Weekend ndio hiyo, kiukweli mambo ni mengi mno na muda ni mchache
Kesho tupo na Gunners Emirates na naitazama hii mechi katika jicho chanya kwa upande wa Man Utd
Kama kuna mechi ambayo Arsenal walipaswa kushinda dhidi ya United msimu huu ilikuwa ni ile ya Old Trafford (enzi za Jose), lakini walishindwa..... Safari hii tena, ukiacha ile game ya FA Arsenal ni underdogs
Ushindi wa Man Utd dhidi ya PSG ni psychological boost kwetu. Ushindi ule umeonesha United anaweza kushinda mechi hata wakati odds zipo against them. This time odds are favouring us. Wakati huo huo kisaikolojia Arsenal hawajiamini sana kutoka na matokeo waliyoyapata siku ya Futuhi.
Kupona kwa baadhi ya wachezaji majeruhi wa Man Utd kunawafanya Arsenal wajione wanyonge zaidi (na wana haki ya kujihisi hivyo). OGS ametuambia kwamba Martial, Matic&/Herrera, watakuwa tayari kushiriki game hiyo, wakati huo huo Pogba aliyepumzika wiki nzima kutokana na kutocheza mechi dhidi ya PSG baada ya kupata red card atakuwepo, hii inatupa picha kuwa Arsenal itakutana na United imara siku ya jumapili.
Torreira kutokuwepo mechi ya kesho baada ya kula umeme kwenye game ya Spurs haitawasaidia Arsenal. Japo mimi siamini kama Torreira ana uwezo unaoimbwa kwenye vibanda umiza na mashabiki wa Arsenal lakini kwa kuwa kwao ni mchezaji muhimu, hivyo kukosekana kwao ni pigo kubwa sana.
Tutegemee battle nyepesi pale katikati kati ya Pogba, Matic, Herrera, Fredy, Tominay, Pereira (watatu kati ya hao niliowataja) dhidi ya mtoto wa miaka 18 Guendouzi, mcheza rafu Xhaka na labda Elney.
Historia itakuwa ina wawazisha sana hao jamaa wa Arsenal kwani hata wanapokuwa favourites huwa Man Utd tunawafunga au tunatoa draw, lakini vipi kuhusu sasa ambapo wao wanaonekana vibonde kwenye mechi ya kesho, nini kitawakuta?
United amecheza mechi jumatano Ufaransa na Arsenal amecheza siku moja mbele yaani alhamisi. Hiyo inamaanisha Arsenal amekuwa na muda mchache wa kupumzika na kujiandaa kwa ajili ya mechi ya kesho kuliko United. Nakumbuka Mourinho alivyokuwa Europa alikuwa analalamika sana kuhusiana na hii disadvantage, na hii ilikuwa sababu kubwa ya yeye kuamua kuyapa mashindano "mamoja" (Europa League) kipaumbele kukwepa ule msemo unaosema mtaka yote kwa pupa hukosa yote. Na alifanikiwa kuchukua kombe la Europa League.
Kitu pekee ninachoona LABDA kinaweza kuwapa moyo Arsenal ni kuwa nyumbani katika mchezo huo kwani katika game 7 za mwisho walizocheza nyumbani, Arsenal wameweza kushinda zote.
Wakati Arsenal wanaweza kufurahia kuwa na home advantage, pia watakuwa na kumbukumbu kuwa United yeye amekuwa na makali sana akiwa ugenini kwani kati ya mechi 9 za mwisho alizocheza ugenini ameshinda zote na nikumbushe tu kati ya hizo mechi alizoshinda ugenini ipo mechi ya Spurs, Chelsea, PSG na mechi ya ARSENAL.
Namalizia kwa kusema pamoja na yote niliyoyasema, tunahitaji wachezaji wetu wacheze katika viwango vyao tunavyovifahamu ili tuweze kushinda game hiyo.
Sent using
Jamii Forums mobile app