Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Sawa mkuu ni kweli hana control kama Morata

Lakini vitu vingine vyote amemzidi Morata

Kitu cha kutambua wachezaji huwa hawafanani mkuu

Hivi mfano kati ya Beckham na Quaresma au Kleberson unamkubali nani? Hao jamaa wawili walikuwa ni machachari, lakini Beckham japo hakuwa na anao anao lakini alikuwa ni hatari

Ni muhimu kutambua kila mchezaji ana strengths na weakness zake, Lukaku hana control kubwa sana (ila control anayo) lakini ana utilize strengths zake nyingine

Kuna siku nilisema tatizo Lukaku is not likable player ....... Hicho tu ndio kinamponza, yaani sometime watu wanamlaumu kwenye jambo hadi nabaki nacheka tu



Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuelewa mkuu, labda nikuulize, unaamini lukaku ni namba 9 wa kumtegemea atushindie makombe kama EPL? Kama ilivyokuwa RVP?
 
Leo matokeo yametoka kama nilivyotarajia Spurs na Arsenal wadraw na ss tushinde,pamoja na kwamba ushindi ulikuwa wakibabe

sana yaani tumeforce king pale...Hawa madogo wakina Mctominay wanajitahidi ila kiuwezo bado sana ndo yale niliyokuwa nasema

tunahitaji kufanya usajili wamaana summer, kiungo leo kilipwaya sana ila nilijua maana Saint miaka yote wapo vizuri sana pale kati

toka kipindi cha kina Wanyama walikuwa wanatusumbua Midfield,sema cha msingi tumechukua point 3..
Plus City kushinda japo naye kwa mbinde

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa ni kwanini hakumuachia mwenzake aondoke na mpira.

Pogba sio mpigaji mzuri wa penalty,sijui ni kwanini kocha kampa hayo majukumu. MUFC wapigaji wazuri wa penalty ni Mata na Herrera, haya young pia na Martial wanamzidi pogba. Tatizo ni masifa mengi.
Mkuu umewaza kama mimi
 
Kwasababu ametuokoa au?😀😀

Bado hakumfanyi kuwa kama akina Kun Agùero
Upgrade ya Lukaku labda Griezeman tu (kwa wachezaji waliopo sokoni)

Lakini Lukaku bado ni mchezaji muhimu kwetu, na tusipomthamini ataondoka tubaki na vitoto vile viwili tuone kitakachotukuta

Au tumuache halafu tum replace na striker wa £150mil tuishie kusajili wachezaji 2 tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwanza muelewe Pogba ndo mpiga penati wa timu yetu na kila timu ina mpigaji wake.

katika msimu huu Pogba amekosa penati mbili tu kati ya penati zote alizopiga na hazikuwa za ushindi kwamba eti akikosa hiyo penati timu itakuwa imepoteza mechi.

style ile ya upigaji ndo style yake hata akipataga huwa anapiga kwa style ile ya kukimbia hatua ndogondogo.

hakuna anaejua kama Lukaku angepata ile penati maana hata yeye ameshakosa penati akiwa na United under Mou, ila ki-fair play Pogba alipaswa ampe Lukaku huenda ingekuwa hat trick ya kwanza tangu RVP afanye hivyo msimu wa 2013 against Olimpiacos under Moyes.

OLE
MUFC
GGMU
Aya ya mwisho hiyo ......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anacheza vzr sana akicheza kule juu pembeni kuliko kati
FB_IMG_1551550439120.jpeg
 
Nimekuelewa mkuu, labda nikuulize, unaamini lukaku ni namba 9 wa kumtegemea atushindie makombe kama EPL? Kama ilivyokuwa RVP?
Anaweza kutushindia

Lakini inabidi ifanyike surgery ya timu hasa kumuongezea nguvu ili aishwe mipira

Probably tukipata midfielder wa kumpa nguvu Pogba, winga mtundu wa kaliba ya akina Silva wa City au mpiga krosi nzuri na tukiimarisha nyuma (kumbuka timu ya ushindi inaanza kujengwa nyuma) tuna uwezo wa kuchukua kombe na Lukaku

Hivi mkuu kuna forward ambaye anatumia kila nafasi ya kufunga? Yaani ana convert 100% ya nafasi za magoli anazopata.

Aina ya wachezaji kama Lukaku ni wachezaji wanaotaka service, sasa kwa United pale creative players ambao sio wachoyo ni wawili tu ambao ni Pogba na Mata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuelewa mkuu, labda nikuulize, unaamini lukaku ni namba 9 wa kumtegemea atushindie makombe kama EPL? Kama ilivyokuwa RVP?
Striker peke yake hawezi kukupa ubingwa, ubingwa unapatikana Kwa timu nzima kuanzia kipa,beki, viungo na washambuliaji kucheza vizuri , Leicester walichukua ubingwa striker akiwa Vardy.Kwa miaka 3 iliyopita Hary Kane ndio striker bora EPL lakini hajawahi kuwapa Spurs ubingwa.

RVP alicheza Arsenal miaka karibia 10 lakini hakuwapa ubingwa sababu timu ilikuwa mbovu alivyokuja United (ilikuwa timu bora) msimu wa kwanza tu akachukua ubingwa

Romelu Lukaku yupo kwenye top 20 ya wafungaji bora wa muda wote kwenye EPL na ana miaka 25 tu licha ya kuwa na control mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom