Since miaka ya mwisho ya SAF Man City walishaanza kuwa tishio kwetu (nakumbuka wanatufunga 6-1,na tulivyowafunga 4-3 Owen anafunga goli la ushindi) tangia hapo sisi tunarudi nyuma wao wanazidi kuimarika na kama management hawataamka very soon wataanza kutuacha
Wakuu
Belo na
Damushin heshima kwenu kwa michango yenu iliyoshiba kuhusu klabu yetu pendwa hasa kipindi hiki tunapo batizwa kwa moto kila uchwao.
Kuhusu mstari wa mwisho naomba nitofautiane na ninyi ifuatavyo: Manchester ya Fergie haikuwekeza kuifunga city wala top clubs za wakati huo kama arsenal,chelsea na liverpool kama kipaumbele chake. Fergie alikuwa anahakikisha timu zilizo nje ya top 4 anakusanya point nyingi kadri iwezekanavyo kuliko kukomaa na game 1 ngumu halafu ukikutana na blackburn,portsmouth,astonvila,etc unapigwa au kudroo.
Hata sasa kama united hii ingekuwa inafungwa na big 4 zote lakini ikachukua ubingwa tusingejali kama city amesajili wachezaji wazuri au la.[/QUOTE]
maelezo yako yenye madai ya kuwa sir alex ferguson alijenga timu kwa dhumuni la kupambana na timu zote zinazoshiriki ligi kuu ya uingereza yana ukweli kwa asilimia kubwa sana muheshimiwa
fuentte na sababu kubwa ni kuwa timu kubwa zitakupa jumla ya pointi 18 kwa msimu mzima lakini unapozifunga timu za wastani zitakupa pointi 96 kwa msimu mmoja, tokea nianze kufuatilia mpira wa miguu na umri wangu huu unaokaribia robo karne tokea nizaliwe ni Tanzania pekee ndio nimeshuhudia klabu kubwa za
simba na yanga ndio zinazotengeneza timu kwa ajili ya kuhakikisha pindi watakapokutana mmoja wapo asifungwe na mwenzake, namaanisha ya kwamba simba au yanga yupo radhi afungwe na
Pamba FC au
ashanti united mechi zote mbili kuliko kufungwa mechi moja tu na mtani mwenzake asiyekuwa na uwanja hata wa mazoezi.
takribani miezi minne tokea msimu wa ligi umeanza nchini uingereza kwa kiasi kikubwa humu ndani tumekuwa tukijitahidi wachangiaji tofauti kuzungumzia mwenendo wa manchester united, yameshazungumzwa mengi sana lakini kwa kiasi kikubwa michango mingi utakayokutana nayo humu ndani yanakupa mambo mawili makubwa ambayo ndio yanayoisumbua manchester united kwa miaka hii.
- kupoteza nguvu na ushawishi wa kupambana na timu pinzani zote 19 zinazoshiriki ligi kuu ndani ya uwanja.
- kupoteza nguvu na uwezo wa kupambana na uwekezaji wa manchester city kadri miaka inavyosogea mbele ndani ya uwanja na nje ya uwanja ijapokuwa hizi athari za nje ya uwanja hazijajidhihirisha waziwazi kwa kiasi kikubwa.
Tatizo la kwanza lilianza baada ya kuondoka mwanadamu mgumu, muelewa na mwenye kwenda na wakati anayeitwa sir alex ferguson ndani ya klabu ya manchester united lakini tatizo la pili lilianza kuota mizizi mirefu na migumu kuing'oa tokea nyakati za sir alex ferguson akiwa madarakani. Tuachane na tatizo la kwanza ambalo linazungumzwa kila siku humu ndani turudi kwenye tatizo la pili ambalo amelizungumza Belo kupitia comment yake hapo juzi.
baada ya msimu wa 2007/2008 kumalizika ambapo manchester united walibeba ubingwa wa ligi kuu na ligi ya mabingwa kwa kuifunga chelsea vugu vugu la maandalizi ya msimu mpya wa 2008/2009 lilianza rasmi barani ulaya, nchini uingereza kwa kiasi kikubwa habari zilizokuwa zinazungumzwa zaidi kwa miezi miwili ya usajili ni :
- habari ya dimitar berbatov kutakiwa na manchester united
- habari ya robinho kutakiwa na chelsea.
- mwishoni ni habari ya waarabu kutaka kuinunua newcastle united baadae man city.
September 1- 2008 ambayo ilikuwa ni siku ya kwanza kwa matajiri wa kiarabu kuanza rasmi kuimiliki manchester city ambayo mwanzoni ilikuwa inamilikiwa na tajiri fisadi
thaksin shinawatra ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa Thailand ndipo balaa lilianzia . Jambo la kwanza walilolifanya hawa waarabu walituma ofa ya paundi millioni 32.5 kwa muhuni
daniel levy ambaye ndiye mwenyekiti wa tottenham hotspurs kwa ajili ya dimitar berbatov kumbuka upande wetu kwa miezi 2 tulikuwa tunampigania kwa ofa ya paundi millioni 27- 30.
Unapodhamiria kutanua himaya yako ya utawala jambo muhimu la kwanza unalotakiwa kulifanya ni kuanza kuwatawala majirani zako kwanza ndipo ufanye maandalizi ya kuwatawala maadui wako wa mbali, kitendo cha waarabu wa etihad kutuma ofa kwanza kwa
berbatov ambaye tulikuwa tunampigania kwa miezi miwili ilikuwa ni ujumbe tosha kwetu sisi wenye kuonyesha dalili za wazi za majirani kudhamiria kututawala sisi kwanza ndipo waelekeze nguvu kwa wengineo. Bahati nzuri siku hiyo mzee fergie akafanikiwa kuvunja dili la berbatov la kuelekea manchester city baada ya kuongeza dau na pia kumtoa Fraizer Campbell kwa mkopo. balaa likawageukia chelsea ambao na wao pia miezi 2 walikuwa wanahangaika na
robinho kutoka real madrid na hatimaye chelsea wakapokonywa tonge mdomoni baada ya manchester city kukubali kulipa paundi millioni 32 na mshahara unaofikia million 270 kwa wiki.
maumivu haya tunayoyapata kipindi hiki yasingelikuwa makali sana laiti kama waarabu wa etihad wangelifanikiwa kuinunua klabu yoyote kama newcastle united kwa sababu sisi ni wababe wa mji wa manchester na pia ni wababe wa nchi nzima ya uingereza kisoka na wanachokihitaji man city ni kutuondolea heshima ya ubabe wa uingereza na ubabe wa mji wa manchester na dalili zinaanza kuonyesha man city wanaelekea kwanza kufanikiwa kuondoa ubabe wa man utd ndani ya jiji endapo tusipokuwa makini.
- mwanzoni ukiangalia upande wetu sisi kwa kiasi kikubwa sana tulikuwa tunajenga timu kupitia mfumo wa kununua wachezaji ambao walikwisha tengenezwa na timu nyengine mfano nistelrooy, veron, andy cole, yorke, berbatov, ferdinand n.k
- kuwapa nafasi vijana waliofaulu kupitia mfumo wa academy mfano cleverley, welbeck, brown, chadwick, oshea, scholes, gibson, fletcher n.k
- kununua wachezaji ambao wanakuja kutengenezwa kwa asilimia fulani ndani ya klabu mfano ronaldo, rafael, fabio, chicharito, vidic, smith, marehemu liam miller kutoka celtic n.k
kwa hivyo ulikuwa unakuta kwa muda mrefu ndani ya manchester united ulikuwa unakutana na timu yenye muunganiko wa wachezaji wa aina kuu mbili kwenye kikosi cha kwanza.
- wale wenye viwango vikubwa sana tokea mwanzoni mfano ferdinand, roy keane,van persie, giggs, berbatov, tevez, scholes n.k
- wale wenye viwango vya wastani ambao wanahitaji kwa kiasi kikubwa uwepo wa wachezaji wenye viwango vikubwa ili wapate kujijenga zaidi kiuwezo kwa mfano ujio wa chicharito, ujio wa smalling oshea, evans n.k.
ukija upande wa majirani zetu wanapoingia sokoni wanatafuta wachezaji watakaowapa faida ya hapo kwa hapo, aina hii ya ujengaji wa timu unapobahatika kupata wachezaji wenye viwango vikubwa sokoni basi huchelewi kupata mafanikio tofauti na yule anayejenga timu kwa kutumia aina tatu nilizozieleza hapo juu ambazo kwa kiasi kikubwa ndio tunazozitumia mwanzoni. Kwa mfano angalia chelsea walivyopata mafanikio ndani ya muda mfupi baada ya kufanya uwekezaji wa wachezaji waliokwishaiva kwa ajili ya mapambano iliwachukua miaka miwili tu kujitangaza kwenye ulimwengu wa soka.
wakati wewe unamsubiri
welbeck,
gibson,
cleverley apandishe kiwango chake ili awe mrithi wa
paul scholes, rooney na
michael carrick pindi watakapochoka mwenzako anakwenda spain kumng'oa
yaya toure,
sergio aguero na
david silva ili wampe mafanikio ya haraka.
mwanzoni kabla ya mabepari hawajavamia mchezo wa soka tulikuwa hatupati tabu sana kwa sababu wapinzani wetu wakiwemo arsenal, walikuwa na mfumo huu tunaoutumia sisi ila tofauti
mzee wenger alikuwa haendi na wakati ukimlinganisha na
alex ferguson,
mzee wenger alikuwa na tabia za kuwa tayari kuvumilia miaka mitatu akimsubiri
fabregas au
henry ili azibe tatizo lakini
fergie alikuwa hana tabia hiyo ndio maana ilifika baadhi ya nyakati hakuona tabu kufungua pochi lake kwa dhumuni la kufanya malipo ya gharama kubwa kwa ajili ya kutatua tatizo la timu yake, kwa mfano jaribu kurejea usajili wa
michael carrick,
van persie,
rio ferdinand,
dwight yorke, nistelrooy n.k.
ukiachana na mbinu, ubora na uzoefu wa kocha kwenye mashindano timu yenye muunganiko wa aina mbili nilizozieleza inapokutana na timu inayojengwa kwa mfumo wa kukusanya wachezaji nyota watupu ndani ya kikosi lazima timu A itapata tabu kuliko timu B itakavyopata tabu. Bahati mbaya sana nakiri hadharani nyakati za mwisho za alex fergie timu yetu tayari ilishajaza zaidi group hili la wachezaji wenye viwango vya wastani kuliko group la wachezaji wenye viwango vikubwa ila ubora wa kocha ndio ulitufanya tutembee kifua mbele kwa miaka ya mwishoni.
jaribu kufikiria hizi baadhi ya biashara tulizozifanya kwa nyakati tofauti.
- tulimuondoa mchezaji bora ronaldo ambaye ana uwezo wa kukupa magoli 40 kwa msimu tukaleta wachezaji wa wastani akiwemo valencia, obertan, michael owen. Dili la ronaldo lilipaswa kuzibwa na watu kama frank ribery kipindi kile, tatizo la kuwa na wachezaji wenye viwango vya wastani ndani ya timu ndio hili hawakupi uhakika wa kupandisha viwango vyao kwa haraka kama alivyozungumza Belo.
- tulikataa kumsajili carlos tevez ambaye majirani zetu walimchukua kwa paundi 27 millioni, huyu tevez aliondoka msimu mmoja na ronaldo. inamaana tuliwaondoa watu wawili wenye uwezo wa kukupa magoli 60 kwa msimu mmoja na nafasi ya tevez ilizibwa na msenegal mame biram diouf ambaye alishindwa kufikia matarajio yetu. carlos Tevez alipokwenda etihad alifunga magoli 29 msimu wake wa kwanza na kuifanya city ishike nafasi ya 5 wakati msimu wa nyuma yake man city walishika nafasi ya 10. Hivyo tuliendelea kumtegemea rooney huku tukisubiri dimitar berbatov aweze kuendana na falsafa ya timu. Msimu wa 2010/2011 carlos tevez aliwasaidia man city kushika nafasi ya 3 baada ya kufunga magoli 23 wakati man utd tulibeba ubingwa na kufungwa na barcelona. msimu huu kiupande wetu dimitar berbatov anafunga magoli 21 kwa msimu mzima. Msimu huu balaa la kuwafunga man city kwa tabu likajiendeleza tena, unakumbuka tik tak la wayne rooney?
kwa ufupi ukianzia mwaka ambao man city wanafanya sajili za wachezaji waliokwisha tengenezwa na timu nyengine kiupande wetu sisi wale wachezaji wenye viwango vikubwa walikuwa wapo katika nyakati zao za mwisho na wale wanaopaswa kuziba nafasi za mafundi kama giggss (umri 37), scholes (umri 34), evra (32), vidic (31), ferdinand (33) ,carrick (32), rooney (30) kupitia mfumo wa academy au kuwanunua kupitia timu nyengine viwango vyao wengi wao vilibaki vile vile bila ya kufikia viwango vya mafundi wetu, ni
David De gea peke yake ndiye anatupa faida ile tunayoihitaji kwa kuweza kuziba nafasi ya
edwin van der sar.
ndio tukasema tishio la man city lilianza tokea nyakati za mwisho za alex ferguson akiwa madarakani bila ya kusahau kipigo cha magoli 6, tuacheni na habari za mzee wetu sir alex ferguson ambaye alijenga emperor kubwa kwa miaka 26 ya utawala wake pale old trafford.
hivi labda tujaribu kujiuliza
- jee smalling na phil jones kabla na hata baada ya kuondoka fergie wamefikia angalau viwango vya ottamendi na vicent kompany ambao hawana nafasi kwa majirani zetu? cha ajabu hawa wote wawili walicheza pamoja na walinzi bora kwa zaidi ya miaka 10 ambao ni vidic na ferdinand, lile dhumuni la kuwanunua wakiwa na viwango vya kawaida na kuwatengeneza ili kuziba nafasi za magwiji wa ulinzi halijazaa matunda kwa asilimia 40 kwa maoni yangu lakini.
lakini upande wa pili wa shilingi tokea aondoke ferguson cha ajabu tumeachana kabisa na mpango wa kununua wachezaji wenye viwango vya kawaida na tumeiga tabia za majirani zetu za kufanya uwekezaji wa wachezaji waliokwisha tengenezwa moja kwa moja na timu nyengine lakini cha kushangaza sana matokeo tunayoyapata afadhali ya ferguson na gurupu lake la wachezaji kama vile
obertan, buttner, fabio, bebe, macheda aliweza kupambana dhidi ya manchester city na timu nyengine japokuwa presha ilikuwa kubwa kuliko hawa wazee wa kutumia hela waliorithi nafasi ya fergie
mambo yanayoendelea kutuumiza vichwa na kutufanya tugawanyike kimtazamo
- je turudi tena zama za ferguson za kusajili wachezaji wenye viwango vya wastani na wale wenye viwango vikubwa huku tukiendelea kuwavumilia kwa miaka angalau 3 tukiwa chini ya mwalimu asiyekuwa na presha yoyote, nyakati za ferguson tuliwahi kukaa miaka 3 bila ya ubingwa na miaka 3 baadae tukachukua makombe kwa miaka 3 mfululizo (rejea misimu ya 2003, 004, 005, 006,007 na 2008).
- kama leo hii tunasajili wachezaji bora tunaishia nafasi ya 2 hadi ya 7, vipi kuhusiana na hawa average kama walivyokuwa akina vidic, heinze, alan smith, ronaldo kutoka sporting si tutaishia nafasi ya 10? kwa sababu majirani zetu hawatoacha mfumo wa kununua wachezaji bora labda makocha wa timu pinzani wawe na akili za arsene wenger
- je tunasajili wachezaji bora au tunauziwa wachezaji wenye majina bora?
- tatizo letu ni mwalimu na uongozi wa manchester united?
- kama tatizo ni uongozi mbona nyakati za fergie alifanya kazi na watu hawa waliopo madarakani lakini matokeo mazuri yalionekana?
- kama tatizo ni walimu mbona jose na van gaal wana cv nzuri?
- mbona david moyes alisifika kwa kuwapa nafasi vijana alipokuwa everton lakini kwetu kashindwa, rejea ubora wa wachezaji kama vile rodwell, jagielka, baines, pienaar steven, osman leon, arteta n.k?
- mbona majirani zetu wachezaji wao waliofeli wanahesabika?
- je laana ya liverpool tumeirithi sisi hivyo basi hata kama tutamsajili messi na guardiola ndio yale yale? (mhhhh ila mimi siamini ujinga huu)
miaka 6 tumefanya usajili wa wachezaji wafuatao lakini hatujawahi kuvuka hata robo fainali ya UEFA wakati majirani zetu wamefika nusu fainal zaidi ya mara mbili, huu usajili tulioufanya kwa kuangalia majina yao ni wachezaji wanaopaswa kukupa ubingwa tena mbele ya timu ngumu kama ya real madrid na barcelona.
sir alex baada ya kufungwa nusu fainal na AC milan msimu uliofuata alimuongeza tevez, owen hargreavez, anderson na luis nani tukabeba ubingwa lakini nyakati hizi balaa liko palepale licha ya usajili tunaoendelea kufanya
paul pogba = 95 million
mkhitaryan = 25 million
lindeloff victor = 30 million
marcos rojo = 15 million
luke shaw = 27 million
eric bailly = 25 million
lukaku = 75 million
nemanja matic = 30 million
fred = 55 million
diogo dalot = 20 million
antony martial = 55 million
juan mata = 27 million
maroaunne fellaini = 27 millioni
herrera ander = 27 million
depay memphis 17 million
schneiderlin = 26 million
angel dimaria = 54 million
daley blind = 15 million
matteo darmian = 14 million
bastian schweinsteiger = 3 million
radamel falcao = mkopo.
ibrahimovic = free
- ndani ya miaka 10 hii manchester united wamebeba makombe 3 ya ligi kuu ya uingereza
- ndani ya miaka 10 hii chini ya utawala wa sheikh mansour man city. wameshinda makombe 3 ya ligi kuu ya uingereza.
- ndani ya miaka 10 hii chelsea wamebeba makombe 3 ya ligi kuu ya uingereza.
- ndani ya miaka 10 hii leicester city wamebeba kombe 1 la ligi kuu.
- bila ya kusahau ndani ya miaka 10 arsenal, liverpool kwa pamoja wameendelea kuwa washiriki wa ligi kuu.
mpaka muda huu manchester city yupo juu ya man utd kwenye msimamo wa ligi kuu, tukisema manchester city anamzidi manchester united kwa miaka 10 hii ninakosea?