johnmweusi
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 201
- 268
Unajua tunacho tofautiana ni kitu kimoja. Mourinho ni binadamu na ana mapungufu kama walivyo binadamu wengine. Ila unacho sahau ni kwamba kila kocha ana hitaji watu wa aina Fulani ili kuweza kufiti kwenye mfumo wake. Usipo mpa watu wanao fiti kwenye huo mfumo basi usitegemee kupata Matokeo mazuri.Kama bodi ya utd ingekuwa inaangalia mpira wa Pasi nyingi (mpira mnao ita ni wa kisasa) LVG asinge fukuzwa. Shida ya Manchester haikuwa kucheza mpira mzuri shida KUBWA ni makombe. Na hii task aliyeonekana(binafsi naamnini anayeweza kufanya mpaka saiz) ni Mourinho.Hahaaha nyie jamaa mnachekesha. Si huyu huyu mou Anampanga Smalling na Benchi anakuwepo Rojo au huwa hamna macho.
Nakujibu tu, Namba ya matic , herera anacheza vyema kabisa. Na mmesahau herera alivyokuwa anapigwa benchi.
Katika Kipindi Cha mourinho amesajili wachezaji tisa. Kwa kocha mwenye uwezo tungekuwa tunaona soka la maana hata kama team inakuwa inafungwa. Timu kila siku back pass. Hivi mfumo wa back pass ni mpaka uwe na wakina Ronaldo na Messi ndio usicheze hivyo.
Mou ni mweupe kimbinu. Anatuharibia team tu hana lolote. Ni bora asipewe hela afukuzwe aje kocha mwenye mbinu za mpira wa kisasa. Sio kumwaga hela kwa kocha wa hovyo. Team inapack basi muda wote mpaka pre-season.
Nasikia Anataka amuuze Rojo huu si ujinga kabisa ,halafu anataka hela asajili beki. This is totally wrong disbursement of Funds. Kutwa kuongea shits kwa wachezaji.
Wachezaji wote ambao walikuwa na promising performance kipindi cha Van Gal chini yake wote wamekuwa butu kutokana na mambinu yake ya kujihami kuliko kusakata soka. Rashford na Martial ni mfano tu.
Kipindi cha kati hapa alianza kumchezesha Pogba kama Holding Midfielder mpaka Giggs na Paul scholes siku hiyo walikuwa BT sports walilalamika sana kuwa mourinho anataka kuua kipaji cha Pogba.
Chini ya Mou team haiwez fika kokote.
Kwa mtazamo wangu ukiniuliza kuhusu Rojo kutaka kuuzwa naona wameangalia udhaifu wa Rojo. Rojo ni beki mzuri na anatufaa kabisaa ila shida ni MTU ambaye huna uhakika wa yeye kucheza mechi tano mfululizo(injuries). Na ukimuweka sokoni anauzika Kwa bei mzuri, sasa kwanini usichukue hela hiyo halafu ukatafuta beki ambaye sio injury prone??
Tangu Fergie ameondoka basi msimu uliopita ndio msimu bora kwa Man utd kwenye ligi ila kilicho tuangusha ni kwamba Man City alikuwa bora zaidi yetu.
BODI IMPE MOU WANAJESHI ANAO WATAKA, BAADA YA HAPO NDIO TUTOE HUKUMU.