Kocha wa Manchester United Jose Mourinho
amewataka waandishi wa habari kumuheshimu
baada ya timu yake kupata kipigo cha magoli
3-0 wakiwa uwanja wa nyumbani dhidi ya
Tottenham.
Mourinho akionekana kukerwa na maswali ya
waandishi, alinyanyuka kitini na kukatisha
mahojiano na wanahabari baada ya mchezo huo
uliopigwa katika uga wa Old Trafford.
Kipigo hicho cha Jumatatu usiku ndio kikubwa
zaidi akiwa uwanja wa nyumbani toka aaze
maisha yake ya ukocha, na pia kwa mara ya
kwanza amepoteza michezo miwili kati ya mitatu
ya mwanzo ya ligi.
"Nimeshinda mataji mengi ya ligi (ya England
EPL) kuliko makocha wote 19 (wa timu nyengine
zinazoshiriki EPL) ukiwaweka pamoja," amesema
Mourinho. "Nimeshinda mataji matatu na wao
mawili."
"Heshima, heshima, heshima bwana," aling'aka
Mourinho akitoka kwenye chumba cha mikutano
ya wanahabari.
Mourinho awatahadharisha Manchester
United
Mourinho 'hatastaafu akiwa Man Utd'
Goli la kichwa la nahodha Harry Kane na mawili
mengine yaliyofungwa na Lucas Moura yameipa
ushindi wa tatu mfululizo Tottenham na
kuwapandisha mpaka nafasi ya pili kwenye
msimamo wa EPL.
Mourinho, raia wa Ureno amenyenyua taji la EPL
mara tatu kwa vipindi viwili tofauti akiwa na
Chelsea, wakati Pep Guardiola na Manuel
Pellegrini wakishinda mara moja kila mmoja
wakiwa na Manchester City.
Mreno huyo pia ameshinda mataji mawili ya ligi
ya Ureno akiwa na Porto, mawili Italia akiwa na
Inter Milan, na moja Uhispania akiwa na Real
Madrid. Pia ameshinda mataji mawili ya klabu
bingwa Bara la Ulaya. Taji kubwa zaidi alilolitwaa
na Man United ni kombe la Europa mwaka 2017.
"Mnataka kama kufanya muujiza juu ya timu
yangu, ambayo ilicheza vizuri na kwa mpango,
tulikuwa vizuri sana lakini mmekuja hapa na
mnajaribu kuugeuza mkutano huu kwa
kuniangushia mzigo wa lawama," alifoka
Mourinho.
Mourinho anatafuta vijisababu vya kuhama
Man Utd?
Alipoulizwa namna United walivyojilinda dhidi ya
Spurs, alikuwa na haya ya kusema: "Samahani.
Inabidi uniambie kitu gani ni muhimu zaidi maana
sielewi. Pale ninapopata ushindi, ninapokuja hapa
mara nyingi tu mnaniambia hamkufurahishwa na
namna timu ilivyocheza."
'Wachezaji hawamtaki Mourinho'
Mshambuliaji wa zamani wa Blackburn na
Chelsea, Chriss Sutton ameiambia BBC kuwa
inaonekana kama wachezaji wa Man United
hawamtaki kocha wao.
"Sidhani kama Spurs walikamia mchezo toka
dakika za awali, lakini pale walipoweka mguu
chini, wakaitawala timu ammbayo haina uongozi.
Kuna lawama nyingi zinatolewa kwa sasa na
wachezaji wanaonekana hawataki kucheza chini
yake (Mourinho)."
Kwa mujibu wa Sutton, kwa kiwango
kilichooneshwa na kama kocha angekuwa ni
Louis van Gaal basi mashabiki wangekuwa
wanaimba nyimbo za kutaka atimuliwe.
"Rekodi ya Mourinho ni nzuri kweli, lakini kama
Man United wanataka kukubaliana na uduni, basi
hiyo ndiyo hali yao kwa sasa. Man City na
Liverpool wapo katika kiwango tofauti kabisa,"
amesema Sutton na kuongeza, "Ni aibu kupokea
kipigo cha 3-0 na sijui baada ya hapa, wao kama
timu au kocha wataelekea wapi."