lembu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2009
- 19,363
- 25,458
Falsa
Makocha wote uliowataja kila mmoja kafukuzwa kwa makosa tofauti. Na kazi ya ukocha ndio pekee iliyobaki duniani na falsafa ya kuajiri na kufire
Mou hakufukuzwa Chelsea kwa sababu ya falsafa yake mbovu au haifai bali kuokoa jaahazi kwa sababu ya kutofautiana na baadhi ya wachezaji muhimu kwenye timu. Kwa silimia 70-80 makocha wengi hufukuzwa kwa sababu hiyo hiyo ya Mou pale Chelsea
Niseme kuhusu falsafa ya kupaki mabasi. Kila kocha anaitumia hiyo falsafa isipokuw tu hawafanyi rasmi. Mou alipohojiwa juzi juzi almuuliza muuliza swali nenda kawaulize akina Keane enzi zake akipoteza mpira katikati ya uwanja je atabaki katikati ya uwanja au atarudi nyuma kukaba? jibu ni kwamba atarudi kupaki mabasi!
Timu inayozidiwa lazima ipaki mabasi na timu nzuri obviously haiwezi kupaki mabasi bali itacheza mpira. Makocha wote wanafahamu hili
Kamuulize Luiz Felipe Scolari kocha wa Brazil kuwa angepewa nafasi ya pili ya kucheza na timu nzuri kama ya Ujerumani angeshambulia lakini pia angepaki mabasi ili asifungwe magoli ya aibu 7 kwa nunge kama yale Brazili iliyofungwa kwenye kombe la dunia la 2014
Kwa ufupi falsafa ya Mou siku zote itaonekana mbovu kwa timu mbovu na itaonekana nzuri kwa timu nzuri. Na kwa bahati mbaya falsafa zote hata hii ya Pep inakuwa mbaya kwa timu mbovu na inakuwa nzuri kwa timu nzuri.
Wewe huwezi kufikiri kwa falsafa hiyo hiyo Chelsea ya 2004 na 2005 jumlisha ile ya 2014 ilikuwa sio tu timu iliyokuwa ikicheza mpira bali pia iliyovunja rekodi nyingi za EPL ambazo baadhi ya rekodi sasa ndio inataka kuvunjwa na Man City
falsafa ya Mou ndio hamjaielewa na sidhani kama mtaielewa. Falsafa za mpira hutofautiana kutoka kocha kwenda kocha mwingine. Kocha wa kaliba ya Mou hawezi kuja Man United halafu nyie ndio mumpe formation ya kucheza. Kama hamkutaka falsafa yake mabosi waliompa mkataba walijua fika nini Mou anawaza na atafanya nini.Najitoa rasmi kwenye mjadala kuhusu mourinho .. Nimeeeleza saaaaaaaana kwa kina kuhusu unsuitability ya Mourinho pale Manchester united ....
Naona watu Wengine mnajikita kwenye vikombe alivyotupa Mourinho kama sababu ya ubora na asitimuliwe.. Come oooooooon
Wenger hajawahi kuwapa arsenal vikombe ,hivi mnaikumbuka unbeaten run ya arsenal kubeba ubingwa bila kufungwa ???
Carlo anchelot alipigwa chini Bayern Munich alikuwa hajawapa vikombe??
Huyo Jose Mourinho alipigwa chini Chelsea na Madrid alikuwa hajawapa vikombe ??..
Hivi Claudio Raniel kocha wa zamani wa Leicester city alivyofukuzwa alikuwa hajawapa ubingwa leiciter city ????
Unamtambua Manuel Pellegrin kocha wa zamani wa man city , hakuwahi kuwapa vikombe the cityzens???
Hivi unadhani Ferguson kabla ya kustaafu hakuwahi kupitia kashikashi za kufukuzwa baada ya vipindi flan vigumu???
Futa hayo Mawazo kuwa kocha kuchukua vikombe ni kikwazo cha kocha kutofukuzwa. Kocha hudumu kikosini kwa sababu ya "Good existing Performance" Basiiiiiii hizo record hazina maana timu inapokuwa haichezi vizuri na haina muelekeo wa kuchukua vikombe.
Mimi hata sikuelewi unaposema utamlaumu Mourinho ila hutamlaumu kwa kumuona Smalling akiwa kikosini.
Sasa ndugu yangu kama kocha anamuweka benchi Marcus Rojo na kumuanzisha Smalling huoni kama hizi ni shutuma za kutupiwa Mourinho???? Kama wewe na Mimi tunaona kasoro za Smalling na kocha bado anazidi kumuamini Nani wa kulaumiwa ???
Ni kweli tupo UEFA, FA na EPL tuko Nafasi ya pili , ila tambua ligi bado inaendelea na kwa kiwango hiki Mimi binafsi siamini kama tutamaliza Nafasi ya pili EPL. First Leg ya UEFA vs Sevila imeshatuonesha uelekeo wa team yetu. Siioni Timu ikifika Fainali UEFA. Sidhani kama tuna ubavu wa kuwa na msuli wa kuwazuia Madrid,Mancity au Bayern. Kubali au kataa. Kikombe pekee tulicho na uwezo wa kukichukua msimu huu ni FA.
Nawakumbusha tena na tena na tena na tena .... Mourinho hana uwezo wa kimbinu kuivusha team yetu kufika pale tunapotaka ifike.
Muda utaamua kwa sababu mpira ni mchezo wa Wazi