, Na usishangae kuwa mwarabu ameongeza hela kwenye hilo deal ili tu ahalalishe big spendings zake.

Kuhusu deal la Man utd na Adidas, wameambiwa washiriki tu UEFA champions league, so that means ata akitoka group stage deal iko pale pale hata kwa miaka minne. Hii should be enough to tell you that jamaa wanataka visibility na sio mafanikio yako tu.

Just because you are winning titles it gives you chance to negotiate. Ofcourse sponsoring the title winner has to be different from runners up.

Mpaka leo woodward anasecure better deals than Man city na tunashindana kwa nafasi ya nne tangu aondoke fergie.

Mafanikio yanakuletea fans lakini city haijapata bahati hio bado
 
 
 

Sorry for jumping in your arguments, kuna kitu nikieleze pia kuhusu fanbase.

Man Utd amekuwa kwenye kilele cha mafanikio for almost 2.5 decades (almost 25 years), fanbase aliyoitengeneza kwa kipindi hicho huwezi kuifuta ndani ya miaka 10.

City ndo kwanza wameanza kupata washabiki, leo hii mtaani (huku Tanzania) unaweza atleast kuona watu kadhaa wamevaa jezi ya City. Ila unaweza kumaliza wiki hujaiona ya Man Utd.

Na new age wanaoanza kushabikia mpira na kuchagua timu (10 - 20 years of age) wakipewa 2 options kati ya Utd na City under no influence, 80% wataichagua City.

Na hiyo fanbase miaka kadhaa ijayo na wao watakuwa wengi na imagine some thing like other 10 years hawa watakuwa ni purchasers, City will be having a good fanbase by then.

Na kama Guardiola anaendelea kuwepo na hao scouts waliopo, City inatengeneza identity moja ya hatari sana na ya kuvutia.

Imagine, City anacheza mchezo ambao neutrals au hata fans wa timu zingine tunainjoi kuangalia, fanbase inaanza namna hiyo.

Nani anaikumbuka Arsenal ya 2003/04, 2004/05 hata ile ya 2005/06 iliyocheza final UEFA? Timu ilikuwa inavutia kiasi kwamba hata wapinzani tinainjoi kuangalia games zao.

Kuhusu endorsement: viewerships zina-determine sana ukubwa wa deal, na City kwa EPL ni one of the most watched teams, leo hii Man Utd wanakimbia kuangalia game zao.

Miaka michache nyuma ilikuwa Man Utd akicheza hata na timu gani, mabanda ya mpira yalikuwa lazima yaoneshe game ya Utd na wanajaza, leo hii kaangalie uone wanaingia wangapi.
 
Hata lukaku unamlaumu basi huyo rashford mechi kama tano sahv anaboronga tu mna muoverrate huyo angekuwa timu nyengine hata haanzi
Ukiondoa mashuti ya rashford ambayo waga anachomeka mzizi kwenye kiatu cha mguu wa kulia hana tofauti na Ayoze Perez wa Newcastle United.
 
Wameshinda kombe juzi juzi, asante kwa kuongeza ushahidi kuwa mafanikio ndio yanaleta mashabiki
 
Mkuu umeongea umeongea kitu cha msingi hususani kwenye suala PERFOMANCE YA MUDA MREFU INAVYOWEZA KUONGEZA AMA KUPUNGUZA WASHABIKI

Kuna watu wanakunja shingo kwamba Man Utd haiwezi kupoteza washabiki sababu ya brand...... Mfano mtoto/kijana yupo nanjilinji huko, anaanza kufuatilia mpira wa Ulaya sasa hivi, aipende United sababu ya brand ili iweje

Hawafahamu kipindi cha mwisho mwisho mwa zama za Jose pale OT viti vikianza kuwa kwenye wazi kwenye baadhi ya mechi, wakati United inasifika kujaza watu 75,000 iwe Man anacheza na Barnsley au Liverpool ...... Sasa hii ya uwanja kupwaya wanadhani imesababishwa na nini? POOR PERFOMANCE

Hawa wanaosema brand haitashuka regardless ya performance na matokeo uwanjani hawajui hata baadhi ya mashabiki humu waliacha kuangalia game za United kwenye TV kipindi cha mwishoni zama za Jose?

Hawa watu hawajui kuwa kesho kuna baadhi ya watu humu wataacha kucheki game ya United kwa kuwa wanahisi United hawata perform. Ni vipi, performance ikiwa ni mbovu kwa muda mrefu, say miaka 5 au 10 ijayo, je United hatapoteza mashabiki?

Mwisho labda niseme, kiujumla kwa sasa bado mtaani jezi za United ni nyingi kuliko za City, ila zimepungua na za City zimeanza kuonekana. Je kwa muda mrefu hali hii ikiendekea hatuoni kwamba United power itafifia?



 
Cristiano Ronaldo, Park JiSung, Rio, Vidic, Anderson, Nani walikuja United hawana majina.

United wakawapa majina wakauza jezi na kuvunja rekodi mbalimbali.

Jezi alizozouza Van Persie akiwa United ni zaidi ya mara mbili ya jezi alizouza akiwa Arsenal.

Tatizo sio jina la mchezaji, ila akifanya vizuri kwenye timu kubwa kama United lazima awe gumzo duniani.

Martial alivyokuwa Monaco alikuwa useless kwenye mapato ya timu, alivyokuja United amebaki historia.

Rashford angecheza Southampton angekuwa wa kawaida sana tu. Vardy angecheza United na speed yake ya kutupia angekuwa famous kuliko Lukaku.

Hivi unajua % ngapi ya mashabiki wa mpira wa miguu duniani wanashabikia United?
 
Hatutafika huko.

Glazer na Ed watakuwa wameshaondoka.
 
Media ya uingereza inawapigia debe sana wachezaji wake inawapa sifa za uwezo ambao hawana baada ya kina lingard na rashford sasa angalia hudson odoi sahv nae ndo walewale wakina rashford
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…