Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hakuna kitu hapa..tunachapwa tena. Kwa namna yoyote huwezi kuniambia Martial anamuweka benchi Mata. Upuuuzi huu.
 
hamna ki2 hapo ! huyo young,smalling na martial kutokea kulia watazingua sn
Smalling yuko vizuri sana..mechi tatu za mwisho amecheza VIZURI SANA.,huwezi kwa namna yoyote kumuweka nje eti acheze Baily ambaye katokea majeruhi ya muda mrefu. Young ni mzuri ni mkongwe mechi ngumu hizi huwa anakuwa mgumu sana, naona ndio pekee anamkaribia Valencia.
 
Hakuna kitu hapa..tunachapwa tena. Kwa namna yoyote huwezi kuniambia Martial anamuweka benchi Mata. Upuuuzi huu.

Hivi mkuu Martial alikukosea nini? "achana na kumweka benchi Mata"
 
Hivi mkuu Martial alikukosea nini? "achana na kumweka benchi Mata"
Ni mchezaji wa kawaida sana kiwango kidogo, utoto mwingi na kibaya zaidi tabia yake ya kusimama kule mbele wakati wenzake wanakaba mipira chini. Anaetakiwa kubaki pale mbele ni Lukaku peke yake lakini pamoja na hayo huwa anarudi nyuma kusaidia na kuchukua mipira.
 
Kama matatizo yake ni hayo, si yanatatulika lakini

Vipi kuhusu mchango wake kwenye timu? au hana
 
Kama matatizo yake ni hayo, si yanatatulika lakini

Vipi kuhusu mchango wake kwenye timu? au hana
Hana mchango mpaka sasa dakika ya 14 beki Young kashapanda na kupiga krosi mbili (ingawa zilikuwa mbovu) yeye yuko pale kama winga anarukaruka tu hajafanya chochote Beki anatoka nyuma anakuja kumpiku!!!
 
Man U hatuna Timu ya kucheza na Big Team huo ndio ukweli tuache Siasa kweny soka, Soka ni Mipango na Hamasa sasa kama sisi hatuna mipango hata hamasa ya wachezaji haipo naona Top 4 tunaiaga taratibu.

Hili Likocha bora hata lipate likizo.
 
Napita kimya kimya kwanza...
Ila baadae kidogo(kama mtapata kipigo) nitakuja na "spade" kufukua makaburi..!
Kwa wale msiotaka kuniona humu ndani ni vyema mkaniweka kwa ignore list mapema kabisa..!
 
Back
Top Bottom