Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kama ungekuwa makini kusoma vizuri post zangu ungeelewa nimeongelea Draw za Barca na Mancity! na nimeongea hvyo kutokana na historia inavyosema sasa sielewi point yako hapo haswa ni ipi!
Nimesima ndo nikaelewa kuwa draw za barca na mancity wanapewa vibonde. Lini mancity kwenye ¼ final kapewa kibonde. Nulitaka kujua tu team gani hawa jamaa wamepewa vibonde? Post yako ni nzuri ila inalaumu maamuzi sahihi na kulalamika kuwa wanapewa vibonde. Ila ungejibu tu hao vibonde ni kina nani? na wakali ni kina nani? Ili tuweze kuchambua hapa.
 
Man Utd inatakiwa itoe kitita kinono kwa kocha kusajili wachezaji majembe wa kuziba nafasi muhimu.

Timu ina mapungufu sana. Ukiangalia fixture ya Man City ndo utajua umuhimu wa kuwa na kikosi kipana.

Angalia;

April 9/10 - Man City vs Tottenham (A) UCL
April 14 - Man City vs Crystal Palace
April 16/17 - Man City vs Totenham (H) UCL
April 20 - Man City vs Tottenham (H)
April 24 - Man City vs Man Utd (A)

Kama una kikosi legelege lazima ule za uso zote. Mechi zote muhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro mawazo mazuri.. Pia kwa taarifa zilizopo ni kwamba kuna percent kubwa dembele hatocheza..ila kwa upande wetu kikosi tutakacho kipanga ni sahihi kupambana na barca??.. Sioni sehemu ya matic kucheza ningependa
Herrera+perreira+fred/pogba yani tujiadhari kwa chochote.. Ila pia ole naamini atapanga Herrera+matic+pogba ambako sio sahihi kabisa..tukijitaidi kumkaba messi ambaye siku izi namuona kama ndo play maker wao mkubwa naamini tutaweza..
Nmeona nae messi anamsifia scott mctominay..ila nngependa tuwe na pure defensive mid wawili na mmoja acheze kma central at the same time.. Pia kma ni pogba acheze kma attacking and also akae kma CMD pia.. Tukijitaidi kuperform vizuri kati naamini tunawaweza kabisa
We didn’t want the ball because when Barcelona press and win the ball back, we lose our position – I never want to lose position on the pitch so I didn’t want us to have the ball, we gave it away, I told my players that we could let the ball help us win and that we had to be compact, closing spaces.” (jose mourinho).

maneno haya aliyazungumza jose mourinho baada ya kumalizika kwa mechi ya pili ya nusu final kati ya inter milan na barcelona mwaka 2010 pale nou camp.
  • tunacheza na timu ambayo ni bora linapokuja suala la umiliki wa mpira kuliko juventus na PSG
  • tunacheza na timu ambayo ni bora linapokuja suala la pressing (tension unayompa mpinzani wako pindi unapopoteza mpira) kuliko liverpool na manchester city.
  • tunacheza na timu ambayo ni mabingwa wa kuwapa timu pinzani pressure hali inayopelekea wapinzani kupoteza muelekeo wanapokuwa na mpira na wasijue cha kufanya.
wakuu tunatokaje hapa?​
kuna uwezekano na sisi tutamuiga kocha wetu wa zamani na mbinu zake za kuwaruhusu barcelona wawe na mpira kila wakati huku tukiwazuia wasifike kwenye eneo letu la hatari?

kufanya hivyo je tuna ukuta kama wa inter milan ya mwaka 2010?

upande wa kushoto wa barcelona ndio chachu yao kubwa ya mafanikio kwa sababu ya ushirikiano wa jordi alba na lionel messi, ukija kwetu sisi upande wetu wa kulia hatupo vizuri hususani kwenye kushambulia na hata kulinda kwa nidhamu, hivyo basi adui yoyote tutakayekutana naye atautumia udhaifu huu tulionao kabla hata ya mechi kuanza, tunajiandaaje kwa ajili ya kuwazuia wendawazimu watatu (alba + messi + dembele/ coutinho) na wakati huo huo tunawapa pressure upande wa kushoto ili alba apunguze kiherehere cha kushambulia mara kwa mara?

ernesto valverde naye pia ni mwendawazimu linapokuja suala la kujilinda na kama kilichotukuta mechi ya PSG walipomzuia paul pogba upande wa kushoto pia na barcelona wanao uwezo huo wa kumzuia labile, je tuna plan nyengine kama barcelona na wao wataamua kuja na style ya man marking kwa paul pogba, tukumbuke psg walipomzuia pogba tulipiga shuti moja kwa dakika 90.
mwezi huu mmoja uliobaki kama ningelikuwa nipo karibu na OGS ningelimshauri amuondoe nemanja matic na nafasi yake ichukuliwe na herrera huku nafsi ya pogba acheze fred kama ilivyokuwa mechi ya pili ya PSG.
HERRERA + MATIC + FRED​

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesima ndo nikaelewa kuwa draw za barca na mancity wanapewa vibonde. Lini mancity kwenye ¼ final kapewa kibonde. Nulitaka kujua tu team gani hawa jamaa wamepewa vibonde? Post yako ni nzuri ila inalaumu maamuzi sahihi na kulalamika kuwa wanapewa vibonde. Ila ungejibu tu hao vibonde ni kina nani? na wakali ni kina nani? Ili tuweze kuchambua hapa.

Shida ndo hyo unakosa umakini mi nimeongelea Draw sijasema hatua gani kuna round of 16 nayo inafanyika draw labda kama ulikuwa hujui,2015-16 City alipangiwa Dynamo Kiyv,2016-17 City alipangiwa Monaco,2017-18 City alipangiwa Basel,2018-2019 City alipangiwa Schalke 04 Sasa mpka hapo jiongeze we mwenyewe ukishindwa basi!
 
Ila sisi man u kuna matatizo tunatakiwa kuya solve.
Tukikutana na decent team inayopress, mfano arsenal jana.
Pale kwenye midfield huwa hapaeleweki(hata wawepo PMH), pasi zinapotea sana.
Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri hata leiceter city walitupa shida kwenye midfield.

sina uelewa mkubwa sana wa masuala ya mpira hususani kwenye tactics kama wengineo lakini miaka yangu yote tokea niifahamu manchester united nikiri ya kwamba manchester united hatujawahi kuwa bora kwenye kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa sana kama timu nyengine mfano zile zinazotoka Hispania, Germany (bayern munich).

kama nitakuwa nipo sahihi manchester united ndio timu kubwa pekee ambayo bado imeshikilia falsafa za kiingereza huku timu nyengine mfano liverpool na man city wameshaachana kitambo na mpira wa kiingereza wa kuziba nafasi nyeti kwenye maeneo ya hatari (Space Oriented Zonal Marking). Ni mfumo ambao nimeushuhudia kwa miaka yangu yote ya kuishabikia manchester united tokea mwaka 2001 ukitupa faida kubwa sana hususani tunapokutana na timu zenye uwezo mdogo sana wa kumiliki mpira kama zilivyo timu za uingereza lakini tunapokutana na timu zinazo dominate possession na counter pressing tunapata tabu sana na kwa ushahidi wa hilo jni pale tunapokutana na timu za spain na hata timu ya taifa ya uingereza bado ni waumini wa style hii ya kiuchezaji.

Ili uweze kudominate possession mara kwa mara unapaswa kwanza umdhibiti adui kwenye eneo lake la kujidai kitu ambacho manchester united hatufanyi mara kwa mara labda tuwe kwenye situation ya kutafuta magoli kama ilivyokuwa kwenye mechi yetu ya southampton au kuna mechi fulani mwaka 2008 tulikwenda half time tukiwa nyuma kwa magoli mawili dhidi ya spurs ya darren bent, lennon, pavlyuchenko n.k, ukija upande wa wapinzani wetu wakubwa kama liverpool na manchester city wao wanaanzia kukaba juu ndio maana ukiangalia mechi zao unakuta eneo la kati kati wapo wengi hivyo basi inakuwa ni vigumu kwa timu pinzani kufika maeneno yao ya hatari na hata wanapopoteza mpira wanarudi kwenye maeneo yao kwa haraka sana, ndio maana mechi ya guardiola na klopp inakuwa ni ngumu sana kwa pande zote mbili.

kama hatuwezi kuachana na utamaduni wetu wa soka la kuziba maeneo yetu ya kujidai basi atleast wachezaji wetu wanapaswa wabadilike kifikra na kiuchezaji ndipo baadae tuelezekeze shutuma kwa kocha na benchi lake la ufundi, msingi mkuu wa kuhakikisha timu inakuwa na umiliki mzuri wa mpira unapaswa uanzie eneo la ulinzi ndio maana guardiola alipotaka kuingiza falsafa yake ndani ya manchester city alianza kurekebisha eneo la ulinzi hivyo basi na sisi tunapaswa kuliangalia kwa jicho la tatu eneo letu la ulinzi kwa kuanzia golikipa.

Tuna golikipa mzuri sana linapokuja suala la kuokoa michomo ya magoli lakini ukigeuza sarafu utagundua ya kwamba kwa timu kubwa za uingereza (man city, liverpool, chelsea) sisi ndio tuna golikipa muoga wa kucheza ukilinganisha na hao niliowataja. mipira mingi anayoianzisha david de gea ni ile ambayo yupo kwenye presha ndogo sana, pengine safu yetu ya ulinzi ndiyo inamfanya david awe mzito wa kuanzisha mipira mara kwa mara bila ya kuwa na khofu yoyote. ukiwaangalia makipa kama ederson, allison, ter stegen, buffon, arrizabalaga, manuel neur wote hawa wanazidiwa na david degea kwenye saving lakini wanamzidi kwenye kucheza.

Josep guadiola hakumuondoa joe hart kwa sababu ni mbovu bali alimuondoa kwa sababu hii ya kutokuwa na uwezo wa kucheza hivyo basi david degea anapaswa aende na wakati kama wenzake. ukiangalia ukuta wa juventus nyakati zile ulikuwa unaundwa na walinzi wasiokuwa na degree yoyote ya skills mfano chiellini, barzagli, bonucci, lichsteiner lakini cha ajabu unamkuta buffon anaanzisha mipira hata kama adui yupo karibu.

smalling, young, jones, darmian:​
utawezaje kumiliki mpira kwa kiwango cha 60 - 70% kila mechi ikiwa mchezaji wako wa kikosi cha kwanza ni ashley young ambaye kila mechi anayocheza lazima apoteze mipira kipumbavu zaidi ya mara 5 kwa kupiga long pass zisizo na uhakika na mara tano akiwa out of possession ya kuanziwa mipira kama wanavyofanya walinzi wengine mfano wa jordi alba, walker, robertson, pique n.k.

ndio maana nawapenda sana manchester city na sera zao za kuendesha timu kwa sababu kocha mpya anapokuja anapewa uhuru wa kufanya anachokihitaji tofauti na sisi, timu yetu imejaza wachezaji wazito wanaoshindwa kufanya maamuzi ya haraka hata kama wapo under pressure, ndio maana tunapokutana na timu bora mfano wa juventus, barcelona, liverpool, man city tunaishia kudhalilishwa kimpira japokuwa tunapata ushindi, wachezaji kama ashley young, smalling, jones hata kama utawapeleka barcelona hawezi kubadilika tena kimpira kwa sababu wao wenyewe hawataki kubadilika kiuchezaji.

unapomuangalia gerrard pique jinsi anavyojiamini halafu unamuangalia smalling utafikiri mmoja kati yao amezaliwa na miguu minne kumbe wote ni sawa kihuduma wanazopewa na klabu zao. Ili tuimprove kwenye kumiliki mpira ni lazima eneo letu la ulinzi liundwe na wachezaji mfano wa lindeloff, shaw na hata eric bailly linapokuja suala la ubunifu na si nguvu.

marcus rashford, mctominay, sanchez, martial​
kwa ufupi wachezaji wengi wa kiingereza tabia zao zinafanana kiuchezaji kwa sababu ni wazito wa kuomba mipira tofuti na ilivyokuwa kwa paul scholes nyakati zake vile vile ukiangalia timu yetu kwa sasa tuna wachezaji takribani 6 ambao viwango vyao vinategemea na jinsi wanavyoamka.

kiukweli napenda sana kumuona rashford akifanikiwa kwa sababu ametoka kwenye damu ya manchester united lakini baadhi ya nyakati haeleweki anapomiliki mpira anakuwa ovyo sana utafikiri uwanjani anacheza na mbuzi. mimi nadhani kwanza waingereza waache kumjaza sifa za kumuaminisha ya kwamba uwezo wake anaweza kumfikia ronaldo, kabla hajafikia level za ronaldo ajaribu kwanza kufikia level za andy cole mmoja kati ya washambuliaji waliokuwa wanakupa faida kubwa sana kwenye eneo la ushambuliaji hata kama hafungi magoli.

kama nilivyosema mwanzo hata nyakati za alex ferguson tulikuwa hatumiliki mpira kama manchester city ya guardiola au chelsea ya maurio sarri kwa sababu si utamaduni wetu, tulichokuwa tukikifanya ni kumiliki mpira kwa kiwango cha wastani huku tukishambulia kwa posession, kwa ufupi ulikuwa unafahamu ni wapi movement za kutengeneza magoli zinaanzia na wapi zitaishia ndio maana safu yetu ya ushambuliaji ilikuwa na uwezo wa kufunga na kutengenezeana magoli mengi kupitia maeneo tofauti ukilinganisha na nyakati hizi ambapo tunategemea zaidi miujiza ya upande wa kushoto.

lakini pia kama umiliki wa mpira ni muhimu sana basi nyakati za LVG tulikuwa tunamiliki mpira kwa kiwango kikubwa lakini hatukuwa na mipango imara ya kushambulia ndio maana si ajabu kukuta mechi nyingi tuliishia kutoa suluhu. jambo muhimu ni kuhakikisha tunapokuwa na mpira adui anapaswa kuwa na pressure kubwa ya kufungwa na si kuwa katika hali ya kumfanya adui arelax kama kilichotukuta kwenye mechi zetu dhidi ya juventus na PSG uwanjani kwetu.

ball possession ni muhimu sana lakini bila ya kuwa na mipango imara ya kutengeneza nafasi na kujilinda tutakuwa hatuna tofauti na manchester united ile ya LVG au arsenal ya wenger.

kwa hili la kuwa na possession ndogo kwenye mechi kubwa tumhukumu ole msimu ujao ndio itakuwa ni muda sahihi zaidi kuliko wakati huu ambao ameikuta timu bila ya kuongeza chochote.

1552685426085.png
 
Duuh aisee kweli kuna watu wapo deep humu nimefurahi sana kusoma hoja zako humu mkuu sababu mawazo yako yanendana

sana na ninachofikiria mimi...kwa ufupi tunachokosa kikubwa kwenye hii club ni "Director of Football" kwenye modern football

sahiv hyu mtu lazima uwe nae mfano City yupo,Juve Yupo,Barca Yupo,Atletico yupo etc Club kubwa karibia zote,hyu mtu kazi

yake ni kuangalia Coach anataka acheze vipi na wachezaji watakaofaa kwenye huo mfumo ni wapi na kwenda sokoni kuwa

nunua,ukiangalia tunavyofanya usajili sisi nikama hatujui tunahitaji nini na ndo maana mwisho wa siku tunaishia kununua

wachezaji wengine level za chini mfano wakina Darmian na kuendelea kuwaongeza mikataba wakina Jones,wachezaji wa

maana kama kina De jong wanaishia kwenda Barca,Ed woodward ni Banker mwanauchumi sio DoF hana uelewa wa ndani wa

mpira hvyo hana uwezo wowote wa kumpinga Coach na haelewi club inahitaji nn,mfano Moyes alivyoomba Fellaini anunuliwe na

yye akaenda kumnunua tena kwa bei mbaya,hzi timu kama Juve na City wamefanikiwa kufanya usajili mzuri ndani na kipindi

kifupi sababu ya DoF hvyo naona nasisi inabidi tufanye michakato aje mtu wa maana pale kama Dof na nimeshasikia Club

inamtafuta mtu atakae fit hyo nafasi vizuri.
 
Ila mkuu pamoja na mambo mengine, mimi kama fans wa Man u , nikushukuru kutokana na mchango wako wakuitangaza Man u. Yaani kule liverpool, barca, arsenal threads nimeona kila timu una wish ikutane na man u quarter final.
Naona hata uzi wenu wa chelsea umeususa.

Sent using simu mbovu
Nilitaka hii itokee ..

Kelele zitapungua kabisa ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom