Manchester United (Red Devils) | Special Thread

WANASEMA hivi, dawa ya jeuri kiburi. Winga Anthony Martial anawafanyia jeuri Manchester United, basi nao wameamua kumjibu baada ya kuelezwa watafyeka mshahara wiki mbili kutokana na kitendo chake cha kutoweka mazoezini kwa siku nane.
Imeelezwa hivi, kutokana na hilo, Martial ambaye aliondoka kambini kwenda kwa mpenzi wake, Melanie Da Cruz, aliyejifungua mtoto hivi karibuni, ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake kwa siku nane na hivyo, panga kali litapita kwenye mshahara wake, baada ya kumpiga faini ya Pauni 180,000 ambayo ni sawa na mshahara wake wa wiki mbili
 
Three man midfield rotation:

1️⃣ Pogba - Matic - Fred
2️⃣ Pogba - Fred - Pereira
3️⃣ Matic - Fred - Pereira
Fred hawezi kumuweka bench Pogba. Nafikiri Pereira na Fred ndiyo watakuwa wanabadilishana nafasi. I wish Pogba aongeze umakini kulenga goli.

Halafu nafikiri tofauti na wengine, MUFC itakuwa moto sana msimu huu. Ubingwa upo hakuna sababu ya kuwa wanyonge.
 
Nakuunga mkono mkuu
 

1️⃣ Pogba - Matic - Fred
2️⃣ Pogba - Fred - Pereira
3️⃣ Matic - Fred - Pereira[/QUOTE]

Ina maana Herrera atakuwa mchezaji wa qarabao na FA tu,au sababu ya upya wa hao wachezaji?
 
1️⃣ Pogba - Matic - Fred
2️⃣ Pogba - Fred - Pereira
3️⃣ Matic - Fred - Pereira

Ina maana Herrera atakuwa mchezaji wa qarabao na FA tu,au sababu ya upya wa hao wachezaji?[/QUOTE]Hapana mkuu hiyo sio official kila mchezaji ana nafasi tunajaribu kuchek dimba la kat litakuwaje hapo bado kuna mata,fellain,scott wengi tu
 
Manchester United defender Chris Smalling has agreed a deal with Wolves, according to reports in the Daily Express.
The England international is contracted to Old Trafford until the summer of 2019.
 


 
Adidas hana ubavu wa kuvunja mkataba kwa situation ya sasa ya Man U na akiondoka unakuja mkataba mkubwa zaidi ya huo.

Unafuatilia mauzo ya jezi? Watu kama Depay, Bastian etc hawawezi popote duniani kuingia top 5 ya wauza jezi bora duniani isipokuwa manchester. Yule neymar mkali pale barcelona alikuwa akisubiria kwa depay mauzo ya jezi.

Demu wa lindelof alikuwa na kablog kake uchwara sasa hivi mamilioni ya watu wanaingia kila siku,

Mambo haya unayapata man utd tu hata madrid na barca hawana nguvu ya kui challenge man u linapokuja suala la biashara, hapa ondoa hofu.
 
Wote hao uliowataja nani ana cv kali kuliko Van Gaal?
 
Ukisema wachezaji wa kawaida unakuwa umemaanisha nini?

Pogba,matic,fred,herrera pereira
Lukaku,martial,sanchez,degea,bailly,shaw,young..wote hawa ni wachezaji wa kawaida??...wachezaji wasio wa kawaida ni akina nani??
Ukimtoa sanchez na de gea pengine na matic waliobakia wote ni vijana ambao wanahitaji kushikwa akili watulie.
Hebu tuangalie
MADRID~ experience ya modric na kroos katikati, una ramos nyuma na benzema na ronaldo mbele(kabla hajaenda juve) hapo bado kuna marcelo pia. Wote ni wachezaji ambao ni winners wana makombe kibao wanajua wawin vipi mechi.

MAN CITY~ wana silva na fernandinho kati wana Aguero na nyuma yupo kompany bila kumsahau de bruyne japo si sana, wote hawa ni viongozi wanaotuliza timu

BARCELONA~ kuna Pique, Bosquet, Messi, Jordi Alba na Iniesta kabla hajastaafu wote hawa uelewa wao wa club na uongozi wao kwa wachezaji wengine utamfananisha na nani?

JUVENTUS~ huku ndio usiseme kina Chielini, Buffon kabla hajaondoka, Higuain, marchisio, Matuidi etc wote wanajua nini maana ya kuchezea juve.

Sisi Angalau Pogba baada ya kuwin world cup anaweza kuwa matured msimu huu na kutusaidia ila wachezaji wetu wengi wana potential ila bado kuwa viongozi wa timu na kuwa na experience ya kuua mechi. Mtu kama martial, Rashford, shaw, pogba, Lingard, lukaku, wote wana utoto mwingi sana huwezi fananisha na hizo club hapo juu.

Mourinho amefanya kazi kubwa sana na hio timu na point 81 sio mchezo Leicester amechukua ubingwa na hizo point, its just Man city amefanya vizuri sana, ila sisi pia tumefanya vizuri, na naamini tuna kocha sahihi
 
Herrera kati ya casemiro, modric na kroos anamueka nani bench?
 
Rashford na Martial sio winga wa asili na wote wanacheza upande wa kushoto tunahitaji winger wa kulia, kama unaangalia mpira.

Mchezo wa rashford na martial ni akipata mpira anaingia ndani wachezaji hawa wanaitwa wing forward,

Tunaohitaji sisi ni winger wa kizamani design ya beckham ama giggs ama valencia etc ambao wakipata mpira wanatia majaro, tuna mtu kama Pogba, Lukaku, smalling, Fellaini etc wote ni magiant wanahitaji sana cross ila hatuna mtu wa pembeni wa kuzileta.
 

Mkuu Katika Modern Football kwani Bado Upo Mpira huu Wa Winger Kibendera?
Mbona sasahivi Mawinga wote Ni Mafoward ambao unawakutia Wanafunga Magoli mengi Kuliko Mastriker!!
Winger Wa Kina Beckam umeshapotea Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…