Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Aaah jamaa mbona akiwa anatupia mnamsifia siku ikiwa sio yake mnamponda hivi Bolingoli wa watu?
Japo wewe sio united, lakini umeuliza swali la msingi sana hapa

Hao watoto akina Rashford na Martial sijui wanafanya jambo gani kubwa kiasi cha baadhi ya watu kumchukia Lukaku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Chicharito.

Sent using Jamii Forums mobile app
Chicharito alikuwa ni pocher tu

Lakini Lukaku anafanya mambo mengi mno

Hata kwenye build up ya magoli mengi huwa inaanzia kwake

Mfano akipata mpira na yupo peke yake, anaweza ku hold mpira kusubiri team mates. Angalia mfano game ya Cristal Palace licha ya kufunga magoli 2, goli la Young lilianzia kwake, Pogba then Young

Angalia pia, mchango wake timu inapokuwa haina mpira (defensive duties), anakaba na anajitoa sana. He plays for the badge.

Anapokuwa na mpira na hayupo kwenye nafasi nzuri ya kufunga, sio mchoyo..... Anatoa pasi pale wenzake wanapokuwa pazuri zaidi yake.

Movement zake hasa kwenye mipira ya juu,hata asipofunga kwa kichwa anaweza ku disturb mabeki wa timu pinzani na team mates wake wakafanya jambo.

Kumbuka bila Lukaku tunategemea mipira ya kukimbizana tu (one dimension) kwa hiyo tukikutana na timu inayopaki hatuwezi kufanya jambo. Lukaku anaweza kutupa dimension ya mbio (maana na yeye ana mbio) na mipira ya juu.

Lakini lingine Lukaku ni nuisance kwa mabeki wa timu pinzani, sidhani kama mabeki wa timu pinzani wana enjoy kumkaba Lukaku with his physical presence





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom