Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Wakuu hongereni kwa kucheza vizuri japo tulifungwa

Poleni kwa kusumbuliwa na vidudu Mtu wa kutoka timu nyingine wasiojua mpira zaidi ya matusi (sizungumzii wastaarabu kama Don Clerenzo et al. )

Observation yangu, kiufupi over all tulicheza vizuri, hususani baada ya kufungwa goli

Bado kuna shida kwenye creativity, tunamtegemea sana Pogba ambaye kuna siku huwa hayupo kwenye form (kwa jana amecheza wastani, sio vibaya).

Ole kuna mambo arekebishe

Ana imani na baadhi ya wachezaji hususani wa kiingereza wasio na kiwango toshelezi. Mfano alihitaji sana goli, lakini anamtoa Lukaku (ambaye ni tishio kwenye mipira yote ikiwemo ya juu) halafu anamuacha Rashford (sisemi Rashford ni mbovu, lakini si mchezaji wa kumuweka benchi Lukaku)

Ole alinishangaza pia kumtoa Dalot na kumuacha Young. Young ni captain wetu, anacheza kwa moyo wote kwa ajili ya timu, anajua thamani ya badge ya United lakini uzalendo kwa timu pekee hautoshi, tunahitaji uwezo.

Kumtoa Dalot ambaye ni mpiga krosi mzuri halafu anamuacha Young siamini kama ni uamuzi mzuri. Sub ya Pereira alipaswa kumtoa Young.

Smalling so far he is our best central defender, hata nikiambiwa niwapange kwa umuhimu, ataanza yeye atafuta Lindelof. Najua hapa tunatofautiana.

OGS ameshapata midfielder yake. Pogba akiwa na Fred na Tominay unaona timu inakuwa na haraka hata katika kupanga mashambulizi, kabla ya kufanya usajili OGS ajikite kwenye hii midfielder 3.

Messi alicheza? Sikumuona kabisa, labda kwa sababu ya kimo chake, hakuwa man-marked lakini alipotezwa kabisa. Ukiniambia nikumbushe tukio la Messi jana ni pale alipotoka damu, na virafu uchwara alivyokuwa anacheza.

Kichekesho, leo sisikii Messi akitajwa tajwa

Bosquet alicheza virafu vingi sana, ishara kwamba mechi ulikuwa ngumu kwao.

Nafasi ya kuwatoa Barca bado ipo

Man Utd ni wafalme kutoka nyuma na kushinda. Hili halijaanza msimu huu (waulize Juventus 1998/1999). Sitakumbusha kilichowakuta Juventus na PSG msimu huu.

Lakini bado nakubali Barca ni moja kati ya timu (ngazi ya club) bora duniani, ndio maana inakutana na bora wenzake kama United. Kuna timu humu hazijawahi kukutana na Barca tangu 2006, siku chache baada ya Kikwete kuapishwa kuwa rais wetu kwa mara ya kwanza

Luke Shaw kutokuwepo mechi ya Camp Nou ni kikwazo. Lakini wapo watu watakaofanya kazi ambayo amekuwa akiifanya kwa siku zote.

We are Manchester United

Sent using Jamii Forums mobile app
 
atakapoondoka marcos rojo hii namba 16 ni bora apewe scott mctominay, sielewi kwa nini tunataka kuingia kwenye mtego wa media za kiingereza za kutaka kumsajili declan rice.
hivi rakitic pamoja na arthur melo walikuwepo uwanjani?​
kama yupo mdau anayeamini siku moja rashford atakuwa mchezaji bora basi aendelee kuwa na imani hiyo mpaka kufa kwake.
man utd 0 barcelona 1
View attachment 1068168
Nizungumzie hapo kwa Rashford, huyu dogo si haba kipaji cha mpira anacho hasa ukilinganisha na wachezaji wa kiingereza.
Shida kubwa aliyonayo na inaendeleza kumdidimiza ni kujiona kwamba ni lazima afunge ndiyo aonekane.
Moja ya makocha ninawaheshimu ni Pep, Sterling akiwa Liverpool alikuwa mzuri lakini alikuwa anapoteza sana mipira kwa kulazimisha kufunga, alivyoenda kwa Pep kabadilika, anajua nitoe pasi muda gani, nikae wapi kusubiri pasi au nipige ndani muda gani.
Aguero kuna kipindi alikuwa naye ni hero ball, akawa analamba benchi mara kadhaa mpaka somo la ushirikiano na timing likamwingia.
Rashford anahitaji kocha kama Pep, ambaye anakufundisha kwa vitendo, means ukizingua unakaa benchi.
Imagine mshambuliaji unaweza kufunga goli bado Pep anakwambia pale ulitakiwa utoe pasi afunge fulani.
Team work kwenye front line ndiyo nguzo kuu ya ushindi na inanyanyua viwango vya wachezaji. Leo Liverpool tuna shida ya Salah anataka kufunga, Mane anataka kufunga, Firmino pekee ndo hana hizo.
 
muda utaongea
1068276
 
Nizungumzie hapo kwa Rashford, huyu dogo si baba kipaji cha mpira anacho hasa ukilinganisha na wachezaji wa kiingereza.

Shida kubwa aliyonayo na inaendeleza kumdidimiza ni kujiona kwamba ni lazima afunge ndiyo aonekane.

Moja ya makocha ninawaheshimu ni Pep, Sterling akiwa Liverpool alikuwa mzuri lakini alikuwa anapoteza sana mipira kwa kulazimisha kufunga, alivyoenda kwa Pep kabadilika, anajua nitoe pasi muda gani, nikae wapi kusubiri pasi au nipige ndani muda gani.

Aguero kuna kipindi alikuwa naye ni hero ball, akawa analamba benchi mara kadhaa mpaka somo la ushirikiano na timing likamwingia.

Rashford anahutaji kocha kama Pep, ambaye anakufundisha kwa vitendo, means ukizingua unakaa benchi.

Imagine mshambuliaji unaweza kufunga goli bado Pep anakwambia pale ulitakiwa utoe pasi afunge fulani.

Team work kwenye front line ndiyo nguzo kuu ya ushindi na inanyanyua viwango vya wachezaji. Leo Liverpool tuna shida ya Salah anataka kufunga, Mane anataka kufunga, Firmino pekee ndo hana hizo.
Rashford mchoyo sana namshangaa sana Firmino hana mitamaa ya kufosi kushinda hovyo
Man wakipigwa hua wanageuka wachambuzi.
Uzi huu sio tukifungwa tu uchambuzi upo kila siku kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu klabu yetu
 
We kuna vitu hukuviona kulikua kuna mikakati sana pâle kati yakuwafanya barcelona kutopata mianya ya kupenyeza mipira yahatari, unafikiri barca kufunga goli moja nihiari yao !! Forwad line yako ndo ilikua butu ila midfild players wamefanya kazi yao kiasi chake

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo ndio tujipongeze kwa kufungwa/kujifunga moja tu, wakati Barca saizi yetu kabisa!! Ilitakiwa tuwatandike za kutosha!!
Huo ubutu wa forward line ni makosa ya nani kama sio kocha na benchi lake!!?

Mechi za hivi karibuni tumekuwa na mfumo usiobadilika, waliishatusoma ndio maana kufungwa inakuwa kawaida licha ya uwezo wa hali ya juu anaoonesha goal kipa
 
kama tulistahili kupigwa saba na badala yake tukafungwa moja unaanza kucritisice sasa huoni kama timu ndo ilifanya vizuri??
Kwa hiyo goli moja nilakusifia timu!!!, sema tu na Barca nao hawakuwa kwenye form nzuri. Hebu karudie kuona mechi ya Juve ya jana, halafu fikiria kama ndio ingekuwa tunakutana nao kwa tulivyocheza jana tungesalimika? Si ingekuwa aibu ya mwaka?

Check replay. Angalia hata mabeki tu walivyokuwa wanapoteza poteza mipira sehemu za hatari kabisa,
 
Kwa hiyo ndio tujipongeze kwa kufungwa/kujifunga moja tu, wakati Barca saizi yetu kabisa!! Ilitakiwa tuwatandike za kutosha!!
Huo ubutu wa forward line ni makosa ya nani kama sio kocha na benchi lake!!?

Mechi za hivi karibuni tumekuwa na mfumo usiobadilika, waliishatusoma ndio maana kufungwa inakuwa kawaida licha ya uwezo wa hali ya juu anaoonesha goal kipa
Sawa camp nou ndyo mtajiona kuwa kumbe hamna tofaut na Girona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom