BLOOD DIAMOND
Member
- Mar 24, 2017
- 92
- 122
Hapo kwa linderlof mzee umepepesa,,yule Iceman ndio best defender Bora ktk ligiWakuu hongereni kwa kucheza vizuri japo tulifungwa
Poleni kwa kusumbuliwa na vidudu Mtu wa kutoka timu nyingine wasiojua mpira zaidi ya matusi (sizungumzii wastaarabu kama Don Clerenzo et al. )
Observation yangu, kiufupi over all tulicheza vizuri, hususani baada ya kufungwa goli
Bado kuna shida kwenye creativity, tunamtegemea sana Pogba ambaye kuna siku huwa hayupo kwenye form (kwa jana amecheza wastani, sio vibaya).
Ole kuna mambo arekebishe
Ana imani na baadhi ya wachezaji hususani wa kiingereza wasio na kiwango toshelezi. Mfano alihitaji sana goli, lakini anamtoa Lukaku (ambaye ni tishio kwenye mipira yote ikiwemo ya juu) halafu anamuacha Rashford (sisemi Rashford ni mbovu, lakini si mchezaji wa kumuweka benchi Lukaku)
Ole alinishangaza pia kumtoa Dalot na kumuacha Young. Young ni captain wetu, anacheza kwa moyo wote kwa ajili ya timu, anajua thamani ya badge ya United lakini uzalendo kwa timu pekee hautoshi, tunahitaji uwezo.
Kumtoa Dalot ambaye ni mpiga krosi mzuri halafu anamuacha Young siamini kama ni uamuzi mzuri. Sub ya Pereira alipaswa kumtoa Young.
Smalling so far he is our best central defender, hata nikiambiwa niwapange kwa umuhimu, ataanza yeye atafuta Lindelof. Najua hapa tunatofautiana.
OGS ameshapata midfielder yake. Pogba akiwa na Fred na Tominay unaona timu inakuwa na haraka hata katika kupanga mashambulizi, kabla ya kufanya usajili OGS ajikite kwenye hii midfielder 3.
Messi alicheza? Sikumuona kabisa, labda kwa sababu ya kimo chake, hakuwa man-marked lakini alipotezwa kabisa. Ukiniambia nikumbushe tukio la Messi jana ni pale alipotoka damu, na virafu uchwara alivyokuwa anacheza.
Kichekesho, leo sisikii Messi akitajwa tajwa
Bosquet alicheza virafu vingi sana, ishara kwamba mechi ulikuwa ngumu kwao.
Nafasi ya kuwatoa Barca bado ipo
Man Utd ni wafalme kutoka nyuma na kushinda. Hili halijaanza msimu huu (waulize Juventus 1998/1999). Sitakumbusha kilichowakuta Juventus na PSG msimu huu.
Lakini bado nakubali Barca ni moja kati ya timu (ngazi ya club) bora duniani, ndio maana inakutana na bora wenzake kama United. Kuna timu humu hazijawahi kukutana na Barca tangu 2006, siku chache baada ya Kikwete kuapishwa kuwa rais wetu kwa mara ya kwanza
Luke Shaw kutokuwepo mechi ya Camp Nou ni kikwazo. Lakini wapo watu watakaofanya kazi ambayo amekuwa akiifanya kwa siku zote.
We are Manchester United
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
