Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ni wapubavu.. nimeona jamaa wanakasiriks hadi wanashikana mashati kwenye vibanda vya kucheki Mpira..
Ukitaka kumalizia mkazo wa ugumu wa maisha yako binafsi kwenye ushabiki wa mpira ndio utajikuta unatokwa na matusi bila sababu.

Tumekuwa na akina King Ngwaba humu kila siku tunabishana na sijawahi ona wakitokwa na matusi.

😂😂ajabu leo sijui hivi vitoto vimetokea wapi vinachafua thread.
 
tutaongea lugha moja once OGS akipata mahitaji yake

tumecheza vizuri somehow
Kwa upande wangu naona tatizo lilikuwa kule mbele.
Ila kwenye kiungo wamepiga kazi, supply ya mpira kwa messi ilipungua .mpaka akawa anaingia deeper.

Ila RB, ni tatizo linaitaji ufumbuzi wa haraka.
Too bad, Luke hatokuepo Camp Nou


Sent using simu mbovu
 
Leo kuanzia kocha mpaka wachezaji walipanic.
Kocha alishindwa kupanga kikosi cha kazi na bado ankfanya sub za hovyo.
Wachezaji ndio ilikuwa full kupoteana pale kati, yani hawaonani, pasi hazifiki.

Kufupi tulistahili kupigwa hata saba.
Kikosi cha ovyo? wewe ulitaka acheze nani? na unajua majeruhi ya timu kuelekea game ya jana mkuu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi humu wanaongea tu kiushabiki...lakini jana generally performance ya timu ilikua vizr na timu iliweza kupambana na barca vizr...bado hatuna mlima mkubwa kama gemu ya psg .pia hii timu toka aje ole inafanya vzr zaid away kuliko nyumban.. tumeshinda emirates..turin...paris...darajani..
 
Kwanza nimpongeze Ole Gunnar Solskjaer kwa timu selection na mbinu...

Hasa namna mfumo alioutumia wa 4-4-2 lkn wenye mbinu nyingi mfano mtazame alimchezesha Diogo Dalot kama winga upande wa kushoto huku shaw akiwa full back wake ambaye hakuruhusiwa kupanda mbele kushambulia na ndo mana tumeona mpk mipira ya kurushwa upande wa kushoto alikuwa akiirusha Dalot mwenyew na si shaw.

Kwenye midfield Fred alikua katulia sana sambamba na Pogba na McTominay ambae alikuwa akicheza kulia lkn muda mwingi akiongezeka katikati ili kuwasaidia Pogba na Fred kukaba huku upande wa kulia Young akipewa kibali cha kushambulia zaid kwenye upande wake wa kulia japo alikua mbovu sana.

Fred na McTominay walikua bora sana huku Pogba akiwa na mchezo wa kawaida na hakuwa na impact sana.


Kwenye ushambuliaji Lukaku alikua yuko vizur kiasi chake leo na tumeona hata kwa namna alivyokuwa aki- hold mipira na kukontroo leo. Ila Rashfoard alikua hovyo kabisa hakuna cha maana alichofanya na alikosa sana utulivu wa kufanya maamuzi.

Sub kidogo OGS aliniuzi kumtoa Lukaku mwanzo badala ya Young alaf Dalot angeenda kucheza kama right back alaf angeingia Martial kwenda kucheza left wing. Na baadae kumtoa Rashfoad kuingia Lingard. Au angetoka Dalot akaingia Martial huku lukaku akibaki uwanjani.

Baadae tumepiga sana cross alf mtaalamu wa mambo hayo katolewa nje sasa tunafanyaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
atakapoondoka marcos rojo hii namba 16 ni bora apewe scott mctominay, sielewi kwa nini tunataka kuingia kwenye mtego wa media za kiingereza za kutaka kumsajili declan rice.
hivi rakitic pamoja na arthur melo walikuwepo uwanjani?​
kama yupo mdau anayeamini siku moja rashford atakuwa mchezaji bora basi aendelee kuwa na imani hiyo mpaka kufa kwake.
man utd 0 barcelona 1
View attachment 1068168
Hv huyu dogo raia wa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tonight, Ashley Young lost possession a total of 32 times and attempted 11 crosses with 0 meeting their target. No player on the pitch lost possession more or had a worse crossing rate than him.
Huyu jamaa huwa hajifunzi sijui au ndo kuishiwa maana anapenda kupiga long ball ambazo most of the time hazifiki sehemu husika lakini haachi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
atakapoondoka marcos rojo hii namba 16 ni bora apewe scott mctominay, sielewi kwa nini tunataka kuingia kwenye mtego wa media za kiingereza za kutaka kumsajili declan rice.
hivi rakitic pamoja na arthur melo walikuwepo uwanjani?​
kama yupo mdau anayeamini siku moja rashford atakuwa mchezaji bora basi aendelee kuwa na imani hiyo mpaka kufa kwake.
man utd 0 barcelona 1
View attachment 1068168
Tominay anapaswa kuwa regular stater

Rashford anakuzwa kuliko uwezo wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom